kahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 25 Jul 2026 04:33:42
Texts reveal 14-year-old allegedly murdered by singer D4vd had pregnancy and abortion
Texts between singer D4vd and Celeste Rivas Hernandez, the 14-year-old he is accused of murdering, reveal she had been pregnant and had had an abortion before her death. The messages were shown during a hearing for a judge to determine if the singer, whose legal name is David Anthony Burke, should go on trial for [...] The post Texts reveal 14-year-old allegedly murdered by singer D4vd had pregnancy and abortion appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 25 Jul 2026 04:35:56
Trump vows to investigate EU over fining of US tech companies
Donald Trump says the US will launch an investigation into the European Union and threatened a fresh tariff over fines handed to some of the biggest American tech companies. It comes days after the European Commission fined Google €890m ($1bn) for operating in a way that squeezed out competitors to its services. In a post [...] The post Trump vows to investigate EU over fining of US tech companies appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 25 Jul 2026 04:38:04
ICC top prosecutor removed over sexual misconduct allegations
Members of the International Criminal Court (ICC) have voted to dismiss Karim Khan as chief prosecutor for alleged sexual misconduct. Elected the ICCs third prosecutor in 2021, Khan was suspended last month. The decision to remove him was passed with 82 votes in favour. The courts oversight body found in June he had committed a [...] The post ICC top prosecutor removed over sexual misconduct allegations appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 25 Jul 2026 04:16:44
Tanzanian lecturer arrested over anti-government protests charged with terrorism
A Tanzanian university lecturer who was arrested earlier this month over allegations of inciting anti-government protests has now been charged with terrorism. Melkisedek Kaijage, who works at the University of Dodoma, had appeared at a magistrates court to request bail after spending 15 days in police custody when the charges were changed. He was among [...] The post Tanzanian lecturer arrested over anti-government protests charged with terrorism appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sat, 25 Jul 2026 03:55:34
Familia ya Sharon Otieno yafurahia uamuzi na kusema ni ukurasa mpya
FAMILIA ya Sharon Otieno imesema imepata afueni baada ya Mahakama Kuu kumpata na hatia aliyekuwa Gavana wa Migori Okoth Obado pamoja na wasaidizi wake wawili kwa mauaji ya binti yao, ikisema hukumu hiyo ni mwanzo wa ukurasa mpya baada ya kusubiri haki kwa karibu miaka minane. Akizungumza kwa simu na Taifa Dijitali Ijumaa, baba yake Sharon, Douglas Otieno, alisema ingawa haki imepatikana, hukumu hiyo imefufua maumivu ya kumpoteza binti yao. "Hata kama haki imetendeka na tunahisi afueni kidogo, bado hukumu hii imeturudisha kwenye maumivu ya zamani. Ni kana kwamba jeraha limetoneshwa. Tulikuwa mahakamani jana na hali ilikuwa ya kutuumiza sana kisaikolojia," alisema. Aliongeza kuwa familia sasa inaona mwanzo mpya baada ya kusubiri haki kwa miaka minane. Douglas Otieno na mkewe Melida Auma walizungumza kabla ya kurejea nyumbani kwao Homa Bay, wakisema sasa wanafahamu waliohusika na mauaji ya binti yao
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sat, 25 Jul 2026 02:55:33
Obado sasa ni kunywa uji na kuumwa na chawa gerezani
