taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Fri, 02 Oct 2026 08:55:01
Balaa kaunti ikikosa jaa la taka
WAKAZI wa mji wa Bomet wanakabiliwa na tatizo kubwa baada ya kaunti hiyo kukosa jaa rasmi la kutupa taka. Hali hiyo imesababisha mapipa ya taka katika sehemu mbalimbali za mji kurundika uchafu huku harufu mbaya ikisumbua wakazi na wafanyabiashara. Tatizo hilo lilizuka baada ya jaa la muda lililokuwa likitumika kwa miaka 12 karibu na nyumba 220 za bei nafuu kufungwa kabla ya ziara ya Rais William Ruto mnamo Septemba 4. Inadaiwa kuwa eneo hilo lilifungwa kwa idhini ya Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Mazingira (Nema). Mkurugenzi wa Nema katika Kaunti ya Bomet, Richard Kering, alikiri kuwa mji huo hauna jaa lililoidhinishwa rasmi. Alisema serikali ya kaunti imekuwa ikichelewesha kutenga eneo linalokidhi masharti ya mazingira. Kutokana na ukosefu wa jaa, wafanyakazi wa kaunti wamekuwa wakichoma taka usiku ili kupunguza mrundikano wa taka katika mapipa ya mji. Mwenyekiti wa tawi la Bomet la Chama cha Wafanyabiashara nchini Kenya, Leonard Langat, alionya kuwa hali hiyo ni janga linalosubiri kulipuka, hasa wakati huu ambapo mvua ya El Niño inatarajiwa kuanza mwezi ujao. Wanafunzi wa Bomet University pia wamepinga mpango wa kuanzisha jaa jipya karibu na chuo hicho na Mto Nyangores, ambao ni chanzo muhimu cha maji kwa wakazi na wanafunzi. Gavana Hillary Barchok amekiri kuwa kaunti hiyo inakabiliwa na tatizo la afya ya umma na kusema juhudi zinaendelea kutafuta suluhisho la kudumu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Fri, 02 Oct 2026 07:55:08
Wakazi wafidiwa Sh350 milioni kwa madhara ya jaa la taka
MAHAKAMA ya Mazingira na Ardhi imeamuru Serikali ya Kaunti ya Mombasa kuwalipa zaidi ya wakazi 200 wa eneo la Mwakirunge fidia ya Sh350 milioni kutokana na ukiukaji wa haki yao ya kuishi katika mazingira safi na salama uliosababishwa na uchafuzi kutoka jaa la taka eneo hilo. Katika uamuzi wake, Jaji Lucas Naikuni alisema wakazi hao, wakiongozwa na mwanaharakati wa mazingira Ainea Ragen, walithibitisha kuwa jaa hilo limekuwa likasababisha madhara ya muda mrefu kwa maisha yao. Jaji huyo alibaini kuwa Serikali ya Kaunti ya Mombasa pamoja na Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Mazingira (NEMA) walishindwa kuchukua hatua za kutosha kuzuia na kudhibiti uchafuzi wa mazingira unaotokana na shughuli za jaa la Mwakirunge. "Jaaa la Mwakirunge limekuwepo kwa muda mrefu na bado linaendelea kufanya kazi hadi leo. Hivyo basi haki ya wakazi ya kuishi katika mazingira safi na yenye afya inaendelea kukiukwa," alisema jaji huyo. Mahakama ilisema ushahidi uliowasilishwa ulionyesha kuwa hatua na uzembe wa maafisa ulisababisha madhara ya kimazingira na kukiuka Kifungu cha 42 cha Katiba, kinachohakikisha kila mtu ana haki ya mazingira safi na yenye afya. Mbali na fidia hiyo, mahakama pia imeamuru kaunti hiyo kuanza mara moja ujenzi wa ukuta wa simiti kuzunguka jaa hilo. Ukuta huo unatakiwa kuwa na urefu wa angalau mita sita, uwe na milango salama ya kuingilia na kutoka. Kaunti imepewa muda wa miezi 12 kukamilisha kazi hiyo na pia kuweka walinzi wa kutosha pamoja na mfumo wa kudhibiti watu wanaoingia katika eneo hilo. Aidha, mahakama imeagiza serikali ya kaunti kuandaa na vifaa vya kisasa vya kuchoma taka vinavyokidhi viwango vya kimataifa vya afya na usalama. Hata hivyo, jaji alikataa ombi la wakazi kutangaza kipande hicho cha ardhi ya ekari 50 kuwa ardhi ya jamii, uamuzi uliomaanisha kuwa jaa hilo halitahamishwa kwa sasa.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Fri, 02 Oct 2026 07:55:08
Teknolojia itasaidia wakulima kukabili mabadiliko ya tabianchi, waziri
Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo Mutahi Kagwe amewataka wakulima nchini kutumia teknolojia, huduma za kidijitali na mbinu za kilimo zinazozingatia mabadiliko ya tabianchi ili kukabiliana na hali ya hewa isiyotabirika, gharama kubwa ya uzalishaji na kupungua kwa rutuba ya ardhi. Akizungumza Jumatano wakati wa ufunguzi rasmi wa Maonesho ya 125 ya Kimataifa ya Biashara ya Nairobi katika Uwanja wa Jamhuri, Kagwe alisema teknolojia inaweza kuwasaidia wakulima kufanya maamuzi bora kuhusu mazao ya kupanda, wakati wa kupanda, pembejeo za kutumia na masoko ya kuuza mazao yao. Alisema mustakabali wa sekta ya kilimo hautategemea serikali pekee