taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 17 Aug 2026 11:19:20
Zaidi ya nguruwe 1,000 waangamizwa na Homa
ZAIDI ya nguruwe 1,000 wamefariki katika Kaunti ya Kiambu kutokana na ugonjwa wa African Swine Fever (ASF), huku Serikali ikiongeza juhudi za kudhibiti kuenea kwa homa hiyo ya nguruwe ambayo imeendelea kusababisha hasara kubwa kwa wafugaji maeneo mbalimbali nchini. Kurugenzi ya Huduma za Mifugo Nchini, ndiyo Directorate of Veterinary Services (DVS) imeagiza idara za mifugo katika kaunti kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa, usalama wa mashamba, kudhibiti uhamishaji wa nguruwe na kuzindua kikosi cha kukabiliana haraka na milipuko. Milipuko mikubwa imeripotiwa katika kaunti za Tharaka-Nithi, Kiambu, Busia, Embu, Kakamega, Siaya na Migori, miongoni mwa nyingine, na kusababisha vifo vya nguruwe wengi na hasara za kiuchumi kwa wafugaji. Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo katika Idara ya Maendeleo ya Mifugo chini ya Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, Dkt Allan Azegele, alisema ASF ni ugonjwa unaoambukizwa kwa urahisi na kuenea haraka miongoni mwa nguruwe, huku kiwango cha vifo kikifikia asilimia 70 kulingana na aina ya virusi, umri na uwezo wa mnyama kukabiliana na ugonjwa huo. "Nguruwe wakubwa na wadogo wanaweza kuathirika pakubwa," alisema kwenye mahojiano na 'Akilimali Dijitali'. Takwimu za Kenya Animal Biosurveillance System (KABS) na Laboratory Information Management System (LIMS) za Januari hadi Juni 2026 zinaonyesha kuwa ugonjwa huo umeripotiwa katika maeneo kadhaa. Tharaka-Nithi ilirekodi visa 108 vya maambukizi na vifo 97 kati ya Januari 5 na 11, sawa na kiwango cha vifo cha karibu asilimia 90. Embu ilirekodi visa vitatu na kifo kimoja kati ya Mei 18 na 24. [caption id="attachment_191232" align="aligncenter" width="300"] Nguruwe wakisherehekea malisho. Picha|Sammy Waweru[/caption] Hata hivyo, mlipuko mkubwa zaidi umeshuhudiwa Kiambu, ambako zaidi ya mashamba 20 eneo la Juja, Thika na Ruiru yameathirika tangu katikati mwa Mei. Karibu nguruwe 1,470 wameripotiwa kuugua au kufa, huku baadhi ya wafugaji wakipoteza hadi asilimia 100 ya nguruwe. Kwenye mahojiano Dkt Azegele alithibitisha kuwa ASF haiambukizwi kwa binadamu wala kuwa tishio kwa afya ya umma. "Nyama ya nguruwe iliyokaguliwa na kuthibitishwa na mkaguzi aliyeidhinishwa ni salama kwa matumizi," alisema. Hata hivyo, Homa hiyo ya nguruwe inaweza kuangamiza mifugo yote na kuvuruga biashara, kuwaacha wafugaji bila mapato. Hasara za kiuchumi zinazohusishwa na ASF nchini hukadiriwa kufikia Dola 7 milioni (Sh905.1 milioni) kila mwaka. Kwa sasa hakuna tiba wala chanjo inayopatikana kibiashara dhidi ya aina za virusi vya ASF zinazosambaa nchini. Azegele alisema kukua haraka kwa virusi kunafanya iwe vigumu kutengeneza chanjo inayofaa kwa aina zote. Aidha, aliwataka wafugaji kuimarisha usalama wa mashamba kwa kudhibiti watu, wanyama, magari na vifaa vinavyoingia katika makao ya nguruwe. "Nguruwe wapya wanapaswa kununuliwa kutoka kwa wazalishaji wanaoaminika, kutengwa na kufuatiliwa kabla ya kuunganishwa na wengine," alishauri afisa huyo. Magari yanayoingia na kutoka mashambani yanapaswa kusafishwa kwa dawa, huku sehemu za kuoshea miguu zikiwekwa karibu na makazi ya nguruwe. Wafugaji, pia, wameonywa dhidi ya kuwapa nguruwe mabaki ya chakula ambayo hayajatibiwa. [caption id="attachment_191233" align="aligncenter" width="300"] Zaidi ya nguruwe 1,000 wamefariki Kaunti ya Kiambu kutokana na Homa ya nguruwe. Picha|Sammy Waweru[/caption] Dkt Azegele