taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 28 Sep 2026 03:55:44
Kauli tata ya Kalonzo kuhusu 'uwezekano wa kufanya handisheki na Ruto' yazua gumzo
KIONGOZI wa Wiper Kalonzo Musyoka amezua mjadala kuhusu msimamo wake wa kisiasa baada ya kuonyesha dalili ya kuwa atashiriki handisheki na Rais William Ruto upinzani ukishindwa uchaguzi wa 2027. Bw Musyoka amesisitiza kuwa siasa za ushindani kati ya Rais Ruto na vinara wa upinzani inastahili kuzingatia masuala yanayohusisha maslahi ya nchi badala ya uhasama wa kisiasa. "Ukitushinda, tunaweza kutathmini ukiwa na tabia nzuri. Tukikushinda, tutaangalia masuala haya yote. Tuangaliane kwa sababu tuna nchi na Mungu haheshimu binadamu licha ya hadhi yake," akasema Bw Musyoka. Bw Musyoka alikuwa akizungumza jana katika Kaunti ya Siaya ambayo ni ngome ya kisiasa ya marehemu kigogo wa siasa za upinzani Raila Odinga. Hatua ya kinara huyo wa Wiper kumsifu Rais Ruto imeibua mjadala kuhusu mahali ambapo uaminifu wake wa kisiasa upo. Siku tatu zilizopita alimsifu Rais kwa kujenga barabara inayoelekewa kwake Tseikuru. "Bw Ruto kwa sababu ya kuogopa sisi ameweka bidii barabara ifike Tseikuru na namwambia awekee bidii imechelewa kwa sababu barabara hiyo ingekuwa imefika Maua. Bw Ruto anatumiwa na Mungu kwa njia spesheli. Kuweka hiyo bidii si Ruto ni Mungu. Kufikia Agosti mwaka tukikuja nyumbani itakuwa imekaribia sana," akasema Bw Musyoka wakati wa Ukumbusho wa miaka 20 tangu mauti ya mamake. "Sasa tuna chuo cha kitaifa cha kiufundi baada ya kuongea na Ruto. Tunakubali kuwa hii inafaa kuwa chuo cha kitaifa cha kiufundi," akaongeza. Kauli ya Bw Musyoka imekuja wakati ambapo kuna kutoaminiana ndani ya upinzani huku Rais Ruto akitumia kauli za kiongozi huyo wa Wiper kumkejeli na kusema kuwa ni kati ya viongozi wanayemtambua kazi yake. Aidha Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki miezi ya nyuma amekuwa akimsifu Bw Musyoka na kumrejelea kama kiongozi muungana ambaye anastahili kuungana na serikali ili kuwafanyia Wakenya kazi. Jana Bw Musyoka pia aliitaka serikali kuelekeza nguvu kwa wapinzani watakaokuwa kwenye debe badala ya kumlenga Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 28 Sep 2026 03:29:31
Kris Kristofferson Net Worth
Kris Kristofferson was an American singer, songwriter and actor who had an estimated net worth of $50 million at the time of his death in 2024. He built his wealth through a long career in music, songwriting, acting, recording and live performances. Kristofferson became one of the most respected songwriters in country music, writing songs [...] The post Kris Kristofferson Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 28 Sep 2026 03:37:42
Machine Gun Kelly Net Worth
Machine Gun Kelly, also known as MGK or mgk, is an American musician, rapper, singer, songwriter, actor, and entrepreneur who has an estimated net worth of $35 million. Born Colson Baker, MGK first gained attention as a rapid-fire rapper from Cleveland before becoming one of the most versatile artists of his generation. His career has [...] The post Machine Gun Kelly Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 28 Sep 2026 03:45:17
Yelawolf Net Worth
Yelawolf has an estimated net worth of $4 million. The American rapper, whose real name is Michael Wayne Atha, built his wealth through music, album sales, touring, collaborations, and other entertainment projects. He first gained widespread attention with his 2010 mixtape "Trunk Muzik" before signing with Eminem's Shady Records in 2011. Yelawolf went on to [...] The post Yelawolf Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 28 Sep 2026 03:06:31
Merle Haggard Net Worth
Merle Haggard had an estimated net worth of $5 million at the time of his death in 2016. The American country singer, songwriter and musician built his fortune through a career that spanned more than five decades and produced dozens of chart-topping songs. Known by the nickname "The Hag," Haggard became one of the most [...] The post Merle Haggard Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 28 Sep 2026 03:13:36
