taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sat, 29 Aug 2026 03:55:46
Wafanyabiashara waandamana wakilalamikia ushuru wa juu
BIASHARA ziliathirika jijini Nairobi jana huku wafanyabiashara wadogo wakimiminika barabarani kupinga kile walichokitaja kuwa ongezeko la ushuru na ukadiriaji mpya wa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje uliowekwa na Mamlaka ya Mapato Kenya (KRA). Waandamanaji walikusanyika katika eneo la Archives kabla ya kuandamana kuelekea makao makuu ya KRA katika jengo la Times Tower katikati mwa jiji. Wafanyabiashara hao walisema mabadiliko ya kiwango kinachotumiwa kukadiria thamani ya bidhaa za uagizaji yameongeza gharama za biashara na kupunguza faida zao. Kwa mujibu wao, KRA imepandisha kiwango cha ukadiriaji kutoka 2.5m hadi 3.2m, hatua wanayodai imeongeza kwa kiasi kikubwa kodi inayolipwa kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, hususan kutoka China. Walisema mabadiliko hayo yamesababisha ongezeko la takriban asilimia 28, huku thamani ya bidhaa kwa madhumuni ya kodi ikiongezeka kutoka Sh2.5 milioni hadi Sh3.2 milioni.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Sat, 29 Aug 2026 04:00:00
And tender goes to...: Ruto's family linked to Sh2.8 billion police uniform deal
Questions mount over police uniform supplier Nalitex after its office could not be traced and its registered address links to businesses associated with Rutos family.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sat, 29 Aug 2026 02:55:57
Tahadhari pombe feki ikitamba nchini
YOTE huanza kwa chupa ya pombe ya bei nafuu, chapa inayofahamika au kinywaji kilichonunuliwa katika baa inayoaminika. Kisha huja ladha ya ajabu, kuwasha koo, kutapika, kushindwa kuamka au hata madhara mabaya zaidi. Kote nchini Kenya, watumiaji wa pombe wanaeleza visa vya kunywa vileo wanavyoshuku kuwa ni bandia au vilivyotiwa kemikali hatari. Baadhi yao waliishia hospitalini, wengine wameogopa kunywa tena huku wengine wakibadilisha kabisa aina ya pombe wanazotumia. Visa hivyo vinaendelea kuibuka katika maeneo mbalimbali nchini na hata kusambaa kwenye mitandao ya kijamii huku mamlaka zikijitahidi kudhibiti tatizo hilo. Wiki hii pekee, maafisa kutoka mashirika mbalimbali walinasa mamia ya chupa za pombe zinazoshukiwa kuwa bandia katika maeneo ya Eastleigh na Jericho jijini Nairobi. Operesheni hiyo pia ilifanikisha kukamatwa kwa stampu za ushuru zinazoshukiwa kuwa feki, chupa tupu na vifuniko vya chupa. Katika mtaa wa Eastleigh, jumla ya chupa 868 za vinywaji mbalimbali zilinaswa, huku 315 zikipatikana Jericho. Ripoti ya utafiti mwaka 2025 iliyochapishwa na Mamlaka ya Kupambana na Bidhaa Bandia (ACA) ilionya kuwa sekta ya vinywaji vya kileo inakabiliwa na changamoto kubwa ya bidhaa ghushi zinazohatarisha afya ya watumiaji na uadilifu wa soko. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, divai ndiyo bidhaa inayoghushiwa zaidi kwa asilimia 50.12, ikifuatiwa na bia kwa asilimia 47.44. Mvinyo ulirekodi asilimia 42.68 huku vodka ikifikia asilimia 36.95. John Kamau, mkazi wa Kiambu, anasimulia jinsi alivyokumbwa na matatizo makubwa baada ya kunywa pombe katika baa moja katikati mwa Nairobi. "Pombe ilikuwa chungu kupita kiasi. Niliendelea kuinywa kwa sababu nilikuwa tayari nimelipia. Asubuhi iliyofuata nilipatwa na maumivu makali ya kichwa, tumbo kuuma na kutapika mara kwa mara. Hata kufikia Jumatatu sikuweza kwenda kazini," alisema. Kamau alisema alitumia takriban Sh3,000 hospitalini kununua dawa na tangu wakati huo ameamua kuacha pombe kabisa. Mark Pollard, mshauri wa biashara kutoka Australia ambaye amekuwa akifikiria kuhamia Kenya, alisema alitapika na kuharisha mara mbili katika mazingira yanayomfanya ashuku pombe bandia. "Mara ya pili nilikuwa nimekunywa kiasi kidogo sana cha kileo nilichonunua kutoka duka maarufu. Ndani ya muda mfupi nilianza kutapika na kuharisha kupita kiasi," alisema. Hata hivyo, alikiri kuwa hawezi kuthibitisha kwa asilimia mia moja kwamba pombe ndiyo ilisababisha matatizo hayo kwa kuwa huenda kulikuwa na sababu nyingine za kiafya au chakula. Mfanyabiashara na mwandishi wa masuala ya kitaaluma Robert Ouko