alisema mabaki ya chakula kutoka kwa hoteli yanapaswa kupikwa vizuri kabla ya kupewa nguruwe, huku akisema kupika mabaki hayo kwa kutumia karibu asilimia mbili ya soda ash au magadi soda kunaweza kusaidia kuangamiza virusi. Serikali pia imewataka wafugaji kuripoti mara moja dalili zisizo za kawaida au vifo vya ghafla vya nguruwe kwa maafisa wa mifugo. Katika maeneo yaliyoathirika, wakulima wanapaswa kufuata masharti ya karantini na udhibiti wa uhamishaji wa wanyama. Mizoga ya nguruwe inapaswa kutupwa kwa usalama na uangalifu chini ya mwongozo wa maafisa wa mifugo ili kuzuia kuenea zaidi kwa virusi vya Homa ya nguruwe, ASF. Dkt Azegele alisema idara za mifugo katika kaunti zimeagizwa kuongeza kasi ya ukaguzi katika masoko ya mifugo, machinjioni na maeneo ya kuuza nyama za nguruwe. Hali kadhalika, zitahakikisha visa vinavyoshukiwa vinathibitishwa kwenye maabara kwa haraka, mienendo ya wanyama inafuatiliwa na wafugaji kuelimishwa kuhusu dalili za ugonjwa huo. Virusi vinavyosambaa nchini ni vya Genotype IX, aina ambayo tafiti zimeonyesha kuwa na uwezo mkubwa wa kusababisha maradhi mbaya na vifo vingi. [caption id="attachment_191234" align="aligncenter" width="300"] Nguruwe wakiwa kwenye zizi safi. Picha|Sammy Waweru[/caption] Wasiwasi zaidi umeibuliwa na uwepo wa nguruwe wanaobeba virusi bila kuonyesha dalili. Utafiti ulibaini virusi vya ASF katika tishu za viungo vya ndani vya asilimia 15.9 ya nguruwe walioonekana kuwa na afya katika eneo la mpaka wa Kenya na Uganda. Serikali imezindua mfumo wa kidijitali kusajili mifugo nchini unaojulikana kama Animal Identification and Traceability System (ANITRAC), utakaosaidia kutambua wanyama na wamiliki wao, pamoja na kufuatilia historia yao, magonjwa na mienendo tangu kuzaliwa hadi kuchinjwa, kusafirishwa nje au kufariki. Kwa sasa, asasi mbalimbali za mifugo zimeagizwa kuimarisha ufuatiliaji katika maeneo yaliyo katika hatari kubwa, hasa Kiambu, Tharaka-Nithi na Embu, pamoja na maeneo ya mipakani. Kenya inakadiriwa kuwa na takriban nguruwe 800,000.
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 17 Aug 2026 10:50:07
Uasin Gishu youth embrace sports to foster peace
Dozens of young people in the Langas area of Uasin Gishu County gathered for a football tournament on the weekend, using the opportunity to foster unity and promote peace ahead of the 2027 general election. The tournament, organized within the Langas community, brought together youth from diverse backgrounds and social strata, with organizers aiming to...
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 17 Aug 2026 10:56:11
Pedalling for Purpose: A 1,100-Kilometre Charity Ride from Busia to Mombasa
Thirteen students from Starehe Boys' Centre have completed a grueling 1,100-kilometre charity cycling expedition from Busia to Mombasa to raise a Sh10 million education fund for needy learners. The students arrived in Mombasa on Sunday, bringing to an end the 14-day Dr Geoffrey Griffin Memorial Bike-A-Thon, an annual ride that celebrates the legacy of...
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 17 Aug 2026 11:04:44
Mombasa County employees warned to stay out of political activities
Public servants have been reminded to stay away from political activities as the clock ticks towards the August 10, 2027, General Election and instead to focus on serving Kenyans faithfully and efficiently. Mombasa Governor Abdulswamad Shariff Nassir has warned county employees against engaging in politics, advising them not to be swayed by political influences. Governor...