Waylon Jennings Net Worth
Waylon Jennings was an American country music singer, songwriter and musician who had an estimated net worth of $2 million at the time of his death in 2002. He became one of the defining figures of the outlaw country movement, a style that challenged Nashvilles traditional approach to country music in the 1970s. Jennings built [...] The post Waylon Jennings Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 28 Sep 2026 03:20:28
Jessi Colter Net Worth
Jessi Colter is an American country music singer and songwriter who has an estimated net worth of $5 million. She became one of the most recognizable female artists associated with the outlaw country movement of the 1970s, a genre closely linked to her second husband, country music star Waylon Jennings. Colter achieved her biggest commercial [...] The post Jessi Colter Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Mon, 28 Sep 2026 03:00:00
Vote smuggling: Registration bureau, IEBC on the spot as Ugandans issued IDs and voters cards
As Kenya inches towards the 2027 General Election, questions over the integrity of the voters roll are emerging along the Kenya-Uganda border,
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 28 Sep 2026 02:58:35
Willie Nelson Net Worth
Willie Nelson has an estimated net worth of $20 million. The American country music singer, songwriter, actor, author and activist has built his fortune through a career spanning more than six decades. Nelson is one of the most recognizable figures in American music and one of the leading pioneers of the outlaw country movement. His [...] The post Willie Nelson Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 28 Sep 2026 02:55:33
Wantam! Sifuna aidhinishwa na Linda Mwananchi kupambana na Ruto 2027
HATUA ya Linda Mwananchi kumuidhinisha rasmi Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kuwa mgombea wake wa urais, inaonekana kufunga mlango kwa azma ya Gavana wa Siaya James Orengo kuwania uongozi wa nchi kupitia vuguvugu hilo. Katika mkutano huo wa Jumamosi, viongozi wakuu wa vuguvugu hilo waliamua kumuunga Seneta Sifuna huku wakisaka muungano mkubwa wa upinzani kuelekea kwa Uchaguzi Mkuu wa 2027. "Leo (Jumamosi), tulikutana kama uongozi wa Linda Mwananchi na kuamua kusonga mbele pamoja, tukiwa tumeunganishwa na lengo moja la kujibu wito wa Wakenya wanaotafuta utawala bora na kuikomboa nchi. "Pia tuliamua kwamba Edwin Watenya Sifuna ndiye kiongozi wetu na mgombea wetu wa urais," ikasema taarifa ya vuguvugu hilo. Mkutano huo ulihudhuriwa na Bw Sifuna, Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, Seneta wa Kakamega Boni Khalwale, Seneta wa Kisii Richard Onyonka, Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi na Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi. Wengine waliohudhuria ni Mbunge wa Funyula Wilberforce Oundo, Anthony Kibagendi (Kitutu Chache Kusini), Clive Gisairo (Kitutu Masaba), Gavana wa zamani wa Meru Kawira Mwangaza na aliyekuwa rais wa Chama cha Wanasheria Nchini (LSK) Faith Odhiambo. "Orengo alituma udhuru lakini sote tulikubaliana kwamba ni Sifuna pekee atakayeungwa kuwania urais. Hana nafasi sasa kwa sababu wote waliokuwepo walikubaliana kuhusu uwanizi wa Sifuna," akasema Dkt Khalwale. Dkt Khalwale alisema wanachama walijaribu kumshawishi Bw Owino kuwania ugavana wa Nairobi kwa kutumia chama kimoja na Bw Sifuna katika juhudi za kuunganisha ngome zao za kisiasa. "Wengi walimpinga lakini sasa suala hilo ni uamuzi wake kwa sababu yeye alisimama kidete na msimamo wake," akasema Dkt Khalwale. Bw Owino tayari amesajili The Mwananchi Party (TMP), ambayo anakusudia kutumia kuwania ugavana wa Nairobi. Mipango yake ya kisiasa imekuwa ikipingana na juhudi za kupata chama kimoja cha kisiasa, huku Bw Natembeya akisukuma Bw Sifuna kuwania kwa kutumia UDP. Bw Natembeya alisema wiki iliyopita kuwa Bw Sifuna alikuwa tayari kutangaza UDP kuwa chama atakachotumia