taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 12 Jul 2026 05:55:19
Uvumi wa 'kupoteza uume' wazua hofu, vifo na mashambulizi Pwani
KILICHOANZA kama uvumi wa ajabu sasa kimegeuka kuwa chanzo cha hofu, vurugu na vifo katika baadhi ya maeneo ya Pwani, huku polisi na wataalamu wa afya wakikanusha madai kwamba mwanaume anaweza kupoteza sehemu zake za siri baada ya kuguswa na mtu mwingine. Uvumi huo, ambao hauna msingi wa kisayansi wala kitabibu, umefanya watu wengi kuishi kwa wasiwasi. Katika visa kadhaa, watu wasio na hatia wamepigwa na umati wenye hasira baada ya kutuhumiwa kwa madai hayo, huku wahalifu wakidaiwa kutumia taharuki hiyo kuiba simu, pochi na mali nyingine. Kisa kilichotikisa wengi kilitokea Nyali, Mombasa, ambapo waumini wa dhehebu ya Jehovah Witness wanne walishambuliwa walipokuwa wakihubiri kutoka nyumba moja hadi nyingine. Umati uliwalaumu kwa kuhusika na "kupotea" kwa sehemu za siri za wanaume kabla ya polisi kuwaokoa. Baadaye, wakazi wawili, Al Amin Mgunya Johnson na Kennedy Mersyden Milimo, walifikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka ya kuchochea vurugu. Milimo pia alishtakiwa kwa kosa la kumshambulia mmoja wa wahubiri hao. Wote walikana mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana. Mzee wa Mashahidi wa Yehova katika Jumba la Ufalme la Bamburi, Martin Henya, alisema madai hayo ni ya uongo na kusisitiza kuwa dhehebu hilo halihusiki kwa njia yoyote na uchawi au nguvu za kishirikina. Huku kesi hiyo ikiendelea mahakamani, familia moja Mombasa inaendelea kuomboleza baada ya John Kaleghe, mwenye umri wa miaka 24, kuuawa kwa kupigwa na umati katika Soko la Marikiti baada ya kutuhumiwa kwa madai hayo. Msemaji wa familia, Leah Mwandaghina, alisema Kaleghe alikuwa kitindamimba na tumaini la wazazi wake. Alisema familia ilimtafuta kwa siku kadhaa kabla ya kupata mwili wake katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Pwani. Kwa mujibu wake, majeraha aliyopata yalikuwa makubwa kiasi kwamba ilikuwa vigumu kumtambua. Familia pia inadai kuwa alikimbilia polisi kuomba msaada lakini hakufaulu kuokolewa kwa umati. Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) Pwani imesema tayari imerekodi visa 19 vinavyohusiana na uvumi huo katika kaunti za Mombasa, Kilifi na Kwale. Watu wawili tayari wameuawa kwa kupigwa na umma. Mratibu wa DCI Pwani, Benson Kasyoki, alisema watu wote waliodai kupoteza sehemu zao za siri walifanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kubainika hawakuwa na jeraha lolote wala mabadiliko ya viungo vyao. Alisema uchunguzi unaonyesha makundi ya wahalifu yanatumia uvumi huo kuwalenga watu, huku washirika wao wakiiba mali wakati umati unamzingira mtuhumiwa. Wakati huo huo, DCI imeanzisha uchunguzi wa video za CCTV na ujumbe unaosambazwa mitandaoni ili kubaini wanaochochea vurugu na kusambaza taarifa za uongo. Daktari wa mfumo wa mkojo, Dkt Omar Bin Salman wa Kliniki ya Mombasa Urology, alisema kisayansi haiwezekani kwa sehemu za siri za mwanaume kutoweka kwa kuguswa na mtu mwingine. Alifafanua kuwa mabadiliko ya muda yanayoweza kutokea hutokana na misuli ya mwili kujikaza, lakini haimaanishi kuwa kiungo kimepotea. Aliongeza kuwa kama sehemu hizo zingetoweka kweli, mgonjwa hangeweza kuenda haja ndogo na hiyo ingekuwa hali ya dharura inayohitaji matibabu ya haraka. Kwa sasa, maafisa wa usalama wanatoa wito kwa wananchi kupuuza uvumi huo, kutochukua sheria mikononi na kuripoti visa vyovyote kwa polisi.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 12 Jul 2026 04:55:51
Wantam! Mitandao ya siri ya Gen Z ya kuelekeza siasa za Kenya
KIFO cha Cecil Ouma baada ya hafla ya katibu wa vijana Jacob Fikirini kilifungua ukurasa ambao wengi wa Wakenya hawaufahamu kuhusu siasa za nchi. Kijana huyo alifariki baada ya kupigwa risasi akiwa ndani ya gari la afisa mkuu serikalini, lakini simulizi ya maisha yake imeibua mjadala kuhusu mtandao wa vijana wanaotumiwa kuhamasisha mikutano ya kisiasa, kulinda viongozi na wakati mwingine kuhusishwa na vurugu. Kwa wengi, vijana hao hujulikana kama "magenge" au "wahuni". Lakini ndani ya siasa, wao hujiita wahamasishaji – watu wanaoweza kukusanya mamia ya vijana kwa muda mfupi kwa mkutano, kampeni au shughuli nyingine za kisiasa. Hata hivyo, si wahamasishaji wote hufanya kazi kwa maslahi ya wanasiasa. Wapo pia wanaharakati wa kijamii wanaotumia mbinu hizo kuhamasisha wananchi kuhusu uwajibikaji, haki za kijamii na ushiriki katika uchaguzi. Mpiga picha Alans Ademba asema kazi yake inaongozwa na lengo, si fedha.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 12 Jul 2026 03:55:05
