kenyanews.go.ke
@kna Sun, 16 Aug 2026 10:30:05
Mudavadi calls for peaceful campaigns
Prime Cabinet Secretary Musalia Mudavadi has called on political parties and Kenyans to uphold the tenets of the constitution by maintaining peace during, before and after the 2027 electioneering period in the spirit of democracy. Speaking during the commissioning of the newly constructed storey tuition block at Kaliwa Comprehensive School in Teso South constituency Mudavadi...
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sun, 16 Aug 2026 09:17:06
Blow to Borrowers as Court Issues Directives Affecting Bank Loan Interest Rates
The court decision comes days after CBK maintained the lending rates at 8.75 per cent to keep inflation expectations anchored amid rising global economic uncertainties and risks linked to higher oil prices.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 16 Aug 2026 08:54:51
Shelley Duvall Net Worth
Shelley Duvall was an American actress, producer and television personality who had an estimated net worth of $500,000 at the time of her death in 2024. She became one of the most recognizable actresses of the 1970s and 1980s through memorable performances in films including 3 Women, The Shining and Popeye. Duvall built her reputation [...] The post Shelley Duvall Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 16 Aug 2026 09:04:48
Scatman Crothers Net Worth
Scatman Crothers net worth was estimated at $500,000 at the time of his death in 1986. The American actor, musician and voice artist built his career across film, television, radio and music, becoming one of the most recognizable character actors of his generation. Crothers was best known for playing Louie the Garbage Man on the [...] The post Scatman Crothers Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 16 Aug 2026 08:55:16
Ruto afufua maono ya hayati Raila katika Ruwaza yake ya 2060
RAIS William Ruto alipozindua mjadala wa kitaifa kuhusu mustakabali wa Kenya baada ya Ruwaza ya 2030 wiki hii, aliutaja kama juhudi mpya za kuwapa mwongozo wa muda mrefu utakaonufaisha vizazi vya sasa na vijavyo. Hata hivyo, nyuma ya kauli za kuunda mwongozo mpya wa maendeleo, unafanana pakubwa na pendekezo la aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga kuhusu Kongamano la Kitaifa la Vizazi ambalo lilizinduliwa miezi michache kabla ya kifo chake. Mipango yote miwili inaweka wananchi katikati ya maamuzi kuhusu mustakabali wa taifa. Pia inakusudia kuwahusisha vijana, wataalamu, viongozi wa kaunti, wanavyuo, sekta ya biashara, mashirika ya kiraia na viongozi wa kidini katika kujadili mwelekeo wa Kenya. Pendekezo la Raila lilijikita zaidi katika kutafuta suluhu kwa changamoto za kisiasa, kiuchumi na kiutawala zinazokabili taifa. Kwa upande mwingine, mjadala wa Ruto unalenga kufafanua Kenya itakuwa taifa la aina gani baada ya kufikia mwisho wa mpango wa Ruwaza ya 2030. Licha ya tofauti hizo, misingi ya miradi hiyo inaonekana kufanana kwa kiasi kikubwa. Yote inatokana na imani kuwa mustakabali wa Kenya haupaswi kuamuliwa na wanasiasa wachache katika mikutano ya Nairobi pekee. Ruto amependekeza mchakato wa kitaifa utakaowahusisha wadau kutoka sekta mbalimbali ili kuamua dira mpya ya taifa. Kwa mujibu wa vyanzo vya Ikulu, Gavana wa Kisumu Profesa Anyang' Nyong'o amepewa jukumu la kuongoza timu itakayobuni mfumo wa majadiliano hayo. Timu hiyo itapendekeza namna mashauriano yatafanyika kutoka mashinani hadi kiwango cha kitaifa. Muundo huo unafanana pakubwa na mpango ambao Raila alikuwa amependekeza mwaka 2025. Akizungumza katika mahojiano akiwa nyumbani kwake Karen Julai 19, 2025, Raila alisema kongamano hilo lingeanzia katika vituo vya kupigia kura kabla ya kuendelea hadi ngazi za wadi, maeneo bunge na kaunti. Hatimaye, wawakilishi wangekutana katika kongamano kubwa la kitaifa la takribani wajumbe 3,000 kutoka sehemu mbalimbali za nchi. "Hilo lingekuwa baraza halisi la wananchi," alisema Raila wakati huo. Alisisitiza kuwa wananchi wa kawaida walipaswa kupewa nafasi ya kueleza changamoto zao na kuamua vipaumbele vya taifa kabla ya wanasiasa kuingilia mchakato huo. Kwa upande