kahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 11 Oct 2026 05:19:22
Four dead and thousands without power after Hurricane Isaias lashes US
Four people died and hundreds of thousands are without power after Hurricane Isaias battered parts of the southern US with powerful winds and heavy rain. Officials reported two deaths each in the states of Alabama and Florida, which included people who were killed when trees fell on their houses. An estimated 500,000 people in total [...] The post Four dead and thousands without power after Hurricane Isaias lashes US appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 11 Oct 2026 05:21:41
Twelve killed and 300 injured in attack on airport in Saudi capital Riyadh
At least 12 people have been killed and 309 injured in an attack on an airport in the Saudi capital Riyadh, local authorities say. The deaths included four Saudis, two people from Bangladesh and one person each from the US, Jordan, Palestine, Syria, Sudan and Egypt, the Saudi civil aviation authority said. Operations at King [...] The post Twelve killed and 300 injured in attack on airport in Saudi capital Riyadh appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 11 Oct 2026 05:24:00
US justice department investigates TV networks over Trump pool coverage
The US justice department (DoJ) says it is investigating several television networks over whether they broke federal competition laws when they recently suspended pool coverage of President Donald Trump. The agency has asked ABC, CBS, CNN, NBC and Fox News to hand over communications related to the White House TV pool, a system where networks [...] The post US justice department investigates TV networks over Trump pool coverage appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 11 Oct 2026 05:27:56
Drone strike by Sudan paramilitary kills 41 near Ethiopian border, rights group says
A drone attack by Sudans paramilitary forces has killed 41 people in the countrys Blue Nile region bordering Ethiopia, a rights group has said. The strike by the Rapid Support Forces (RSF) targeted a camp for displaced people in the states Abu Shandi area on Friday, Emergency Lawyers said. The UN Office for the Co-ordination [...] The post Drone strike by Sudan paramilitary kills 41 near Ethiopian border, rights group says appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 11 Oct 2026 04:55:46
El Niño: Wakenya milioni 1.5 wako hatarini katika maeneo haya
Nairobi, Kisumu, Busia na Mandera ni miongoni mwa kaunti zilizo katika hatari kubwa ya kukumbwa na athari za mvua ya El Niño, kulingana na Kituo cha Kitaifa cha Operesheni za Kukabiliana na Majanga (NDOC). Kati ya kaunti 18 zinazokabiliwa na uwezekano wa majanga kutokana na utabiri wa mvua nyingi kuliko kawaida, serikali imetambua kaunti hizo nne kuwa miongoni mwa zinazoweza kuathirika zaidi. Wakati huohuo, takriban watu milioni 1.5 wanatarajiwa kuathiriwa na mvua hiyo, huku serikali ikikadiria kuwa watu 500,000 wanaweza kulazimika kuhama makazi yao. Mkurugenzi wa NDOC, Kanali David Samoei, alisema serikali imepatia kaunti hizo nne kipaumbele na inaendeleza hatua za kuzuia au kupunguza athari za majanga yanayoweza kutokea. Alisema serikali imekuwa ikijiandaa tangu Idara ya Hali ya Hewa nchini itoe tahadhari kuhusu uwezekano wa kunyesha kwa mvua nyingi kuliko kawaida katika kipindi cha Oktoba, Novemba na Desemba. "NDOC imeangazia zaidi Nairobi na kufanya mazoezi ya kujiandaa kukabiliana na majanga. Kaunti ya Kisumu pia huenda ikaathirika zaidi kutokana na Mto Nyando, na kwa sasa tunafanya kazi katika kingo za mto huo," alisema Kanali Samoei. Aliongeza kuwa Busia huenda ikaathirika kutokana na Mto Nzoia na eneo la Budalangi, ambako maafisa wa serikali wanaendelea na maandalizi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Rasilimali za Maji. "Mandera inaweza kukumbwa na changamoto iwapo barabara