kahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 20 Aug 2026 07:45:31
Panic as aircraft tyre bursts on JKIA runway, briefly suspending operations
Operations at Jomo Kenyatta International Airport (JKIA) were briefly disrupted on Wednesday evening after an aircraft developed a tyre burst while landing. Officials said the incident happened when the Boscovik aircraft, registration number 5Y-ZBV, landed at JKIA from the Maasai Mara at about 6pm. The aircraft's rear right tyre burst after landing on one of [...] The post Panic as aircraft tyre bursts on JKIA runway, briefly suspending operations appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 20 Aug 2026 08:03:07
Gang steals Sh980,000 from car after Homa Bay contractor visits hotel
Police in Homa Bay are investigating the theft of Sh980,000 from a vehicle shortly after the money was withdrawn from a bank. The cash was stolen on Wednesday afternoon after the proprietor of Comnex Contractor Limited, his brother and their driver stopped at Glory Hotel along the Homa Bay-Kisumu Road. According to police, the group [...] The post Gang steals Sh980,000 from car after Homa Bay contractor visits hotel appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Thu, 20 Aug 2026 07:55:49
Wanafunzi wengi wa Gredi 9 hawawezi kusoma ipasavyo -Ripoti
TAKRIBAN thuluthi moja ya wanafunzi wanaojiunga na Sekondari Pevu kutoka Sekondari Msingi hawana ujuzi muhimu wa kusoma, kuandika na kuhesabu, ripoti mpya imefichua. Ripoti hiyo iliyotolewa na Usawa Agenda, shirika linalofanya utafiti kuhusu elimu ya msingi, pia imeonyesha kuwa wanafunzi katika shule za umma za maeneo ya mashambani ndio walioathirika zaidi. Utafiti huo uliofanywa katika kaunti zote 47 ulihusisha familia 41,156, shule 1,527 na wanafunzi 49,835. Pia ulihusisha jamii za wakimbizi katika kambi za Dadaab, Kakuma na Kalobeyei. Ripoti hiyo inasema asilimia 29 ya wanafunzi wa Gredi 9 hawana ujuzi wa msingi wa kusoma na kuhesabu. Mwanafunzi mmoja kati ya watano wa Gredi 9 hawezi kusoma hadithi ya Kiingereza ya kiwango cha Gredi 3. Hali hiyo pia inawakumba wanafunzi watatu kati ya 10 wa Gredi 7. Hata hivyo, pengo hilo huanza mapema zaidi. Asilimia 41 ya wanafunzi wa Gredi 7 hawana ujuzi wa msingi wa kusoma na kuhesabu. Ripoti hiyo ilisema shule za umma hufanya vibaya kuliko shule za kibinafsi katika kusoma na kuhesabu. "Ushahidi unaonyesha kuwa sera za serikali zimefanikiwa kuwadumisha wanafunzi madarasani, lakini bado hazijafanikiwa kuhakikisha wanajifunza au shule wanazojiunga nazo zina vifaa sawa vya kusoma," ripoti hiyo ilisema. Ripoti hiyo ilibaini pia upungufu mkubwa wa vifaa shuleni. Ni asilimia 27.5 pekee ya shule za Sekondari Msingi zilizo na maabara za sayansi zinazofanya kazi, huku asilimia 27 zikiwa na maktaba. Ni asilimia 34.3 pekee zilizo na vifaa vya kutosha vya kusoma na asilimia 46.3 zilikuwa na kompyuta za wanafunzi. Tofauti za kikanda ni kubwa. Nairobi ina maabara zinazofanya kazi katika asilimia 98.7 ya shule za Sekondari Msingi, ikilinganishwa na asilimia 15.4 Kaskazini Mashariki na asilimia 13.8 Magharibi. Mkurugenzi wa Idara ya Sekondari Msingi katika Wizara ya Elimu Hellen Avisa, alisema changamoto ya ujuzi wa msingi inapaswa kushughulikiwa mapema. Alisema ushahidi uliowasilishwa unapaswa kuchochea hatua katika ngazi ya kitaifa, kaunti na shule. Ripoti hiyo inapendekeza wanafunzi wa Gredi 7 hadi 9 wapewe masomo maalum ya kurekebisha mapengo ya kusoma na kuhesabu. Pia inataka serikali kuongeza uwekezaji katika maabara, maktaba, vifaa vya kusoma na kuhakikisha fedha za shule zinatolewa kwa wakati. Ripoti hiyo ilisema ni asilimia 52.3 pekee ya shule za Sekondari Msingi zinazopokea fedha kwa wakati.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Thu, 20 Aug 2026 08:11:39
Binti aonya mamake akome kuchekacheka na mume wake
KATIKA tukio lisilo la kawaida,msupa mmoja wa hapa alimpigia mamake simu na kumuonya vikali akome kucheka cheka na mumewe kila mara. Mwanadada huyo alishuku kwamba wawili hao walikuwa kwenye uhusiano wa kisiri baada ya jamaa kutoa usemi kwamba mama-mkwe alikuwa amedumisha urembo wake. Matamshi hayo yalimshtua mwanadada huyo aliyehisi kwamba mumewe alikuwa na lengo la kunyemelea mama mkwe. Demu akikasirika zaidi aliporejea nyumbani juzi na kupata mamake mzazi akiongea na mumewe kwa 'video call' huku wakicheka cheka. Alimfokea mumewe akimlaumu kwa kuvuka mipaka na kukosa utu. "Nilidhani wewe ni mtu unayejua mipaka kumbe huna heshima hata kidogo.Unawezaje kumrushia mama-mkwe mistari? Sikujua mamangu mzazi pia anaweza kunisaliti kiwango hiki," alilia kabla ya kuchukua simu na kumpigia mamake kumtaka akome kumharibia ndoa.
read moreRight Column Content