taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Thu, 27 Aug 2026 06:55:22
DCI yachunguza picha iliyomsawiri Machele kama mhudumu harusini
WAPELELEZI mjini Mombasa wanachunguza kisa cha picha ya Mbunge wa Mvita, Mohamed Machele, kubadilishwa na kuonyesha kana kwamba alikuwa mhudumu katika harusi ambako alikuwa mgeni mkuu, katika kile kinachodaiwa kuwa njama ya kumwaibisha. Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) imewasilisha ombi mahakamani ikitaka kupewa ruhusa ya kuchunguza simu ya mkononi inayohusishwa na aliyekuwa mshirika wa karibu wa mbunge huyo, Bw Haani Omar Swaleh, huku uchunguzi wa madai ya unyanyasaji wa mtandaoni ukiendelea. Bw Machele alihudhuria harusi ya mwana wa Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Pwani, Ali Nuno, mnamo Juni 20 katika eneo la Nyali, Mombasa, ambako alipigwa picha kadhaa akiwa pamoja na wageni wengine. Kwa mujibu wa stakabadhi za mahakama, mbunge huyo alishtuka baadaye alipojulishwa kuwa picha yake ilikuwa ikisambaa kwa wingi mitandaoni. Picha hiyo ilikuwa imehaririwa na kuonyesha kana kwamba alikuwa amevalia mavazi ya mhudumu katika harusi hiyo na kuchapishwa kwenye majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii, ikiwemo WhatsApp ya Bw Swaleh. "Baada ya kuhudhuria hafla hiyo, aliarifiwa kwamba alikuwa akivuma mtandaoni. Picha yake akiwa amevalishwa mavazi yaliyomwonyesha kama mhudumu katika harusi hiyo ilikuwa imechapishwa kwenye akaunti mbalimbali za mitandao ya kijamii, ikiwemo WhatsApp ya mshukiwa," stakabadhi hizo zilisema. Akiwa amekerwa na picha hiyo, Bw Machele aliripoti tukio hilo katika Kituo Kikuu cha Polisi Mombasa, chini ya nambari ya OB 49/23/7/ 2026. Inspekta Joseph Ngatia, mpelelezi wa DCI, alisema mbunge huyo aliripoti tukio hilo miongoni mwa sababu nyingine kwa kuwa yeye ni mtu mashuhuri na mbunge anayehudumu. Jumanne, DCI iliwasilisha ombi mahakamani ikimtaja Bw Swaleh kama mshukiwa anayechunguzwa kuhusu picha hiyo iliyohaririwa. Wapelelezi wanasema Bw Swaleh alikamatwa Agosti 20 na simu aina ya iPhone 11 ikachukuliwa kutoka kwake. Simu hiyo ina nambari mbili za IMEI na, kwa mujibu wa stakabadhi za mahakama, inaaminika kuwa ndiyo iliyotumika kubadilisha picha hiyo. Orodha ya vitu vilivyopatikana iliandaliwa baada ya simu hiyo kuchukuliwa. DCI inataka idara ya Uchunguzi wa Kisayansi cha Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Ugaidi (ATPU) kipewe ruhusa ya kuishikilia simu hiyo, kuifikia na kuifanyia uchunguzi pamoja na kutoa taarifa kutoka kwa akaunti za WhatsApp, Facebook na TikTok kwa kipindi cha Juni 20 hadi Julai 20, 2026. Inspekta Ngatia alisema uchunguzi huo wa kisayansi utawasaidia wapelelezi kubaini mazingira ya picha hiyo na kupata ushahidi utakaotumika mahakamani. Wapelelezi pia wanataka mahakama iagize kitengo hicho cha ATPU kuandaa ripoti kuhusu taarifa zilizotolewa kwenye simu hiyo na kutoa cheti cha ushahidi wa kielektroniki kwa mujibu wa Kifungu cha 106B (4) cha Sheria ya Ushahidi. Inspekta Ngatia alisema taarifa wanazotaka kupata ni za kibinafsi na zinaweza kufikiwa tu kwa idhini ya mahakama. "Ni kupitia amri hii pekee ambapo ATPU inaweza kufikia, kuchunguza kwa njia ya kisayansi na kutoa taarifa hizo za kibinafsi zilizohifadhiwa kwenye simu ya mshukiwa," alisema. Aliongeza kuwa taarifa zitakazopatikana zitawasaidia wapelelezi kukusanya na kuthibitisha ushahidi unaohusiana na malalamishi hayo. Uchunguzi huo unahusu madai ya unyanyasaji wa mtandaoni unaotokana na kuundwa, kuhaririwa na kusambazwa kwa picha ya mbunge huyo kwenye mitandao ya kijamii. Kosa hilo linachunguzwa chini ya Kifungu cha 27 cha Sheria ya Matumizi Mabaya ya Kompyuta na Uhalifu wa Mtandaoni ya mwaka 2018. Wapelelezi wanataka kubaini jinsi picha hiyo ilivyohaririwa, aliyehusika katika kuisambaza na iwapo vitendo hivyo vinaweza kuainishwa kama kosa chini ya sheria hiyo.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Thu, 27 Aug 2026 04:56:03
