kenyanews.go.ke
@kna Tue, 11 Aug 2026 10:25:50
Climate-smart farming provides solution to recurring crop failures
The drought spell being witnessed in various parts of the country is a wake-up call for Kenyan farmers to start embracing Climate Smart Agriculture (CSA). A shift to climate-smart agriculture will not only address food security and climate change but also ensure farmers cushion themselves from crop losses and greenhouse gas emissions. In the recently...
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 11 Aug 2026 09:56:25
Six arrested as DCI rescues three Indian nationals in suspected human trafficking case
Detectives from the Operations Support Unit (OSU) have arrested six suspects and rescued three Indian nationals who had been reported missing after arriving in Kenya on August 5, 2026. The Directorate of Criminal Investigations (DCI) said the three foreign nationals were traced to a two-bedroom house in Fort Jesus area of Ruiru, Kiambu County, following [...] The post Six arrested as DCI rescues three Indian nationals in suspected human trafficking case appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 11 Aug 2026 10:00:11
Migori main bridge collapses further, cutting off pedestrians and motorcyclists
A section of the Migori Main Bridge in Suna West Sub-County completely collapsed, posing a serious danger to pedestrians and motorcycle riders who have continued using the crossing despite its closure. The incident occurred on Monday, August 10, 2026, at around 7:47pm, according to police. The bridge had initially been reported damaged and partially collapsed [...] The post Migori main bridge collapses further, cutting off pedestrians and motorcyclists appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 11 Aug 2026 10:08:33
Kenya Power warns against expansion of wind and solar power over grid stability concerns
Kenya Power called for a cautious approach in expanding variable renewable energy (VRE) sources such as wind and solar, warning that their intermittent nature could expose the national electricity grid to instability and increase the cost of power for consumers. The company said wind and solar currently account for about 34 per cent of the [...] The post Kenya Power warns against expansion of wind and solar power over grid stability concerns appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 11 Aug 2026 10:00:28
Wito wa uwekezaji katika Kiswahili ili kisibaki nyuma kidijitali
ZAIDI ya wataalamu 200 wa lugha, wasomi, watengenezaji wa teknolojia na watunga sera kutoka kote Afrika Mashariki na Marekani (US) walikutana katika Chuo Kikuu cha Kisii wiki iliyopita kwa kongamano muhimu lililolenga kuhakikisha Kiswahili kinapata nafasi yake katika mustakabali wa kidijitali. Kongamano hilo la Kimataifa la Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki (CHAKAMA), lilijikita katika namna Akili Unde (AI), majukwaa ya kidijitali na teknolojia zinazoibuka zinaweza kutumiwa kukuza Kiswahili na kukiweka kama lugha yenye ushindani katika uchumi wa kidijitali duniani. Waliohudhuria walijumuisha wasomi kutoka vyuo vikuu vya Afrika Mashariki na maafisa kutoka taasisi za lugha, wawakilishi wa mashirika ya serikali, mashirika ya kitamaduni, pamoja na wasomi kutoka vyuo vikuu vya Marekani. Miongoni mwa wasomi mashuhuri waliohudhuria walikuwa Profesa Clara Momanyi wa Chuo Kikuu cha Kenyatta, mwandishi mashuhuri Profesa Kithaka Wa Mberia, mwandishi wa tamthilia na mtaalamu wa elimu Professa Chacha Nyaigoti Chacha, miongoni mwa wengine. Akizungumza wakati wa kikao cha ufunguzi, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kisii, Profesa Nathan Ogechi, alisema mkutano huo ulikuwa umefanyika kwa wakati mwafaka, wakati ambapo Kiswahili kinapata kutambuliwa kimataifa kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa. Mwaka 2021, shirika la UNESCO lilitangaza Julai 7 kuwa Siku ya Kiswahili Duniani, ikiwa ni mara ya kwanza kwa lugha ya Kiafrika kupewa hadhi hiyo ya kimataifa. "Utambuzi huo haukutokea kwa bahati. Ulidhihirisha ukweli kwamba Kiswahili kimekua na kuvuka mipaka ya Afrika Mashariki na kuwa lugha ya diplomasia, biashara na utamaduni barani Afrika na hata nje ya bara," alisema Profesa Ogechi. Leo, zaidi ya watu milioni 200 huzungumza Kiswahili barani Afrika na katika jumuiya za watu wanaoishi ughaibuni. Lugha hiyo pia inafundishwa katika vyuo vikuu kote Ulaya, Asia na Amerika Kaskazini. Ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kiswahili ni lugha rasmi na ni kichocheo muhimu cha ushirikiano wa kikanda, biashara na diplomasia. Hata hivyo, licha ya hadhi yake kuendelea kukua, wataalamu walionya kwamba Kiswahili kinaweza kuachwa nyuma katika ulimwengu wa kidijitali iwapo hatua za makusudi hazitachukuliwa. Profesa Ogechi alieleza changamoto kadhaa zinazoikabili lugha hiyo katika enzi ya Akili Unde. Changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa data ya kutosha kwa ajili ya kufundishia mifumo ya Akili Unde, rasilimali chache za kujifunzia kidijitali, ufadhili mdogo wa teknolojia ya lugha, pamoja na kuendelea kutawala kwa Kiingereza na lugha zingine za kigeni kwenye mitandao. "Zana za kidijitali hazipaswi kututisha. Kwa kweli, ndizo fursa yetu kubwa zaidi ya kupanua Kiswahili. Lakini ili hilo litimie, ni lazima tuwekeze katika utafiti, data na majukwaa yanayozungumza lugha yetu," aliongeza. Mwandishi wa tamthilia na mtaalamu wa elimu kutoka Kenya, Profesa Chacha Nyaigoti Chacha, alisema Kiswahili kimebadilika kutoka kuwa lugha ya mawasiliano ya kikanda na kuwa mojawapo ya lugha zenye ushawishi mkubwa zaidi barani Afrika. "Kiswahili kina utajiri mkubwa wa kimaana. Kina uwezo wa kusaidia utafiti wa kisayansi, ubunifu na uzalishaji wa maarifa. Kinachokosekana ni uwekezaji wa makusudi katika rasilimali za kidijitali ili kufungua uwezo huo," alisema Profesa Chacha. Alionya kwamba bila maudhui bora ya kidijitali, lugha hiyo itaendelea kutengwa katika ulimwengu wa mtandao, licha ya mamilioni ya vijana kutumia muda mwingi zaidi kwenye intaneti. Kongamano hilo lilipata msukumo mkubwa siku ya Ijumaa wakati Waziri wa Elimu, Julius Ogamba, alipohudhuria kikao cha kufunga na kuahidi msaada wa serikali. Bw Ogamba alisema Wizara ya Elimu itawasilisha pendekezo kwa Baraza la Mawaziri la kuanzishwa kwa Baraza la Kiswahili nchini Kenya. Chombo hicho kinachopendekezwa kitakuwa na jukumu la kuratibu utafiti, sera na maendeleo ya teknolojia kwa ajili ya lugha hiyo. "Hatuwezi kuruhusu lugha yetu ya kitaifa kuachwa nyuma katika mapinduzi ya kidijitali. Serikali iko tayari kushirikiana na vyuo vikuu, kampuni za teknolojia na taasisi za kikanda ili kuhakikisha Kiswahili kinaendelea kustawi mitandaoni," alisema Waziri huyo. Aliongeza kuwa kuunga mkono Kiswahili katika mazingira ya kidijitali pia ni suala la kuhifadhi utamaduni na kuunda fursa za kiuchumi kwa vijana. Bingwa wa Kiswahili na Ushirikiano wa Kikanda barani Afrika, Dkt Caroline Asiimwe, alisema ushirikiano wa kikanda utakuwa muhimu iwapo Kiswahili kitastawi katika enzi ya kidijitali. "Kusherehekea Siku ya Kiswahili ni muhimu, lakini ni lazima tuweke utafiti katikati ya juhudi hizi. Tunahitaji kuzalisha data ya lugha na kuishirikisha katika mipaka mbalimbali. Bila data, Akili Unde haiwezi kujifunza Kiswahili ipasavyo," alisema. Profesa Kithaka Wa Mberia, mwanaisimu mashuhuri, alisisitiza umuhimu wa kurekodi lahaja, misimu na matumizi ya kisasa ya lugha ili kufanya zana za Akili Unde kuwa na ufanisi zaidi. "Akili Unde inayoelewa Kiswahili cha vitabu pekee itafeli. Tunahitaji kuilisha lahaja kutoka Mombasa, Zanzibar na Dar es Salaam. Hivyo ndivyo tunavyoweza kuifanya iwe halisi kwa vijana," alisema Profesa Mberia. Profesa Clara Momanyi alisema ushirikiano kati ya serikali, vyuo vikuu na kampuni za teknolojia lazima uharakishwe ili kuunda zana zinazoweza kutumika kwa vitendo. "Tunahitaji kamusi za mtandaoni zinazofanya