wake, Ruto alipokuwa akizindua mjadala huo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyatta (KICC), alisisitiza mara kadhaa kwamba si mradi wa serikali bali wa wananchi. "Huu si mradi wa serikali. Huu ni mradi wa wananchi," alisema Rais. Aliongeza kuwa serikali itatoa jukwaa na rasilimali lakini haitawalazimisha wananchi maamuzi ya kufanya. Kauli hiyo inaendana kwa kiwango kikubwa na mawazo ambayo Raila alikuwa ametetea kuhusu umuhimu wa wananchi kutumia mamlaka yao ya kikatiba kuamua hatima ya taifa. Raila alipendekeza kwamba nusu ya wajumbe katika mikutano ya mashinani wawe vijana hasa wa kizazi cha Gen Z. Naye Ruto amesema mjadala wa baada ya Ruwaza ya 2030 lazima uzingatie maslahi ya vijana ambao watarithi Kenya ya baadaye. Hata hivyo, kuna tofauti muhimu. Kongamano la Raila lilizaliwa wakati taifa lilikuwa linakabiliwa na malalamishi kuhusu utawala, ukosefu wa ajira, ufisadi na madai ya ukatili wa polisi. Hivyo lilikuwa na mwelekeo wa kisiasa na kikatiba zaidi. Kwa upande mwingine, mjadala wa Ruto umejikita katika maendeleo ya muda mrefu na namna ya kuhakikisha Kenya inabaki na mwongozo mmoja hata baada ya mabadiliko ya serikali. Naibu Rais Kithure Kindiki na Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung'wah wamependekeza kwamba mwongozo huo mpya upewe msingi wa kisheria ili serikali zijazo zisibadilishe mwelekeo wa taifa kila baada ya uchaguzi. Hata hivyo, changamoto kubwa kwa utawala wa Ruto itakuwa kuwashawishi wakosoaji kwamba mchakato huo ni wa kweli na haujalenga kuendeleza ajenda za kisiasa za serikali iliyopo madarakani. Baadhi ya viongozi wa upinzani tayari wanataka ukaguzi wa kina wa utekelezaji wa Ruwaza ya 2030 kabla ya kuanzishwa kwa mpango mwingine mpya. Kifo cha Raila Odinga Oktoba 2025 kilikatiza ndoto ya kongamano lake la kitaifa kabla ya kutekelezwa. Sasa mjadala wa Ruto kuhusu Kenya baada ya Ruwaza ya 2030 unaonekana kufufua kwa namna fulani baadhi ya mawazo hayo, lakini kwa sura mpya ya maendeleo na mipango ya muda mrefu ya taifa.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 16 Aug 2026 09:55:37
Wakenya 40,000 wamefariki katika ajali za barabarani miaka 10-Ripoti
AJALI za barabarani zimeendelea kuwa tishio kubwa Kenya, huku zaidi ya watu 40,000 wakifariki katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, kulingana na takwimu za serikali. Jana, huzuni ilitanda eneo la Nthongoni, Kaunti ya Makueni, baada ya ajali mbaya ya barabarani kusababisha vifo vya watu saba na kujeruhi zaidi ya 60. Abiria walikuwa wakielekea sherehe ya kulipa mahari katika kijiji cha Inyoni, safari iliyotarajiwa kuwa ya furaha ikageuka kuwa ya majonzi. Kiongozi wa jamii Joseph Kyonda alieleza kuwa alipoteza majirani sita na kuomba msaada wa kifedha kwa mazishi yenye heshima. Basi dogo lenye viti 46 lilikuwa limebeba watu 71 wakati ajali ilitokea. Afisa Mkuu wa Afya wa Kaunti, Harvey Mulei, alisema Hospitali ya Matiliku ilipokea majeruhi 28 na Hospitali ya Rufaa ya Makueni ikapokea 36. Manusura walieleza kuwa taa za gari zilikatika kabla ya kuacha barabara na kutumbukia shimoni. Haya yanajiri huku takwimu zikionyesha kuwa miundombinu duni ya barabara, ukosefu wa madaraja ya watembeao kwa miguu na alama za trafiki na uzembe wa madereva na watembea kwa miguu ni sababu nyingi zinazochangia ongezeko la vifo na majeraha barabarani. Hata hivyo, Shirika la Afya Duniani (WHO) linaonya kuwa idadi halisi ya vifo inaweza kuwa kubwa zaidi kuliko inavyoonyeshwa na takwimu rasmi. WHO inaeleza kwamba, Kenya huhesabu tu vifo vinavyotokea mara moja baada ya ajali, huku wengi wanaofariki hospitalini siku au miezi kadhaa baadaye wakiachwa nje ya rekodi hizo. Kwa mujibu wa Shirika la Kitaifa kuhusu Takwimu Kenya (KNBS), watu 114,466 walihusika katika ajali za barabarani kati ya 2021 na 2025. Katika kipindi hicho, watu 22,894 walifariki huku zaidi ya 90,000 wakijeruhiwa. Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama Barabarani (NTSA) inasema ongezeko la idadi ya watu, magari na msongamano wa trafiki limefanya hali kuwa mbaya zaidi.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 16 Aug 2026 08:39:36
Jack Nicholson Net Worth