inayounganisha Mandera na Wajir itafunikwa na maji ya mafuriko," alisema. Kanali Samoei alisema serikali imejiandaa vya kutosha, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu athari zinazoweza kusababishwa na El Niño na hatua za usalama zinazopaswa kuchukuliwa. Alisema NDOC imeratibu vituo vya uokoaji na makazi salama na serikali za kaunti, ambavyo vitatumika iwapo majanga yatatokea. "Tunathibitisha kuwa Idara ya Hali ya Hewa imekuwa ikitoa utabiri sahihi katika siku za hivi karibuni. Kwa hivyo, tulichukulia tahadhari yake kwa uzito na kuanza maandalizi. "Tumeendesha mazoezi ya kujiandaa kukabiliana na majanga katika maeneo ya Nairobi, Garissa na Naivasha. Lengo letu ni kuhakikisha hakuna maisha yatakayopotea katika kipindi hiki kwa kuchukua hatua mapema baada ya kupokea taarifa kutoka kwa idara hiyo," alisema. Kanali Samoei alikuwa akizungumza katika kongamano la siku tatu lililofanyika Nakuru, lililowaleta pamoja wataalamu na wadau kujadili namna ya kujiandaa kukabiliana na majanga. Waliohudhuria ni pamoja na mashirika ya kibinafsi, taasisi na mashirika ya serikali pamoja na wasomi, ambao walitarajiwa kubadilishana mawazo kuhusu maandalizi ya kukabiliana na majanga. Baada ya kongamano hilo, washiriki wataadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Hatari za Majanga (IDDRR) Oktoba 13. Kanali Samoei aliwahakikishia wananchi kuwa serikali inachukua hatua za kulinda usalama wao, huku akiwashauri kufuata miongozo itakayotolewa mara kwa mara na kamati ya usimamizi. "Serikali imetenga rasilimali za kutosha kukabiliana na majanga hayo, huku ikitarajia pia kupata msaada kutoka kwa washirika na sekta ya kibinafsi iwapo kutatokea tatizo," alisema. Naibu Gavana wa Nakuru, David Kones, aliyeshiriki kongamano hilo, alisema serikali ya kaunti imekuwa ikielimisha wakazi kuhusu umuhimu wa kuchukua hatua za kuzuia majanga kuanzia ngazi ya familia.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Sun, 11 Oct 2026 04:10:00
'They wanted to eliminate him': How Raila's car was sprayed with 11 bullets in assassination attempt
Ogeta tells of how violent rallies were the bane of Railas existence and how, on multiple occasions, such situations put his life in harms way.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 11 Oct 2026 03:55:18
Sifuna afichua mikakati yake kisiasa kuelekea uchaguzi wa 2027
Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna anapania kujenga vuguvugu jipya la kisiasa linalozingatia Katiba, uwajibikaji na uchumi unaowajali wananchi, huku akijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa Agosti 2027. Chama chake kipya, The Equitable Party (TEP), kinatarajiwa kubadilishwa jina na kuitwa Linda Mwananchi Movement kufuatia uamuzi wa Kamati Kuu ya Kitaifa (NEC) mnamo Oktoba 8, 2026. Mbali na jina, chama hicho kinapanga kubadilisha katiba yake, rangi rasmi, nembo na kuhamisha makao makuu yake. Hatua hizo zinaashiria juhudi za Bw Sifuna kujijenga upya baada ya kutengana na ODM alikohudumu kama katibu mkuu kwa karibu miaka kumi. Hata hivyo, msimamo wake kuhusu kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua mwaka 2024 unaweza kuibua maswali anapojaribu kuunganisha upinzani dhidi ya Rais William Ruto. Akizungumza na wanahabari jijini Nairobi Ijumaa, Bw Sifuna alitetea jukumu lake katika mchakato huo, akisema haupaswi kuzuia viongozi waliokuwa na tofauti kushirikiana katika uchaguzi ujao. Alipoulizwa jinsi atakavyoshirikiana na Bw Gachagua, ambaye sasa anaongoza chama cha DCP, alisema: "Tayari nilimuondoa madarakani kwa makosa yake. Kwa hivyo, hamuwezi kuniuliza maoni yangu kuhusu makosa ambayo tayari nilimwadhibu." Bw Gachagua ametangaza kuwa yuko tayari hata kuwa naibu wa Bw Sifuna ikiwa upinzani utaamua kuwa seneta huyo ndiye anayefaa zaidi kumshinda Rais Ruto. Hata hivyo, amewahi kuwakashifu viongozi wa Mlima Kenya walioshiriki kumuondoa madarakani, akiwataja kuwa wasaliti. Bw