taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Thu, 09 Jul 2026 07:55:08
Magenge ya wahuni wanawake yaongoza vurugu za kisiasa
KWA miongo kadhaa, taswira ya mhuni wa kisiasa nchini Kenya ilikuwa ya kijana asiye na ajira, aliyevalia fulana ya chama cha kisiasa na kurushia mawe wapinzani kabla ya kutoweka kwenye umati. Wanawake walikuwa na nafasi tofauti. Waliimba nyimbo za kampeni, walicheza, walishangilia na kuhamasisha wapigakura na kwa nadra walihusishwa moja kwa moja na vitendo vya vurugu. Hata hivyo, hali hiyo inaonekana kubadilika katika baadhi ya maeneo ya Kisii. Baada ya msafara wa kisiasa wa Linda Mwananchi kuvamiwa huko Keumbu, katika eneo la Nyaribari Chache Ijumaa iliyopita, wachunguzi waliwakamata wanawake sita na mwanamume mmoja kuhusiana na tukio hilo. Shambulio hilo lilisababisha kifo cha mtu mmoja, majeraha kwa wengine kadhaa na uharibifu wa magari mengi, likiwemo lililombeba aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga. Kukamatwa kwa washukiwa hao kumeibua mjadala kuhusu mwenendo mpya ambapo wanawake wanadaiwa kushiriki kikamilifu katika makabiliano ya kisiasa badala ya kubaki pembeni. Macho mengi sasa yameelekezwa kwa kundi la Ebirongo, linalofanya shughuli zake katika maeneo ya Nyaribari Chache. Kundi hilo lilianzishwa kama kikosi cha kuhamasisha vijana, lakini wanachama wake wanasema baadaye lilipanuliwa na kujumuisha wanawake kwa lengo rasmi la kuimarisha uhamasishaji wa jamii na kuwawezesha wanawake. Wanawake kadhaa waliozungumza bila kutaka kutajwa majina walisema ugumu wa maisha ndio uliowasukuma kujiunga na uhuni. Mjane mmoja mwenye umri wa miaka 31 alisema: "Nilijiunga na Ebirongo Januari mwaka huu. Niliambiwa ni kazi ya kumuunga mkono mheshimiwa. Lakini ukifika uwanjani unaambiwa, 'Zuia huyu asiongee.' Ukikataa, hupati chochote siku inayofuata. Nina familia. Sh1,000 kwa siku ni fedha nzuri." Mwanamke mwingine alisema miezi mingi ya kukosa ajira ilimlazimu kukubali uhuni wa kisiasa. Baadhi yao pia wanaamini wanawake hawashukiwi haraka kama wanaume, jambo linalowarahisishia kuingia kwenye mikutano ya wapinzani bila kuzua wasiwasi. Vurugu hizo pia zimeathiri uchumi wa Keumbu, huku wafanyabiashara wakilalamikia kuporomoka kwa biashara baada ya baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii kutoa wito wa kususia bidhaa kutoka eneo hilo.
read morekenyanews.go.ke
@kna Thu, 09 Jul 2026 07:35:41
Stakeholders back proposed reforms to streamline county business licensing
Business leaders, county officials and members of the public from West Pokot, Trans Nzoia and Turkana counties have welcomed the governments efforts to streamline business licensing through proposed amendments to the County Licensing (Uniform Procedures) Act, 2024, describing the reforms as a major step towards improving Kenyas business environment and attracting investment. The public participation...
read morekenyanews.go.ke
@kna Thu, 09 Jul 2026 07:38:21
Government rolls out digital livestock tracking system to curb banditry, leverage export market
The Ministry of Agriculture and Livestock Development has rolled out the Animal Identification and Traceability System (ANITRAC) in a move aimed at opening up the lucrative international export markets for Kenya's livestock products. According to Agriculture Cabinet Secretary, Mutahi Kagwe, the program will also ensure that Kenya complies with international sanitary and phyto-sanitary standards demanded...
read morekenyanews.go.ke
@kna Thu, 09 Jul 2026 07:39:47
PS Makokha urges church to support BETA through faithful stewardship
Principal Secretary (PS) for Economic Planning Dr. Bonface Makokha has called on religious leaders to partner with the Government in advancing the Bottom-Up Economic Transformation Agenda (BETA), saying the country's economic development depends on faithful stewardship, integrity and collective responsibility. Speaking during the Brethren to Brethren Prayer Breakfast at Pan Africa Christian (PAC) University in...
read morekenyanews.go.ke
@kna Thu, 09 Jul 2026 07:47:15
Government rolls out digital learning infrastructure to transform education
The government has intensified the rollout of digital learning infrastructure in public schools, as part of efforts to prepare learners for the digital economy and improve access to quality education across the country. Speaking during the commissioning of a smart board at Ol Kalou Comprehensive School, Principal Secretary for ICT and Digital Economy Eng. John...
read moreRight Column Content