Jack Nicholson has an estimated net worth of $400 million, making him one of the wealthiest actors in Hollywood history. His fortune has been built through more than five decades of film work, including substantial acting salaries, backend compensation and lucrative deals tied to some of his biggest movies. Beyond his earnings from acting, Nicholson [...] The post Jack Nicholson Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 16 Aug 2026 08:02:02
Peso Pluma Net Worth
Peso Pluma has an estimated net worth of $20 million. The Mexican singer and songwriter has built his fortune through music sales, streaming, songwriting, live performances, collaborations and other commercial ventures. Born Hassan Emilio Kabande Laija, Peso Pluma rose from Mexicos regional music scene to become one of the biggest names in contemporary música mexicana. [...] The post Peso Pluma Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 16 Aug 2026 08:11:10
Bridget Fonda Net Worth
Bridget Fonda is a retired American actress who has an estimated net worth of $50 million. Her wealth is combined with that of her husband, acclaimed film composer Danny Elfman. Best known for her roles in hit films such as Single White Female, Singles, Point of No Return, Jackie Brown, and A Simple Plan, Fonda [...] The post Bridget Fonda Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 16 Aug 2026 08:17:55
Peter Fonda Net Worth
Peter Fonda had an estimated net worth of $40 million at the time of his death in 2019. The American actor, director, producer and author built his fortune during a career spanning nearly six decades, with income coming from film and television acting, directing, producing, writing and other entertainment projects. Fonda became an icon of [...] The post Peter Fonda Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 16 Aug 2026 08:20:27
Seven-year-old boy drowns in dam while grazing cattle in Nyandarua
A seven-year-old boy drowned in a dam in Nyandarua Central Sub-County after he reportedly slipped and fell into the water while grazing livestock with two other children. The incident occurred at a dam near Stage One along the Passenga-Ol Kalou route on Saturday, August 15, 2026, at about 3.30pm. The incident was reported by a [...] The post Seven-year-old boy drowns in dam while grazing cattle in Nyandarua appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 16 Aug 2026 08:22:12
Mob attacks police officers during attempt to rescue murder suspect in Narok
Police officers in Narok County were forced to withdraw from Mogoto village after a mob turned on them while they attempted to rescue a murder suspect from an enraged crowd. The incident occurred on Saturday, August 15, 2026, at about 1.30pm in Mogoto village, Sagamian Location, Narok Amalo Sub-County. According to a police incident report, [...] The post Mob attacks police officers during attempt to rescue murder suspect in Narok appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 16 Aug 2026 07:55:53
Moto bondeni, Murkomen, Cheruiyot waking'ang'ania ubabe 2032
MVUTANO wa kisiasa, tamaa ya uongozi na mapambano ya kumrithi Rais William Ruto 2032 yanaanza kutishia kampeni yake ya kutafuta muhula wa pili 2027 katika Bonde la Ufa, eneo ambalo ni ngome yake kuu ya kisiasa. Makundi mawili yanaonekana kumakinikia siasa za urithi wa uongozi wa eneo huku baadhi ya viongozi wakituhumiwa kuelekeza nguvu zao kwenye uchaguzi wa 2032 badala kuhakikisha Rais Ruto anashinda uchaguzi wa 2027. Kiini cha mzozo huo ni ushindani wa kisiasa kati ya Waziri wa Usalama wa Ndani, Kipchumba Murkomen, na Kiongozi wa Wengi katika Seneti, Aaron Cheruiyot. Baadhi ya wabunge na viongozi wengine wameanza kujiunga na pande zinazowapigia debe wanasiasa hao wawili. Juhudi za kuwatafuta Mabw Murkomen na Cheruiyot kuhusu suala la kuanzisha kampeni za mapema za 2032 hazikufua dafu kwa kuwa hawakujibu simu au jumbe walizotumiwa Mbunge wa Belgut, Nelson Koech, amekiri kuwa mjadala kuhusu nani atamrithi Rais Ruto 2032 umeanza kutawala siasa za Bonde la Ufa, hali ambayo anasema inaweza kuvuruga kampeni za 2027. Bw Koech