Mlimani: Gachagua kumkabidhi Uhuru ripoti hukusu 'ground'
MIKUTANO ya siku 45 inaoendelea nyumbani kwa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, Wamunyoro, Kaunti ya Nyeri, imeibuka kuwa jukwaa muhimu la kujadili mwelekeo wa kisiasa wa eneo la Mlima Kenya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Kwa mujibu wa duru zinazoshiriki katika mashauriano hayo, mojawapo ya mapendekezo yanayojitokeza ni kwamba, Bw Gachagua awanie urais, isipokuwa mahakama iamue kuwa hastahili kushikilia wadhifa wa umma kutokana na kesi yake ya kupinga kuondolewa mamlakani. Mkutano huo ulianza Juni 16 na unatarajiwa kukamilika Julai 31. Katika kipindi hicho, Gachagua amekutana na wajumbe kutoka Mlima Kenya, Nairobi na jamii ya Wamaasai. Akizungumza Jumamosi alipokutana na viongozi wa Ol Jororok, Gachagua alisema atatayarisha ripoti ya mashauriano hayo na baadaye kukutana na Rais (mstaafu) Uhuru Kenyatta. "Baada ya mkutano huu kukamilika nitampelekea Uhuru Kenyatta ripoti ya maoni ya wananchi. Hatutaki kurudia makosa ya 2022 ambapo tuliongoza jamii yetu kwa misimamo tofauti," alisema. Alieleza kuwa lengo la mkutano huo ni kusikiliza matarajio ya jamii na washirika wake kuhusu uongozi wanaotaka mwaka 2027 pamoja na masuala wanayotaka yawekwe mbele katika serikali ijayo.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 12 Jul 2026 02:55:27
Siasa za ubabe: Pesa itaongea katika uchaguzi wa 2027
IKIWA kuna jambo ambalo wachambuzi wa siasa wanakubaliana nalo, ni kwamba uchaguzi mkuu wa 2027 unatarajiwa kuwa wa gharama kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini. Kuanzia matumizi ya helikopta za kukodi, wataalamu wa kampeni, mikakati ya kidijitali hadi kampuni za tafiti za maoni, siasa zimegeuka kuwa biashara inayohitaji mabilioni ya fedha. Hali hii imezua hofu kwamba demokrasia inageuka kuwa uwanja wa matajiri na wafadhili wao pekee. Kutokana na hali hiyo, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imependekeza kanuni mpya za kudhibiti matumizi ya fedha za kampeni ili kuongeza uwajibikaji na uwazi. Chini ya mapendekezo hayo yaliyochapishwa Julai 6, 2026, mgombea urais ataruhusiwa kutumia hadi Sh4.44 bilioni katika kampeni, huku vyama vya kisiasa vinavyowasilisha wagombea kuanzia udiwani hadi urais vikipewa matumizi ya juu ya Sh17.7 bilioni. Wagombeaji wa ugavana, useneta na uwakilishi wa wanawake watatumia kati ya Sh12.3 milioni na Sh123 milioni kulingana na ukubwa wa eneo lao, huku wagombeaji wa ubunge wakiruhusiwa kutumia kati ya Sh17.5 milioni na Sh123 milioni. Wagombea udiwani watatakiwa kutumia kiwango cha juu cha kati ya Sh2.5 milioni na Sh20 milioni. Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon alisema kanuni hizo zinalenga kuhakikisha fedha za kampeni zinatumika kwa uwazi na uwajibikaji. Hata hivyo, kabla ya kanuni hizo kuanza kutekelezwa, mjadala kuhusu matumizi ya fedha umechacha, hasa kufuatia kampeni za uchaguzi mdogo wa Ol Kalou. Viongozi wa upinzani wakiongozwa na Rigathi Gachagua wameshutumu serikali kwa kutumia fedha nyingi na rasilimali za umma kushawishi wapigakura. "Maafisa wa serikali Ol Kalou ni wengi kuliko wapigakura. Helikopta zimejaa angani kiasi cha karibu kugongana," alisema Bw Gachagua. Katika taarifa ya pamoja, David Maraga, Kalonzo Musyoka, Martha Karua, Fred Matiang'i na Edwin Sifuna walidai vitendo hivyo vinakiuka Sheria ya Makosa ya Uchaguzi, ikiwemo kutoa hongo kwa wapigakura na matumizi ya rasilimali za umma kisiasa. Lakini msemaji wa serikali Isaac Mwaura alitaja madai hayo kuwa ya kupotosha, huku Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung'wah akidai ni ya uongo na propaganda. Mbali na kampeni zinazoonekana hadharani, kuna mtandao mkubwa wa wafadhili ambao hufadhili wagombeaji kwa siri licha ya sheria kuwataka kujitokeza wazi. Katika uchaguzi wa 2022, aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta aliwashawishi wafanyabiashara wa eneo la Mlima Kenya chini ya Mt Kenya Foundation kumuunga mkono Raila Odinga kupitia michango ya mabilioni ya fedha. Kwa upande mwingine, viongozi