taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 21 Jul 2026 18:40:41
Gavana asimulia kusutwa na Rais kwa wapigakura wachache Kaskazini licha uwekezaji mkubwa
GAVANA wa Garissa, Nathif Jama amefichua kuwa mkutano ulioitishwa na Rais William Ruto katika Ikulu mnamo Julai 13 haukulenga tu maendeleo ya Kaskazini Mashariki, bali pia ulijadili idadi ndogo ya watu wanaopata vitambulisho na kujiandikisha kama wapigakura. Bw Jama alisema Rais aliwataka viongozi wa Garissa, Wajir, Mandera, Marsabit na Isiolo kueleza kwa nini wananchi wengi bado hawana vitambulisho licha ya serikali kufuta mfumo wa wanaoomba vitambulisho. "Rais alituambia bado hatuwahamasishi watu wetu kupata vitambulisho na kujiandikisha kupiga kura. Tulitoka katika mkutano huo tukiwa na aibu," alisema. Alisema makadirio ya IEBC yanaonyesha Garissa itakuwa na wapigakura 258,926 pekee mwaka 2027, idadi ambayo alisema haiendani na wakazi zaidi ya milioni moja wa kaunti hiyo. Gavana wa Wajir Ahmed Abdullahi pia alisema viongozi waliagizwa kuongeza idadi ya watu wanaopata vitambulisho na kupendekeza maafisa wa usajili waende moja kwa moja katika shule za upili kuwasajili wanafunzi waliotimiza umri wa kupata kitambulisho. Chanzo kilichohudhuria mkutano wa Ikulu kilisema Rais aliwapa viongozi hao miezi mitatu kuongeza idadi ya waliojiandikisha kupata vitambulisho na wapigakura.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Tue, 21 Jul 2026 09:03:43
KNEC Outlines Steps to Download Digital KCSE Certificates
The development is expected to benefit thousands of former students who lost their KCSE certificates or had them withheld by their schools, with applicants required to pay a Ksh1,500 processing fee.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Tue, 21 Jul 2026 09:15:00
KPA Unveils Lamu Port Growth Plan Ahead of Dangote-Linked Refinery Project
The plans come months ahead of the Ksh2.2 trillion East African oil refinery firm linked to Nigerian businessman Aliko Dangote, which is expected to be constructed near the port.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Tue, 21 Jul 2026 12:35:12
Blow to Politicians as Police Threaten to Withdraw Security
The warning comes as authorities intensify a nationwide crackdown on political goons following a string of violent incidents that have disrupted public events, protests and elections.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Tue, 21 Jul 2026 15:36:12
Ruto Appoints Sossion to TSC, Picks New Govt Spokesperson
The new changes also saw the current Government Spokesperson, Isaac Mwaura, moved from his office and promoted, according to the statement shared by State House Spokesperson Hussein Mohamed.
read moreRight Column Content