alikanusha kuwa anaegemea mrengo wa Seneta Cheruiyot, lakini akasema ushindani huo umeanza kusababisha migawanyiko unaotatiza kampeni za Rais Ruto. "Watu wamesahau kwamba kwanza tunapaswa kushughulikia 2027 kabla hata ya kufikiria 2032. Wanaojihusisha na siasa za urithi wanamdharau Rais kwa sababu huwezi kurithi kile ambacho baba yako bado anamiliki," akasema Bw Koech kwenye mahojiano na Taifa Leo. Mbunge huyo, ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi katika Bunge la Kitaifa, alionya kuwa viongozi wanaoanza kampeni za kumrithi kiongozi aliye madarakani kabla ya muda wake kuisha mara nyingi huishia kupoteza ushawishi na kuzama kisiasa. Alisema baadhi ya viongozi wenye nyadhifa za juu serikalini wanapaswa kuelekeza nguvu zao katika kumsaidia Rais Ruto kupata muhula wa pili badala ya kufuatilia maslahi yao ya kibinafsi. Kwa mujibu wa takwimu za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), kaunti zinazokaliwa na jamii ya Kalenjin—Nandi, Uasin Gishu, Bomet, Kericho, Elgeyo-Marakwet, West Pokot na Baringo—zinatarajiwa kuwa na zaidi ya wapigakura milioni 3.2 waliojiandikisha kufikia uchaguzi wa 2027. Idadi hiyo inaweza kuwa juu zaidi kutokana na uwepo wa Wakalenjin pia kwenye sehemu kubwa ya Kaunti ya Nakuru na pia Narok. Bw Koech alisema changamoto ya usajili wa wapigakura inapaswa kuwa kipaumbele badala ya viongozi kujihusisha na siasa za 2032. Alisema Wakalenjin milioni 1.2 bado hawajajisajili kupiga kura, hali ambayo inaweza kuathiri pakubwa juhudi za Rais Ruto kutafuta muhula wa pili. "Tunapaswa kutafuta mikakati ya kutatua tofauti zetu ili kwanza tushughulikie 2027. Kwa sasa kura kutoka Murang'a na Kiambu karibu zinaweza kufuta kura zote za Wakalenjin," akasema. Seneta wa Nandi Samson Cherargei naye amemvamia Bw Murkomen, akidai hamakinikii kampeni za Rais Ruto huku akimakinikia kuwasambaratisha viongozi wasiokuwa kambi yake . Bw Cherargei alisema hatakubali kulazimishwa kumuunga mkono Bw Murkomen na akapinga madai kwamba yuko katika kambi ya Bw Cheruiyot. "Sitamwaabudu. Hata akidhamini mgombea dhidi yangu, hatafanikiwa. Kwa nini anaendesha kampeni za 2032 na kuzua mvutano miongoni mwa viongozi badala ya kumsaidia Rais?" akauliza. Mnamo Agosti 5, Mbunge wa Keiyo South Gideon Kimaiyo pia alimkosoa Bw Murkomen hadharani, akidai anaingilia siasa za eneobunge lake. Bw Kimaiyo alisema viongozi wanapaswa kuacha za urithi na kuelekeza nguvu zao katika kuhakikisha Rais Ruto anamaliza muhula wake wa kwanza akiwa na rekodi nzuri ya maendeleo. Mbunge wa Aldai, Marriane Kitany, naye amewataka viongozi wa Bonde la Ufa kuwa na umoja, akisema ushindi wa 2027 haupaswi kuchukuliwa kuwa ushatimia. "Tusidhani kwamba tuna urais na kwamba Rais ashachaguliwa. Ukweli ni kwamba kura zetu zinahitajika ili Ruto achaguliwe tena na ashinde kwa idadi kubwa," akasema Bi Kitany pia alitetea rekodi ya maendeleo ya Rais Ruto katika eneo hilo, akitaja miradi mbalimbali ya miundombinu, viwanja vya michezo, nyumba za gharama nafuu na usambazaji wa umeme. Alisema viongozi wanapaswa kuhakikisha miradi hiyo inakamilika ili iweze kuwa msingi wa kampeni za 2027. Mzozo huo unatokea wakati Rais Ruto mwenyewe amekuwa akionyesha wasiwasi kuhusu kiwango cha usajili wa wapigakura Bondeni. Akizungumza katika mazishi Bomet mnamo Mei 1, Rais alisema Wakalenjin milioni 1.8 wenye vitambulisho hawajajisajili kupiga kura, huku wengine 500,000 waliofikisha umri wa miaka 18 pia wakiwa hawajajisajili. Alisema hali hiyo inamlazimisha kutafuta uungwaji mkono katika maeneo mengine ilhali ngome yake ina idadi kubwa ya wapigakura ambao bado hawajajiandikisha.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 16 Aug 2026 07:42:39
Jesús Ortiz Paz Net Worth
Jesús Ortiz Paz is a Mexican-American singer, songwriter, music executive and entrepreneur who has an estimated net worth of $25 million. Also known as JOP, Ortiz Paz is the lead vocalist and business leader of Fuerza Regida, one of the most commercially successful groups in modern música mexicana. Ortiz Paz has built his wealth through [...] The post Jesús Ortiz Paz Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content