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 17 Aug 2026 11:10:09
Laikipia residents enjoy free medical camp
Over 300 residents of Thingithu Ward in Laikipia County received free medical check-ups and advise in a medical camp on the need to prioritize preventive measures to combat the rise in lifestyle diseases. During the camp, residents were screened for prostate cancer, which medics decried was on the rise, yet a majority of men rarely...
read morekenyans.co.ke
@kenyans Mon, 17 Aug 2026 11:08:25
Judiciary Explains Letter Alleging Gachagua Sought to Influence Supreme Court
Former Kenyan Deputy President Rigathi Gachagua was impeached in October 2024 following a motion in the National Assembly and removal by the Senate, with the High Court upholding his removal.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 17 Aug 2026 11:09:34
Two including cop die, 46 injured, 6 cars torched during Linda Mwananchi rally in Homa Bay Town
At least two people were killed while 46 others are in hospitals following chaos that were experienced during the Linda Mwananchi rally in Homa Bay on Sunday. Among those killed was a police driver. He was attached to Nyando police command. His boss who was in the car is among those admitted in hospital with [...] The post Two including cop die, 46 injured, 6 cars torched during Linda Mwananchi rally in Homa Bay Town appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 17 Aug 2026 10:57:29
Wanahabari wajeruhiwa mkutano wa Linda Mwananchi Homa Bay
WAANDISHI wawili wa habari walijeruhiwa na biashara kusitishwa katika Mji wa Homa Bay Jumapili huku mvutano ukizuka kabla ya mkutano wa Linda Mwananchi. Waandishi wa AFP Fred Ooko na Brian Ongoro walishambuliwa karibu saa tatu asubuhi walipokuwa wakiripoti matukio katika mji huo. Wawili hao walisema walivamiwa na kundi la watu waliokuwa na silaha za kienyeji. Vitambulisho vyao vya kazi, leseni za udereva, kamera na mali nyingine zilichukuliwa. Bw Ooko alisema alibururwa barabarani na kupigwa kwa marungu kabla ya mhudumu wa bodaboda aliyemfahamu kuingilia kati na kumsaidia kutoroka hadi Olare. "Mwenzangu Brian Ongoro pia alipigwa. Alipoteza simu na kamera. Leseni yangu, kitambulisho cha kazi na vitu vingine vilichukuliwa," akasema. [caption id="attachment_191227" align="alignnone" width="1600"] Vioo vya magari vilivyovunjwa vyatapakaa katika barabara za Homa Bay wakati wahuni walipokabili msafara wa Linda Mwananchi. Picha|George Odiwuor[/caption] Mji wa Homa Bay ulikuwa kama eneo lisiloweza kufikika baada ya vijana kufunga barabara kadhaa kwa mawe na magogo, huku wengine wakiwasha moto. Biashara zilisitishwa huku maduka na baadhi ya maeneo ya ibada yakifungwa. Msafara wa Linda Mwananchi uliokuwa ukielekea Homa Bay ulilazimika kubadili njia baada ya baadhi ya barabara kuzuiwa. Polisi walitumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji na kufungua barabara. Hapo awali, polisi walikamata washukiwa 15 wa genge la uhalifu katika Kaunti ya Kisumu na kuwapokonya mapanga, visu, kamba, marungu na silaha nyingine. Polisi walisema washukiwa hao walikuwa wakielekea Homa Bay kwa magari matatu. Mmoja wao, Oliver Jaoko almaarufu Oliveti, anadaiwa kuwa kiongozi wa kundi hilo lakini alitoroka wakati wa operesheni. Washukiwa hao 15 wamewekwa chini ya ulinzi wakisubiri kufikishwa mahakamani.
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 17 Aug 2026 09:35:23
Inaugural Mombasa mega marathon ends on a high note
The coastal city of Mombasa came alive as athletes, fitness enthusiasts, leaders, and community members gathered on Sunday for the inaugural Mombasa Mega Marathon 2026. The race organized by the Mombasa County government and a galaxy of civil society organizations sought to promote a healthy lifestyle and champion a drug-free society. The inaugural...