bali ushirikiano kati ya wakulima, watafiti, wawekezaji, sekta ya binafsi pamoja na serikali za kitaifa na kaunti. Maonesho hayo ya siku saba yaliyoanza Septemba 28 na yatakamilika Oktoba 4 yamewaleta pamoja wakulima, wafugaji, watafiti na kampuni za teknolojia kuonyesha ubunifu mbalimbali chini ya kaulimbiu ya kuendeleza kilimo kinachozingatia tabianchi kwa ukuaji endelevu wa uchumi. Baadhi ya teknolojia zinazoonyeshwa ni matumizi ya Akili Unde (AI), droni, vifaa vya unyunyuzaji, mashine za kilimo, mifugo bora, teknolojia za afya ya mifugo na mbegu za mazao yanayostahimili ukame. Kagwe alisema mabadiliko ya tabianchi, gharama kubwa ya uzalishaji na mahitaji mapya ya soko yanawalazimu wakulima kubadilisha mbinu zao za uzalishaji. Alionya kuwa ukame na mafuriko yanayosababishwa na tabianchi yanagharimu uchumi wa Kenya kiasi kikubwa kila mwaka kupitia hasara ya mazao, mifugo na masoko. Alisema serikali inaimarisha huduma za kidijitali katika sekta ya kilimo ikiwemo usajili wa wakulima, huduma za nyanjani, bima na upatikanaji wa pembejeo. Kulingana naye, takriban wakulima 8.9 milioni tayari wamesajiliwa katika mfumo wa kitaifa wa usimamizi wa taarifa za kilimo. Waziri huyo pia alisisitiza umuhimu wa kupima afya ya udongo kabla ya kutumia mbolea. Alisema asilimia 63 ya udongo nchini una kiwango kikubwa cha asidi, hali inayopunguza uzalishaji. "Ni makosa kutumia pembejeo bila kufanya uchunguzi wa kisayansi wa hali ya udongo," alisema. Wakati huo huo, serikali imeanzisha mradi wa kitaifa wa uchunguzi wa udongo kwa njia za kidijitali kwa ushirikiano na Shirika la Utafiti wa Kilimo na Mifugo Kenya (KALRO). Kagwe aliongeza kuwa serikali inawekeza katika afya ya mifugo, mbegu bora, uzalishaji wa maziwa na upanuzi wa masoko ya nyama na bidhaa nyingine za mifugo ili kuongeza mapato ya wakulima. Aliwataka wakulima, wawekezaji na wadau wengine kutumia maonesho hayo kuunda ushirikiano na kupanua matumizi ya teknolojia zinazoweza kuongeza uzalishaji wa chakula na kuboresha mapato katika sekta ya kilimo.
read morekenyanews.go.ke
@kna Fri, 02 Oct 2026 07:42:40
The Moth returns to Nairobi for the seventh year with five powerful stories
The Moth, the world-renowned nonprofit organisation dedicated to the art of live personal storytelling, returns to Nairobi on Saturday, 7 November 2026, for its seventh Mainstage event in the city, once again hosted by Kenyan media entrepreneur and women's rights advocate Adelle Onyango. Staged at the Catholic University of Eastern Africa's LRC Auditorium, the evening...
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 02 Oct 2026 07:18:11
How to Improve Speech Delay in a 4-Year-Old
Speech and language development is an important part of a childs learning, social interaction and emotional development. If a 4-year-old is having difficulty speaking clearly, forming sentences, answering simple questions or communicating their needs, parents and caregivers can support language development through everyday activities. Learning how to improve speech delay in a 4-year-old involves encouraging [...] The post How to Improve Speech Delay in a 4-Year-Old appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 02 Oct 2026 07:25:50
Woman dies after falling into water tank at Kariobangi South construction site
A 50-year-old woman died after falling into an underground water tank at a construction site in Kariobangi South, Nairobi. The woman, identified as Thabita Nduta, had been working at the construction site for about two months when the incident occurred on Thursday morning. According to police, Nduta slipped and fell into an underground water tank [...] The post Woman dies after falling into water tank at Kariobangi South construction site appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 02 Oct 2026 07:39:56
KeNHA Announces Partial Closure of Waiyaki Way
The Kenya National Highways Authority (KeNHA) has announced the temporary partial closure of a section of Waiyaki Way (A8 Road) in Nairobi to allow for highway maintenance works. The affected section is between Kempinski and the Museum Hill Interchange on the Mombasa-bound lanes. According to a notice issued by KeNHA Director General Luka Kimeli, the [...] The post KeNHA Announces Partial Closure of Waiyaki Way appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content