Sifuna hakutaja chama atakachoungana nacho wala kueleza namna mgombea mmoja wa upinzani atakavyochaguliwa. Alisema mazungumzo hayo bado hayajafika wakati wake. "Subirini kwanza. Mazungumzo hayo yatafanyika baadaye sana," aliwaambia wanahabari. Wakili Nelson Osiemo alisema Bw Sifuna atalazimika kueleza jinsi uamuzi wake kuhusu Gachagua unavyoendana na misingi ya kisiasa anayotaka kuweka mbele katika vuguvugu lake jipya. Bw Sifuna anasisitiza kuwa uwajibikaji na kuheshimu Katiba lazima viwe msingi wa uongozi. Alisema utendaji wa rais haupaswi kupimwa kwa miradi inayoonekana pekee, bali pia kwa namna serikali inavyofuata sheria. Akizungumzia deni la taifa na matumizi ya fedha za umma, alisisitiza umuhimu wa uwazi, ushirikishaji wa wananchi na ukopaji unaofuata sheria. "Hauwezi kusema kwamba kwa sababu umejenga uwanja mzuri wa Talanta, basi tukupigie makofi. Hapana. Tunataka uwazi," alisema. Msimamo huo unajiri baada ya miezi kadhaa ya migogoro ndani ya ODM kuhusu ushirikiano wake na serikali jumuishi pamoja na mwelekeo wa chama hicho baada ya kifo cha Raila Odinga. Bw Sifuna alisema alijaribu kupatanisha makundi hasimu lakini akahitimisha kuwa uongozi wa chama ulikuwa ukielekea upande ambao hangeweza kuutetea. Alikosoa ushirikiano wa ODM na UDA akisema unatishia uhuru wa chama, na pia akapinga mchakato wa kuondolewa kwake kama katibu mkuu. Hata hivyo, alisema hana kinyongo na aliyekuwa wenzake na anaiachia hatima ya ODM kwa wapigakura. Alisema timu yake pia inatayarisha sera za kupunguza matumizi mabaya ya fedha za serikali na kupunguza mzigo wa kodi kwa wananchi. Katika elimu, anataka data sahihi za wanafunzi, shule na walimu ili kuimarisha usimamizi wa fedha, huku katika afya akipendekeza hospitali zilipwe madai halali kwa wakati na hatua zichukuliwe dhidi ya madai ya ulaghai. Alisema manifesto ya vuguvugu hilo inaandaliwa kwa usaidizi wa wataalamu na itakaguliwa kabla ya kuchapishwa. Bw Sifuna alisema ataruhusu wapigakura kuamua mustakabali wa ODM katika uchaguzi wa Agosti 11, 2027.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 11 Oct 2026 02:55:21
Dalili Kalonzo anarukwa na vinara wa upinzani kuhusu Ukombozi Alliance
Juhudi za Kalonzo Musyoka kubadilisha jina na muundo wa muungano wa Azimio la Umoja kuwa The Ukombozi Alliance (TUA) zinaweza kumweka katika nafasi nzuri ya kuwania urais kwa tiketi ya upinzani au kumtenga na viongozi wengine kuelekea uchaguzi wa 2027. Kalonzo, ambaye anaongoza chama cha Wiper, amekuwa mstari wa mbele katika kuunda upya muungano huo baada ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, aliyekuwa kiongozi wake. Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa upinzani wanapinga kujiunga na TUA, wakisema wanataka kuhifadhi utambulisho wa vyama vyao na kuunda muungano mpya. Chama cha DCP kinachoongozwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na vuguvugu la Linda Mwananchi linalohusishwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna vimeonyesha kusitasita kujiunga na TUA. Bw Sifuna alisema chama chake kipya, The Equitable Party, kinapanga kubadilishwa jina na kuitwa Linda Mwananchi Movement kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu miungano. "Kwa sasa chama changu kinafanyiwa mabadiliko makubwa. Tuna miundo ya kuweka na makataa ya Tume ya Uchaguzi na Msajili wa Vyama vya Kisiasa ya kuzingatia. Mazungumzo kuhusu miungano yatakuja baadaye," alisema. Kalonzo naye amewataka wabunge wa Wiper walioonekana kushirikiana na Bw Sifuna kuzingatia shughuli za chama chao. Alitaja Mbunge wa Kaiti Joshua Kimilu na mwenzake wa Wundanyi Danson Mwashako. Hali hii inaashiria ushindani wa kutafuta uungwaji mkono mashinani na udhibiti wa vyama huku viongozi wakijaribu kuungana kumuondoa Rais William Ruto madarakani katika uchaguzi mkuu ujao. Naibu kiongozi wa Jubilee Jeremiah Kioni alisema chama hicho hakina haraka ya kujiunga na TUA, akisema upinzani