wa muungano wa upinzani wanakiri kuwa kukabiliana na nguvu za kifedha za serikali iliyoko madarakani ni changamoto kubwa. Profesa Karuti Kanyinga wa Chuo Kikuu cha Nairobi amewahi kukadiria kuwa kampeni za urais nchini hugharimu takriban Sh14 bilioni. Hata hivyo, Martha Karua anasema uchaguzi haupaswi kuamuliwa na fedha bali uadilifu na uwezo wa mgombeaji. Si mashindano ya fedha. Wakenya wanapaswa kuwachagua viongozi kwa tabia, rekodi na uwezo wao wa kuhudumia wananchi," alisema. Aliongeza kuwa chama chake hakitakopa wala kutumia rasilimali za umma kufadhili kampeni. Nao Dkt Fred Matiang'i, Seneta Okong'o Omogeni na aliyekuwa Waziri Mithika Linturi wameeleza wasiwasi kuhusu matumizi makubwa ya fedha na helikopta katika chaguzi ndogo za hivi majuzi. Mashirika ya kutetea demokrasia yameonya kuwa sheria za kufadhili kampeni tayari zipo lakini hazitekelezwi ipasavyo. Mkurugenzi wa Centre for Multiparty Democracy (CMD), Frankline Mukwanja, amesema IEBC inapaswa kusimamia kikamilifu utoaji wa taarifa za michango na matumizi ya kampeni kwa wakati halisi pamoja na kuwaadhibu wanaokiuka sheria. Kwa upande wake, mratibu wa Elections Observation Group (ELOG), Mulle Musau, alisema Sheria ya Ufadhili wa Kampeni ya mwaka 2013 tayari inaeleza vyanzo vinavyoruhusiwa vya fedha na inawataka wagombeaji kufichua wafadhili wao. Mchambuzi wa siasa Mark Bichachi anaamini upinzani utahitaji kutumia teknolojia zaidi kuliko fedha ili kushindana na serikali, huku Profesa Gitile Naituli akisisitiza kuwa ingawa fedha ni muhimu, hazitoshi kushinda uchaguzi. Bila utekelezaji madhubuti wa sheria na uwazi kuhusu fedha za kampeni, wadau wanaonya kuwa uchaguzi wa 2027 unaweza kutawaliwa na nguvu ya fedha badala ya sera, uongozi na maslahi ya wananchi.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sat, 11 Jul 2026 12:01:23
Kenya Met Lists Counties Set for Rains & Unusual Cold for Next 5 Days
According to Kenya Met, while about 15 countries will receive showers, cold weather is also likely to persist, with temperatures in some places dropping to as low as 5°C.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sat, 11 Jul 2026 12:40:10
Questions as DCP Truck Vandalised, Torched During Campaigns
The driver of the truck was alleged to have been kidnapped during the attack, with the incident coming less than 48 hours after IEBC threatened to cancel the by-elections over bribery and violence.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sat, 11 Jul 2026 14:10:19
KDF Begins Talks to Expand Military Cooperation With U.S. and Japan
This comes at a time when there continues to be a growing threat in the Indian Ocean waters over territorial boundaries, terrorism, and illegal fishing, among other things.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sat, 11 Jul 2026 16:23:29
KURA Confirms Dualling of Magadi Road
Residents living within the area have been urging the dualisation of the road to help contain the growing traffic volume, especially at peak hours, even as President Ruto has hinted at its expansion under NIF.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 11 Jul 2026 22:36:35
Parcel truck destroyed in fire on Isiolo–Mandera road
A parcel delivery truck transporting goods from Nairobi to Mandera was destroyed by fire on Saturday morning along the Isiolo–Mandera road in Wajir County. This saw many lose valuables of unknown values. The incident occurred Saturday at about 7:30am, involving a white Mitsubishi Fuso 10-wheeler operated by Tawakal Parcels Company. According to police, the driver, [...] The post Parcel truck destroyed in fire on Isiolo–Mandera road appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 11 Jul 2026 22:40:27
Three killed after BMW crashes into footbridge, bursts into flames on Nairobi's Raila Odinga Road
Three people were killed in a fiery road crash early Saturday morning after a BMW lost control and crashed into a footbridge along Raila Odinga Road in Nairobi's Kilimani area. The self-involved accident occurred at about 3:00 a.m. near the Riara Footbridge. Police said the vehicle was travelling from the Lang'ata direction towards the city [...] The post Three killed after BMW crashes into footbridge, bursts into flames on Nairobi's Raila Odinga Road appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content