kazi, programu sahihi za kutafsiri, istilahi zilizosawazishwa kote duniani na mifumo ya kutambua sauti na miundo ya Akili Unde iliyofundishwa kwa Kiswahili. Mustakabali wa lugha hii uko katika teknolojia. Ikiwa hatupo kwenye majukwaa ya kidijitali, basi hatupo katika mazingira ambako vijana hujifunza na kubuni," alisema Momanyi. Dkt. Juliet Jagero, mwenyekiti wa CHAKAM na mhadhiri mkuu katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jaramogi Oginga Odinga (JOOUST), aliwataka watayarishaji wa maudhui ya kidijitali kuwajibika. "Kadiri Kiswahili kinavyoenea mitandaoni, ni lazima tuhakikishe maudhui tunayozalisha yanakuza umoja, maadili na misingi inayojenga na kuimarisha jamii zetu," alisema. Aliwataka waandishi na wataalamu wa vyombo vya habari kuunda maudhui zaidi ya Kiswahili kwa ajili ya hadhira ya vijana kupitia podikasti, blogu, tovuti za elimu na mitandao ya kijamii. "Hivyo ndivyo tunavyoweza kuhifadhi lugha na wakati huo huo kuunda ajira katika uchumi wa kidijitali," alisema Dkt Jagero. Majadiliano hayo yanafanyika wakati ambapo Kiswahili kinaendelea kupata umaarufu katika diplomasia, elimu na biashara za kuvuka mipaka. Taasisi za kikanda na mashirika ya kimataifa zinazidi kutumia lugha hiyo katika mawasiliano yao. Hata hivyo, wataalamu wanakubaliana kwamba hatua inayofuata ni teknolojia. Kuanzia roboti za mazungumzo hadi wasaidizi wa sauti na programu za kujifunza zinazotumia Akili Unde, lugha zitakazotawala zitakuwa zile zilizo na miundombinu bora zaidi ya kidijitali. Kwa Kenya na Ulimwengu mzima, mkutano wa Kisii uliashiria mwanzo wa kile ambacho wajumbe wanatumaini kuwa juhudi endelevu za kuhakikisha Kiswahili hakizungumzwi tu, bali pia kinaandikwa kwa misimbo ya kompyuta, kinatafsiriwa na kueleweka na mashine.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 11 Aug 2026 10:24:19
Viongozi wasizuiwe kufanya kampeni popote ingawa busara yawahitaji kuepuka uchochezi
KILA kiongozi anaruhusiwa kufanya kampeni mahala popote nchini kwa sababu Kenya ni taifa huru na kila mwanasiasa ana haki ya kuendeleza ajenda yake ya kisiasa. Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua ametangaza kuwa analenga kuzuru Kusini mwa Bonde la Ufa kwa misururu ya mikutano ya kisiasa ya kuuza chama chake cha DCP na azma yake ya urais. Kundi la Linda Mwananchi ambalo linaongozwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna nalo limetangaza kuwa litakuwa na mkutano mkubwa wa kisiasa Kaunti ya Homa Bay wikendi hii. Linda Mwananchi pia ina Gavana wa Siaya James Orengo, Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi miongoni mwa wanasiasa wengine. Mbunge wa Emurua Dikirr David Keter alinukuliwa akimtaka Bw Gachagua asitie guu katika eneobunge lake akisema kiongozi huyo wa DCP anastahili kuelekeza nguvu zake maeneo mengine. Bw Keter anadai kuwa Emurua Dikirr ni ngome ya kisiasa ya UDA. Viongozi wengine kama Seneta Aaron Cheruiyot (Kericho) na Jackson Mandago (Uasin Gishu) nao wamesema kuwa Bw Gachagua yuko huru kufika Bonde la Ufa lakini ajue anafanya kazi bure kwa sababu kura zake haziko huko. Kwa upande mwingine baadhi ya viongozi wa ODM kutoka Kaunti ya Homa Bay wamesema Linda Wananchi wako huru kuzuru kaunti hiyo lakini waepuke lugha ya matusi. Mbunge wa Homa Bay Opondo Kaluma amesema kuwa wanasiasa wa Linda Mwananchi hawafai kuwachokoza raia na kuwatusi huku Gavana Gladys Wanga akionya dhidi ya siasa za uhuni. Mwanzo, katiba iko wazi kuhusu kuzuru na kufanya kampeni kwa mwanasiasa yeyote na Bw Keter hafai kumzima Bw Gachagua asifike Emurua Dikirr. Hawa raia ambao mbunge huyu anamkataza Bw Gachagua asiwahutubie ndio wale wale ambao walimpigia mgombeaji wa DCP Vincent Rotich zaidi ya kura 10,000 kwenye uchaguzi mdogo miezi miwili iliyopita. Hata hivyo, Bw Gachagua naye anastahili kuchunga mdomo na asitoe matamshi ya kuwachochea raia dhidi ya viongozi wao kwa sababu matokeo ya kura yanaamuliwa debeni. Wakati mwingine mdomo wa Bw Gachagua ndio