read morekenyans.co.ke
@kenyans Mon, 17 Aug 2026 10:16:26
UDA Announces Sweeping Changes Amid Mass Defections Ahead of 2027 Elections
To change the constitution of a political party in Kenya, the party must follow internal democratic procedures, a move coming barely a year to the 2027 general elections.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 17 Aug 2026 10:04:19
Guus Til Siblings: Meet Klaartje, Daan and Kees
Guus Berend Til is a Dutch professional footballer who plays as an attacking midfielder for Eredivisie club PSV Eindhoven and the Netherlands national team. Born on 22 December 1997 in Samfya, Zambia, where his father worked in development, he moved with his family to the Netherlands at the age of three and grew up in [...] The post Guus Til Siblings: Meet Klaartje, Daan and Kees appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 17 Aug 2026 10:07:13
Micky van de Ven Siblings: Getting to Know Caya van de Ven
Micky van de Ven is a Dutch professional footballer born on 19 April 2001 in Wormer, Netherlands. He primarily plays as a centre-back and can also operate as a left-back and currently represents Premier League club Tottenham Hotspur and the Netherlands national team. Known especially for his exceptional pace, recovery speed, athleticism and composure on [...] The post Micky van de Ven Siblings: Getting to Know Caya van de Ven appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 17 Aug 2026 10:18:46
Denzel Dumfries Siblings: All About Demelza, Daniëlle and Donovan
Denzel Justus Morris Dumfries is a Dutch professional footballer born on 18 April 1996 in Rotterdam, Netherlands. He plays primarily as a right-back or right wing-back and is known for his powerful overlapping runs, physical presence, aerial ability, and goal-scoring contributions from the flank. He currently represents La Liga club Real Madrid, having joined them [...] The post Denzel Dumfries Siblings: All About Demelza, Daniëlle and Donovan appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 17 Aug 2026 09:48:09
Faida za nishati ya jua katika kilimo
KWA wakulima wanaotumia mfumo wa umwagiliaji maji mashamba na mimea kwa kutumia mifereji, gharama ya nishati inaweza kuwa kikwazo kikubwa katika kuongeza uzalishaji na faida. Hata hivyo, matumizi ya nishati ya jua yanaibuka kama suluhisho kupunguza gharama huku yakihakikisha upatikanaji wa maji shambani. Esther Wariara Ng'ang'a, mkulima kutoka Kiairia, Githunguri, Kaunti ya Kiambu, ni mmoja wa wakulima wanaonufaika na teknolojia hiyo. Kabla ya kutumia pampu ya sola, alitumia takriban Sh500 kila siku kulipia umeme wa kupampu maji kutoka kisimani. "Sasa natumia karibu Sh250 pekee kwa siku. Fedha ninazookoa nazirejesha shambani kwa kuongeza uzalishaji," anasema. [caption id="attachment_191214" align="aligncenter" width="300"] Esther Wariara Ng'ang'a, mkulima kutoka Kiairia, Githunguri, Kaunti ya Kiambu anayetumia nishati ya jua kuendeleza kilimo. Picha|Sammy Waweru[/caption] Mbali na kupunguza gharama, nishati ya jua imemwezesha Esther kupata maji ya umwagiliaji mimea bila kukosekana. Hali hii imemsaidia kumwagilia mimea maji wakati yanapoyahitaji, badala ya kutegemea mvua. "Matokeo yake ni ongezeko la mavuno. Kabla ya kutumia pampu ya sola, nilikuwa nikivuna karibu kilo 50 za managu kwa wiki. Sasa huvuna takriban kilo 200 kwa wiki," anaambia 'Akilimali Dijitali'. Pia huvuna karibu kilo 50 za terere na kilo 100 za sukuma wiki kila wiki, kulingana na mahitaji ya soko. Esther huuza managu na terere kwa Sh50 kwa kilo, huku akiuza zaidi ya kilo 500 za ndizi kwa mwezi kwa Sh45 kwa kilo. "Hulima ndizi na tuna chama cha ushirika kinachotusaidia kupata soko lenye ushindani mkuu," akasema wakati wa mahojiano shambani mwake Githunguri. [caption id="attachment_191215" align="aligncenter" width="300"] Tangi la maji ambalo Esther Wariara Ng'ang'a hupampu maji kwa kutumia sola. Picha|Sammy Waweru[/caption] Pampu ya sola aliipata baada ya kupata mafunzo kuhusu teknolojia za nishati safi kupitia mradi wa Anglican Development Services (ADS) Mount Kenya. Alilipa Sh19,000, ada za kwanza, na sasa hulipa Sh4,000 kila mwezi kwa mwaka mmoja, huku gharama ya mfumo mzima ikiwa Sh67,000. Anasema nishati ya jua imempunguzia gharama za uzalishaji, kuongeza mavuno na kumpa nafasi ya kuwekeza zaidi katika shamba. Lengo lake sasa ni kutumia nishati safi katika shughuli zote za shamba, ikiwemo biogas ya mapishi, ili kupunguza gharama zaidi.
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 17 Aug 2026 09:25:56
KNUT asks teachers to use social media responsibly
KNUT Secretary General Collins Oyuu has advised teachers to use social media platforms responsibly to avoid infringing on the rights of other citizens but urged the teachers' employer not to gag them. Speaking in Bomet, Oyuu took exception with a recent circular said to be from the Teachers' Service Commission (TSC) warning teachers against...
read moreRight Column Content