ALIYEKUWA Gavana wa Migori, Okoth Obado, Michael Oyamo na Caspal Obiero wameanza maisha mapya gerezani baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya mwanafunzi Sharon Otieno, kukikabiliana na utaratibu mkali wa maisha ya wafungwa. Watatu hao wataishi maisha anayopitia kila mfungwa bila kujali hadhi yake. Watatu hao walipelekwa katika Gereza la Mahabusu la Industrial Area Alhamisi jioni, lakini walikuta chakula cha jioni tayari kimekwisha. Wafungwa walikuwa wamemaliza ugali na maharagwe yaliyokuwa yameandaliwa, hivyo wakalazimika kulala bila chakula cha gerezani siku yao ya kwanza. Walikuwa wamekula matunda na kunywa soda kabla ya kuondoka Mahakama ya Milimani majira ya saa kumi na moja na nusu jioni. Katika gereza hilo, waliwekwa katika bweni Block G, sehemu ambayo mara nyingi hutumiwa kuhifadhi mahabusu na wafungwa mashuhuri. Walilala chumba kimoja na aliyekuwa Kamanda wa Kituo cha Polisi cha Nairobi Central, Samson Talaam, ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji ya mwalimu Albert Ojwang. Walikabidhiwa godoro, kitanda na blanketi kabla ya kufungiwa. Kwa Obado, hali hiyo ilikuwa na kejeli yake. Mnamo 2018 akiwa gavana, alitoa televisheni kwa Gereza la Industrial Area ili wafungwa waweze kufuatilia habari. Televisheni hiyo ndiyo iliyokuwa katika chumba alicholala usiku huo. Chumba hicho pia kiliwahi kutumiwa na aliyekuwa Mbunge wa Sirisia John Waluke na aliyekuwa Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu baada ya kupatikana na hatia katika kesi zao za ufisadi. Hii si mara ya kwanza kwa Obado na wenzake kufungwa katika Block G. Walikaa hapo Septemba 2018 walipokamatwa kwa mara ya kwanza kuhusiana na mauaji ya Sharon, kabla ya kuachiliwa kwa dhamana. Obado alikaa humo kwa siku 33. Baada ya kuhukumiwa, wafungwa hukabidhiwa rasmi kwa Huduma ya Magereza Kenya. Kwanza hupimwa afya, kisha hukabidhiwa sare mbili za gerezani huku nguo zao, simu, fedha, saa, vito na mali nyingine zikihifadhiwa hadi watakapoachiliwa. Afisa mmoja wa magereza alisema wafungwa hupangiwa sehemu ya kulala kulingana na kiwango cha hatari wanachoweza kusababisha na si hadhi yao. "Kanuni ni usawa. Wafungwa maarufu hawapaswi kupewa matibabu maalumu. Tunawapanga kulingana na kiwango cha hatari na hali zao," alisema. Maisha gerezani huanza saa kumi na mbili alfajiri kwa kuhesabiwa wafungwa. Hesabu hiyo hurudiwa mara kwa mara siku nzima. Kiamsha kinywa huwa uji iliyo na sukari kidogo. Baadaye wafungwa hukutana katika kikao kinachojulikana kama "bunge la wafungwa" kutoa malalamishi yao kabla ya kupangiwa kazi kama kupika, kulima au usafi. Chakula cha mchana huwa wali na maharagwe, ugali na maharagwe, ugali na mboga, ugali na nyama, githeri au viazi. Mlo wa mwisho hutolewa kati ya saa tisa na saa tisa na nusu alasiri, kisha wafungwa hurudishwa vyumbani kabla ya milango kufungwa saa kumi na mbili jioni. Familia zinaweza kutembelea wafungwa mara kwa mara, lakini kila ziara hudumu dakika zisizozidi 10 na husimamiwa na maafisa wa magereza. Simu hupigwa kupitia simu maalumu ya ustawi wa wafungwa, huku mazungumzo yakifanywa kwa Kiswahili au Kiingereza ili yaweze kufuatiliwa. Fedha pia haziwezi kukabidhiwa mfungwa moja kwa moja. Huwekwa kwenye akaunti yake kupitia ofisi ya ustawi, kisha hutumika kununua bidhaa katika duka la gereza. Afisa huyo alisema siku za kwanza gerezani huwa ngumu kwa wafungwa wengi kwani wengi hupitia mshtuko wa kisaikolojia. Kwa sababu hiyo, hupatiwa ushauri nasaha na maafisa wa ustawi pamoja na wafungwa waliopata mafunzo ya ushauri. Ingawa Obado alikuwa gavana aliyesimamia bajeti ya mabilioni ya pesa na misafara ya magari ya serikali, maisha yake sasa yatafuata ratiba sawa na ya maelfu ya wafungwa wengine: Kuamka alfajiri, kuhesabiwa mara kadhaa, kula chakula cha gharama nafuu, kufanya kazi anazopangiwa na kulala katika mabweni yenye wafungwa wengi huku akisubiri hukumu na rufaa yake.
read moreRight Column Content