Owino alisema tukio lake lilitokea Juni. "Sikuweza kufanya kazi kwa siku tatu. Nimewahi kunywa pombe nyingi hapo awali lakini nilijua hali hii ilikuwa tofauti kabisa na kawaida," alisema. Kwa mujibu wake, watu wengi waliowasiliana naye baada ya kuandika kuhusu suala hilo walisimulia walivyolazwa hospitalini na kupata matatizo ya ini au kongosho (pancreas). Jeremiah Kinuthia, mwenye umri wa miaka 28 kutoka Nairobi, alisema alilazwa katika Hospitali ya Karen baada ya kunywa pombe iliyokuwa na ladha tofauti na ile aliyozoea. "Nilianza kutokwa na jasho na kupata shida ya kupumua. Nililazimika kuwekewa maji mwilini hospitalini," alisema. Tangu tukio hilo, ameacha kutumia pombe kali na sasa hunywa bia pekee. Dkt Joseph Wahome Mukundi, mtaalamu wa sumu katika Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Meru, alisema kemikali inayohusishwa mara nyingi na pombe bandia ni methanol, ambayo hutumika viwandani. Alieleza kuwa methanol hubadilika mwilini kuwa kemikali hatari zinazoweza kusababisha upofu, kuharibika kwa figo, kushindwa kwa viungo vya mwili na hata kifo. "Mishipa ya macho inaweza kuathirika na kusababisha upofu ikiwa mtu hatapata matibabu ya haraka," alisema. Daktari huyo amewataka watengenezaji wa pombe kutumia teknolojia kama misimbo ya QR ili kuwasaidia wanunuzi kuthibitisha uhalisi wa bidhaa. Pia amewahimiza Wakenya kununua pombe katika maduka makubwa na maeneo yaliyoidhinishwa rasmi ili kurahisisha ufuatiliaji iwapo kutatokea matatizo. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa ACA Robi Mbugua alisema bei ya chini isiyo ya kawaida inapaswa kuwa ishara ya tahadhari kwa wanywaji.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 28 Aug 2026 21:17:07
MCAs turn heat on Arati over stalled projects, poor roads
A section of Kisii MCAs has intensified pressure on Governor Simba Arati over stalled development projects, poor roads and alleged delays in implementing programmes for which funds have already been approved. The ward representatives protested on Saturday, accusing the county administration of failing to prioritise service delivery and leaving residents to grapple with deteriorating infrastructure [...] The post MCAs turn heat on Arati over stalled projects, poor roads appeared first on Kahawatungu.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Fri, 28 Aug 2026 21:00:00
And tender goes to: A teacher, missing office and Ruto's link to the new police uniform
Questions mount over police uniform supplier Nalitex after its office could not be traced and its registered address links to businesses associated with Rutos family.
read morekenyanews.go.ke
@kna Fri, 28 Aug 2026 17:26:06
Kajiado residents step up plans to prevent El Niño flooding
Kenya Railways Corporation (KRC), local administrators, and residents of Kajiado North have agreed to work together to address flooding risks along the Riruta-Ngong Meter Gauge Railway (MGR) route ahead of the anticipated El Niño rains. The collaboration will involve identifying and addressing drainage and stormwater challenges that have emerged along the railway corridor, with residents warning...
read morekenyanews.go.ke
@kna Fri, 28 Aug 2026 15:52:31
Journalists urged to uphold fairness ahead of 2027 polls
The Media Council of Kenya (MCK) has launched an intensive training programme for journalists in the Coast region, part of a national drive to prepare 4,000 media practitioners for coverage of the 2027 General Election. The training, held for staff of the Kenya Broadcasting Corporation (KBC), Kenya News Agency (KNA) and Pwani FM in Mombasa,...
read morekenyanews.go.ke
@kna Fri, 28 Aug 2026 16:16:50
Government calls for establishment of structures within the National Youth Council
The government has called on young Kenyans and other relevant stakeholders to work together to ensure peaceful, credible and inclusive elections of the National Youth Council. The long-awaited polls are expected to provide young people with a stronger platform for representation and create more jobs. The election, which is scheduled for October, regrettably, comes 14...
read moreRight Column Content