unahitaji mawazo mapya. Alisema baadhi ya wanasiasa waliounga mkono mgombea wa Azimio katika uchaguzi wa 2022 walipata hasara kisiasa katika maeneo yao, na hawako tayari kujitolea tena kwa mpangilio kama huo. Hata hivyo, viongozi wa Democratic Party Justin Muturi na wa DAP-K Eugene Wamalwa wameunga mkono TUA kama chombo kinachoweza kumshinda Rais Ruto. Wote wamekuwa wakifanya kampeni pamoja na Kalonzo, ambaye wanamchukulia kama mgombeaji anayefaa kupewa tiketi ya urais. Mzozo huo unatokana na kipengele cha makubaliano ya muungano ambacho awali kilionekana kumpa kiongozi wa chama nafasi ya moja kwa moja kuwa mgombea urais. Washirika wa Kalonzo wanasema kipengele hicho kimebadilishwa na sasa wanachama wote wanaweza kuwania tiketi hiyo. Kalonzo pia amesisitiza kuwa kujiuzulu kwa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kama mwenyekiti wa baraza la muungano hakujasababisha pengo la uongozi ndani ya TUA. Kuna juhudi za kumshawishi Bw Gachagua achukue nafasi ya Bw Kenyatta ili kuvutia DCP kujiunga na muungano huo. Gavana wa Siaya James Orengo, ambaye anahusishwa na Linda Mwananchi, pia ametajwa kama anayeweza kupewa nafasi hiyo ili kuvutia wafuasi wa Nyanza. Hata hivyo, Mbunge wa Gatanga Edward Muriu, mshirika wa Bw Gachagua, alisema DCP inataka kwanza kuimarisha uungwaji mkono wake kabla ya kujadiliana na vyama vingine kuunda muungano mkubwa. Mchambuzi wa siasa Profesa David Monda alisema TUA inaweza kuwa vigumu kupata uungwaji mkono wa kutosha bila kuwashirikisha Kalonzo, Sifuna, Gachagua na aliyekuwa Waziri wa utawala wa ndani Fred Matiang'i katika mpangilio mmoja. Alisema viongozi hao wanapaswa kuungana ili kumshinda Rais Ruto au kuhatarisha kushindwa kila mmoja akigombea urais kivyake. Wanaounga mkono TUA wanataka muungano huo uige mfano wa National Rainbow Coalition (Narc), uliomuingiza Mwai Kibaki mamlakani mwaka 2002. Chini ya mfumo huo, vyama havikuvunjwa lakini viliunga mkono mgombea mmoja wa urais na ajenda ya pamoja. Lengo ni kuzuia upinzani kugawanyika na kumpa Rais Ruto nafasi ya kushinda uchaguzi wa 2027.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 10 Oct 2026 20:25:38
9 people killed, including 2 children, in mass shooting in northern Pennsylvania
Nine people, including two children, are reported dead after a mass shooting and an hours-long standoff in Erie. According to CBS affiliate Erie News Now, police were called to Perry Street around 5 p.m. on Friday after witnesses reported seeing a man firing a gun before he entered a home. Two women were found dead [...] The post 9 people killed, including 2 children, in mass shooting in northern Pennsylvania appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 10 Oct 2026 20:31:07
Several injured in attack on airport in Saudi capital Riyadh
Several people were injured in another attack on an international airport in the Saudi capital Riyadh, authorities say, days after Yemens Houthis claimed to have carried out similar strikes on the hub. Operations at King Khalid International Airport in Riyadh were suspended on Saturday after the attack, the Saudi Civil Aviation Authority said in a [...] The post Several injured in attack on airport in Saudi capital Riyadh appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 10 Oct 2026 20:09:26
Cape Media appoints June Ndinya acting CEO, Keneth Kazungu acting Editor-in-Chief
Cape Media, the parent company of TV47, Radio 47 and Cape Studios, has appointed June Akinyi Ndinya as acting Chief Executive Officer (CEO) and Keneth Kadzomba Kazungu as acting Editor-in-Chief following the exit of their predecessors. The Board of Directors announced the leadership changes on Saturday, October 10, 2026, saying the appointments would take effect [...] The post Cape Media appoints June Ndinya acting CEO, Keneth Kazungu acting Editor-in-Chief appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content