kuwania urais. Jaribio la awali la kubadilisha jina la UDP kuwa Ukombozi People's Party (UPP) lilikwama baada ya Kiongozi wa Wiper Patriotic Front Kalonzo Musyoka kusajili The Ukombozi Alliance (TUA), hatua iliyotatiza mipango ya vuguvugu hilo kuhusu jina hilo. Linda Mwananchi imetangaza mipango ya kuzindua chama cha Bw Sifuna cha kuwania urais Oktoba 3. Mmoja wa viongozi wakuu waliohudhuria mkutano wa Jumamosi lakini akakataa kutajwa jina alisema kutokuwepo kwa Bw Orengo hakupaswi kuchukuliwa kama ishara ya mgawanyiko ndani ya vuguvugu hilo. "Alisema hangeweza kuhudhuria mkutano lakini tutamuunga mkono Sifuna kama kila mtu alivyokubaliana. Hakuna mgawanyiko kama inavyodaiwa na tunaamini Orengo yuko pamoja nasi katika kumuunga mkono Sifuna," akasema kiongozi huyo. Aliongeza kuwa maandalizi ya uzinduzi wa chama cha Bw Sifuna yalikuwa yamepiga hatua kubwa lakini akakataa kutoa maelezo zaidi. Bw Owino, katika taarifa baada ya mkutano huo, pia alisisitiza umoja ndani ya vuguvugu hilo, akisema lengo la upinzani kushinda serikali linaweza kufikiwa tu kupitia umoja wao. Bw Orengo hakuhudhuria mkutano wa faragha wa Jumamosi ambako uamuzi huo ulifanywa, licha ya kuwa ametangaza hadharani nia yake ya kuwania urais. Viongozi waliohudhuria kikao hicho walisema Bw Orengo alituma udhuru kwa sababu alikuwa na mwanafamilia mgonjwa, na kusisitiza kuwa kutokuwepo kwake hakupaswi kufasiriwa kama ishara ya mgawanyiko. Bw Orengo amekuwa akisisitiza kuwa umoja wa upinzani haupaswi kuzima azma za wagombea wengine na amekuwa akitaka uteuzi huru wa kumpata mgombeaji wa urais wa Linda Mwananchi. "Hakuna tatizo kushindana ndani ya Linda Mwananchi au upinzani. Muhimu ni kuwasilisha wagombea wote kwenye mchakato wa kuaminika wa uteuzi na, mwishowe, tupate mgombea mmoja wa kukabiliana na Rais William Ruto," akasema gavana huyo hapo awali. Jana Taifa Dijitali ilijaribu kubaini sababu ya Bw Orengo kukosa mkutano huo na ikiwa anaunga mkono kuidhinishwa kwa Bw Sifuna, lakini hakujibu jumbe wala kupokea simu. Gavana huyo alitarajiwa Jumapili kuungana na kiongozi wa Jubilee Fred Matiang'i na Kiongozi wa People's Party of Kenya Ndindi Nyoro kwa ibada katika Kanisa la Dominion Olerai kabla ya mkutano wa hadhara mjini Narok.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 27 Sep 2026 20:31:23
Wetang'ula steps up attacks on Uhuru over 2022 election remarks
National Assembly Speaker Moses Wetang'ula has stepped up his criticism of retired President Uhuru Kenyatta over his recent claim that the late former Prime Minister Raila Odinga won the 2022 presidential election. Speaking during a Sunday church service at Hewani Gospel PEFA Church in Garsen Constituency, Tana River County on Sunday , Wetang'ula questioned why [...] The post Wetang'ula steps up attacks on Uhuru over 2022 election remarks appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 27 Sep 2026 20:33:22
Karua announces death of father Jackson Karua
Former Justice Minister and People's Liberation Party (PLP) leader Martha Karua has announced the death of her father, Mwalimu Jackson Karua. In a statement issued on Sunday, Karua said she had travelled to Kirinyaga earlier in the day to visit her father, accompanied by her siblings. The family spent time with him and sang his [...] The post Karua announces death of father Jackson Karua appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 27 Sep 2026 20:36:47
Ruto says expansion of Mzima Springs water project to begin this year
Expansion of the Mzima Springs water project in Taita-Taveta County will commence this year, President William Ruto has announced. He said the Government will mobilise Sh30 billion for the project to tackle perennial water shortages in the county and neighbouring areas. The project, to be financed through the National Infrastructure Fund, will provide water to [...] The post Ruto says expansion of Mzima Springs water project to begin this year appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content