humchongea kwa sababu matamshi yake huwa yanajikita katika jamii moja nchini. Akienda Bonde la Ufa, auze ajenda yake na sera zake kuhusu jinsi atakavyobadilisha maisha ya Wakenya upinzani ukichukua mamlaka badala ya kutumia lugha isiyofaa na kuchochea fujo. Hii haimaanishi kuwa hafai kuzungumzia miradi ya maendeleo ambayo imefeli au ahadi ambazo serikali ilitoa na haijatimiza. Kila dai la Bw Gachagua linastahili kuandamana na ukweli badala ya uchochezi. Mabw Sifuna, Orengo na Owino nao wakifika Homa Bay wanastahili kuzungumzia ajenda yao ya kubadilisha eneo hilo badala ya kuvamia mrengo pinzani wa ODM unaoongozwa na Dkt Oburu Oginga. Watatu hawa wanafahamu fika kuwa Homa Bay ni kati ya kaunti ambazo zimenufaika pakubwa kimaendeleo kutokana na miradi kadhaa inayoendelea katika utawala huu wa Rais William Ruto. Kwa hivyo, wazungumzie mipango yao ya kustawisha na kuimarisha maisha ya watu badala ya kukosoa miradi inayoendelea ambayo kwa kweli inatarajiwa kubadilisha maisha ya watu wa eneo hilo.
read morekenyanews.go.ke
@kna Tue, 11 Aug 2026 09:40:00
Kajiado death registration remains low despite high birth registration rate
Kajiado County has recorded a wide disparity in civil registration, with birth registration compliance standing at 92.7 per cent while that of death stands at 25.2 per cent. County Civil Registrar Christine Gachau said the county's birth registration rate was above the national average of 71 per cent, but death registration remained significantly below the...
read morekenyanews.go.ke
@kna Tue, 11 Aug 2026 09:50:27
Recruitment agent arraigned over Sh350,000 fake job deal
A 32-year-old Eldoret-based jobs recruitment agent was yesterday arraigned before an Eldoret Court charged with obtaining Sh350,000 from a resident magistrate under false pretenses of securing a job abroad for her sister. Charles Onyimbo Monayo, allegedly told the magistrate he could secure a foreign job for her sister, took the cash, and disappeared. He was...
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 11 Aug 2026 09:49:01
Raila Junior responds to viral video of him addressing Kilgoris residents behind fence
Raila Odinga Junior has responded to a viral video showing him greeting residents from behind a fence in Kilgoris, clarifying the circumstances surrounding the encounter. The video sparked discussion on social media, with some users questioning why the son of former Prime Minister Raila Odinga appeared to be separated from members of the public by [...] The post Raila Junior responds to viral video of him addressing Kilgoris residents behind fence appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 11 Aug 2026 09:02:22
PS Omollo Issues Update on Construction of Mau Mau Road Lot 2 Project
Principal Secretary for the State Department for Internal Security and National Administration Raymond Omollo has issued an update on the ongoing construction of the Mau Mau Road Lot 2 project, which is expected to transform connectivity and economic activity across parts of Kiambu, Murang'a and Nyeri counties. The 154-kilometre project, being implemented by the Kenya [...] The post PS Omollo Issues Update on Construction of Mau Mau Road Lot 2 Project appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 11 Aug 2026 09:07:52
NCIA Launches Intelligence Profiling and Analytics Training for KRA Officers
The National Criminal Investigations Academy (NCIA) has commenced a five-day Intelligence Profiling and Analytics Course for officers from the Kenya Revenue Authority (KRA). The training is aimed at strengthening the officers' capacity in intelligence profiling, analysis and interpretation of information to support informed decision-making and intelligence-led enforcement within KRA. Speaking during the opening ceremony on [...] The post NCIA Launches Intelligence Profiling and Analytics Training for KRA Officers appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content