Suluhu's Party Expels Former VP, Names Replacement
Tanzania came into the spotlight following last year's disputed elections, during which state agents were accused of committing widespread atrocities, including killings, sparking international condemnation.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Thu, 27 Aug 2026 05:29:54
Trump Administration Turns to Foreign Govt Officials in New Crackdown
The Trump administration has directed American embassies worldwide to subject the new official's applications to greater scrutiny as it seeks to tighten the approval processes.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 27 Aug 2026 05:03:49
Casual labourer dies after stone falls from construction site, hits him in Naivasha
A 32-year-old casual labourer died after he was struck on the head by a stone that accidentally fell from the rooftop of a building under construction in Naivasha, Nakuru County. The incident occurred on Wednesday, August 26, at Kabati area in Naivasha Township. Police said the deceased, identified as Charles Ogendo Mutukiza, was outside the [...] The post Casual labourer dies after stone falls from construction site, hits him in Naivasha appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 27 Aug 2026 05:07:21
Man killed by brother in Nyamira land dispute
A 60-year-old man was allegedly killed by his brother while working on his farm in Gekano Sub-location, Nyamira County. The incident occurred on Wednesday, August 26, when Charles Osoro was reportedly attacked while ploughing his land. Police said Osoro's brother, allegedly struck him several times on the back of the head using a hoe, causing [...] The post Man killed by brother in Nyamira land dispute appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 27 Aug 2026 05:51:08
Teacher found dead in Yala restaurant room
A 48-year-old primary school teacher was found dead in a room at a bar and restaurant in Yala Market, Siaya County, in what police are treating as a suspected sudden death. The deceased, identified as Collins Abong'o, a teacher at Bar-Shauri Primary School, was found lying on his back on a bed while fully dressed [...] The post Teacher found dead in Yala restaurant room appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Thu, 27 Aug 2026 04:55:45
Gachagua sasa 'ammaliza' Uhuru Mlimani na Nairobi
CHAMA cha DCP kinachoongozwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kinazidi kujitokeza kama tishio kubwa kwa Jubilee, chama cha aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta, huku kikivamia ngome zake za kisiasa za Mlima Kenya na Nairobi. Huku Uchaguzi Mkuu wa 2027 ukikaribia, Jubilee imepata pigo jingine, viongozi wake kadhaa waliochaguliwa wakitangaza kuhamia DCP. Mbunge wa Kamukunji Yusuf Hassan ndiye wa hivi punde kuondoka Jubilee, hatua inayoonyesha kuwa ushindani kati ya vyama hivyo haupo katika eneo la Mlima Kenya pekee. Nairobi, wabunge wote watatu waliochaguliwa kwa tiketi ya Jubilee wametangaza kuwa watatetea viti vyao kwa tiketi ya DCP. Hao ni Bw Hassan, Mark Mwenje wa Embakasi Magharibi na Amos Mwago wa Starehe. Mlima Kenya, Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Kanini Kega, aliyedhaminiwa na Jubilee, pia amehamia DCP. Viongozi wengine wa Jubilee, wakiwemo wabunge walioteuliwa Sabina Chege, Aden Keynan (Eldas), Samuel Arama (Nakuru Mjini Magharibi), John Waluke (Sirisia) na Racheal Nyamai (Kitui Kusini), wameegemea Serikali Jumuishi. Kuhama huku kunaweza kudhoofisha uwezo wa Bw Kenyatta kujadiliana kisiasa kuelekea 2027 na kumfanya Bw Gachagua kuwa mhusika mkubwa katika siasa za upinzani. Akizungumzia hatima ya Jubilee, Bw Kega alisema wazi kuwa chama hicho kimekufa kisiasa Mlima Kenya na Nairobi. "Hakuna Jubilee Mlima Kenya na Nairobi. Tatizo linaloikabili Jubilee ni ukosefu wa uongozi. Tulipojaribu kufanya mabadiliko, yalipingwa, na sasa mnaona kinachotokea. Kila mtu anaondoka," akasema Bw Kega. Hata hivyo, Naibu Kiongozi wa Jubilee Jeremiah Kioni alipuuza kuhama kwa viongozi hao, akisema wengi wao hawakuwa waaminifu kwa chama hicho na walikitumia tu kupata nyadhifa serikalini. "Si hasara mpya kwetu kwa sababu hawajawahi kujitambulisha na Jubilee. Kwa kweli, ni fursa kwetu kutafuta vijana ambao wamejitolea kuwa nguzo wa chama," akasema Bw Kioni. Alidai kuwa DCP inaonekana kujishughulisha zaidi na kupambana na Jubilee kuliko UDA. Bw Gachagua, hata hivyo, alitangaza Jumanne kuwa DCP imechukua usukani wa siasa za Nairobi baada ya Bw Hassan kujiunga na chama hicho. "Ninataka kutangaza leo kwamba DCP imechukua Nairobi," akasema kiongozi huyo wa DCP. Naibu kiongozi wa DCP Cleophas Malala alisema kuhama kwa Bw Hassan ni ushahidi kuwa chama hicho kinageuka kuwa na sura ya kitaifa, huku Katibu Mkuu John Methu akiahidi uteuzi wa haki kwa wagombeaji. "Nimejiunga na DCP kwa sababu ni chama kinachotaka mabadiliko halisi," akasema Bw Hassan. Kwa kuhama huku, vita vya kisiasa kati ya DCP na Jubilee vinaonekana kuingia katika hatua mpya, huku Nairobi na Mlima Kenya zikitarajiwa kuwa maeneo muhimu ya mapambano kuelekea 2027.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Thu, 27 Aug 2026 05:55:06
Muhoozi kuwania urais 2031 akisema babake, Rais Museveni, atamuunga mkono
KAMPALA, Uganda: MKUU wa jeshi la Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni mwana wa Rais Yoweri Museveni, ametangaza kuwa atawania urais katika uchaguzi wa mwaka 2031. Kainerugaba, mwenye umri wa miaka 52, kwa muda mrefu ametajwa kuwa mrithi anayetarajiwa wa baba yake mwenye umri wa miaka 81, ambaye ametawala Uganda kwa miongo minne. Mkuu huyo wa jeshi pia anafahamika kwa jumbe zake zenye utata kwenye mtandao wa kijamii wa X, zikiwemo tishio la kumkata kichwa kiongozi mkuu wa upinzani, Bobi Wine. Katika ujumbe mmoja kati ya mfululizo wa machapisho aliyoweka X Jumanne usiku, Kainerugaba alisema alikuwa tayari kuwania wadhifa wa juu zaidi nchini humo. "Nitawania wadhifa wa juu zaidi nchini mnamo 2031. Na tutashinda kwa neema ya Mwenyezi Mungu," akasema Kainerugaba. Aliongeza kuwa kwa kuungwa mkono na baba yake, ambaye huwa anamrejelea kwa heshima kama "Mzee", ana uhakika wa kupata asilimia 90 ya kura katika uchaguzi huo. Kainerugaba, ambaye anaongoza kundi la wazalendo wa Uganda (PLU), hapo awali alikuwa ametangaza kuwa angewania urais katika uchaguzi uliofanyika Januari mwaka huu, lakini baadaye akajiondoa na kumuunga mkono baba yake. Alikuwa na nafasi muhimu katika kampeni za kuhakikisha Museveni anachaguliwa tena Januari, huku akiamuru hatua kali dhidi ya wapinzani na kuzimwa kwa intaneti, kulingana na ripoti zilizozingira uchaguzi huo tata. Museveni, ambaye anaongoza chama tawala cha National Resistance Movement (NRM), amekuwa madarakani tangu 1986. Wakosoaji wamekuwa wakiilaumu serikali yake kwa ukiukaji wa haki za binadamu, yakiwemo mateso, utekaji nyara na kuwazuilia watu kiholela, madai ambayo serikali imekanusha. Bobi Wine alikimbilia Amerika mapema mwaka huu, akisema alihofia maisha yake baada ya kupinga ushindi wa Museveni akidai kulikuwa na visa vya udanganyifu. Mwanasiasa mwingine mkongwe wa upinzani, Kizza Besigye, amekuwa gerezani tangu 2024 na anakabiliwa na kesi ya uhaini. Licha ya afya ya Besigye kuendelea kudorora, utawala wa Museveni hauonekani kumakinikia kumwaachilia huru. Haijulikani iwapo Museveni mwenyewe atawania tena urais 2031 baada ya tangazo lake, huku serikali ikisema uamuzi huo utafanywa na rais pamoja na chama chake kwa wakati mwafaka. Mnamo 2031, Museveni atakuwa na umri wa miaka 86 na akiwania, atakuwa kati ya viongozi wakongwe zaidi ambao wamewahi kuwania wadhifa wa urais ulimwenguni.
read moreRight Column Content