kahawatungu.com
@kahawatungu Wed, 14 Oct 2026 05:20:00
Five arrested after man found dead in Kisii club
Police in Kisii County arrested five people to assist with investigations into the death of a 51-year-old man whose body was discovered inside a club at Kiango Shopping Centre in Kenyenya Sub-County. The deceased, identified as Peter Ombeo, was found dead on the floor of Armstrong Club in Kiango Sub-location on October 13, 2026. The [...] The post Five arrested after man found dead in Kisii club appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Wed, 14 Oct 2026 05:23:04
David Robinson Net Worth
David Robinson is a retired American professional basketball player and entrepreneur who has an estimated net worth of $300 million. He built his wealth through a successful NBA career, during which he earned approximately $116 million in salary, and a business career that expanded into real estate, private equity and other investments. Known as "The [...] The post David Robinson Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Wed, 14 Oct 2026 04:19:29
Blow to Kalonzo as Tribunal Blocks Azimio's Change to Ukombozi Alliance
The latest ruling now adds to growing woes in the opposition even as the leaders argue that they remain united to field a single presidential candidate to challenge President William Ruto in 2027.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 14 Oct 2026 03:55:23
Kenya kusubiri siku 21 kabla ya kutangazwa haina Ebola- Wataalamu
WIKI baada ya mgonjwa wa Ebola aliyekuwa ameingia Kenya kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia Uganda kufariki, hakuna kisa kingine kilichothibitishwa nchini kufikia sasa. Wataalamu wa afya wanasema licha ya kutokwepo kwa maambukizi mapya, Kenya italazimika kusubiri siku 21 ndipo itangazwe kuwa huru kutokana na Ebola. "Kila siku inayopita bila dalili inatupa sababu zaidi ya kutumaini kuwa maambukizi ya pili na kuenea kwa virusi ndani ya nchi kumezuiliwa." Akasema Dkt Ahmed Kalebi, mtaalamu wa magonjwa na mtafiti wa afya ya umma. Wizara ya Afya imesema watu 122 waliokutana na mgonjwa huyo wametambuliwa na kuthibitishwa. Kati yao, 108, sawa na asilimia 88.5, wamewekwa karantini na kufuatiliwa kila siku. Hakuna aliyekuwa amepata dalili kufikia taarifa ya Oktoba 11. Sampuli 293 zimepimwa, lakini ni ya mgonjwa huyo pekee iliyopatikana na virusi. Zaidi ya wasafiri 667,675 wamechunguzwa katika vituo 26 vya kuingia nchini. Profesa Shem Otoi, mtaalamu wa kukabili magonjwa yanayoenea na Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Daystar, naye anasema mchakato wa kuwafuatilia wagonjwa haupaswi kukomeshwa kwa sababu mtu ni mzima. "Wasiwasi mkubwa zaidi ungekuwa tukio tofauti kisa ambacho hakiwezi kuhusishwa na mgonjwa anayejulikana," alisema. "Sihofu kisa kimoja au viwili vilivyoletwa kutoka nje. Hofu yangu ni maambukizi ya ndani na ikiwa tutafikia siku ya mwisho bila maambukizi ya ndani, basi tutakuwa salama kama nchi," akaongeza. Mtaalamu huyo aliongeza kuwa Kenya inaweza kuzuia maambukizi ikiwa itawatambua watu wote walio katika hatari, kuwafuatilia na kukatiza kila mnyororo mpya wa maambukizi. Profesa Omu Anzala, mtaalamu wa virusi na mwanachama Jopo la Kupambana na Kuenea kwa Ebola, naye anasema siku 21 zikikamilika ndipo Kenya itakuwa huru dhidi ya maradhi hayo. "Ni baada tu ya siku 21 ndipo unaweza kuthibitisha kuwa kweli hakuna maambukizi mapya," akasema. Ebola haisambazwi kupitia hewa, bali kwa kugusana moja kwa moja na damu au majimaji ya mwili ya mtu aliyeambukizwa au aliyefariki kutokana na ugonjwa huo.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 14 Oct 2026 04:55:03
Faini ya Sh2m, jela miaka mitano kwa kuendesha uchaguzi nje ya vituo rasmi
WABUNGE wanapendekeza sheria kali kwa maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) wakiendesha uchaguzi katika vituo ambavyo havijaidhinishwa rasmi. Maafisa hao wataweza kutozwa faini ya Sh2 milioni au kifungo cha miaka mitano jela, au adhabu zote mbili wakipatikana na hatia. Pendekezo hilo limo katika Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Makosa ya Uchaguzi wa mwaka 2024, ambao unatarajiwa kujadiliwa katika hatua ya kamati katika Bunge la Kitaifa wiki hii. Mswada huo unalenga kuimarisha uadilifu wa uchaguzi kwa kuhakikisha matokeo yanayotangazwa na maafisa wa IEBC yanatoka vituo vilivyoidhinishwa rasmi kupitia tangazo la serikali. Kwa sasa, kuendesha uchaguzi katika kituo kisichoidhinishwa hakujatajwa kama kosa la uchaguzi chini ya sheria inayotumika kwa sasa. Mswada huo unapendekeza kurekebisha kifungu cha sita cha Sheria ya Makosa ya Uchaguzi ili kuingiza kosa hilo pamoja na makosa mengine yanayohusiana na kutangaza na kubadilisha matokeo. Pia, maafisa wa IEBC watakaochelewesha bila sababu kutangaza matokeo ya uchaguzi au kubadilisha kimakusudi matokeo yaliyokwisha kutangazwa watakuwa wakitenda kosa la uchaguzi. Mswada huo uliofadhiliwa kwa pamoja na Kiongozi wa Wengi katika Seneti, Aaron Cheruiyot (Kericho), na mwenzake wa Wachache, Stewart Madzayo (Kilifi), ulitokana na mapendekezo ya Kamati ya Mdahalo wa Kitaifa (Nadco). Ripoti ya Nadco iliidhinishwa na Bunge mnamo Februari 2024, baada ya mazungumzo ya pande mbili yaliyolenga kupunguza joto la kisiasa kufuatia maandamano yaliyosababisha vifo baada ya uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022 kupingwa na kiongozi wa wakati huo wa Azimio, Raila Odinga. Seneti iliidhinisha mswada huo Novemba 19, 2024, kabla ya kuwasilishwa katika Bunge la Kitaifa, ambako ulisomwa kwa mara ya kwanza Desemba 3, 2024. Katika uchaguzi mkuu wa 2022, IEBC iliidhinisha vituo 46,232 vya kupigia kura, ikilinganishwa na vituo 40,883 katika uchaguzi wa 2017. Hata hivyo, kesi iliyopinga matokeo ya urais ya 2017 ilidai kuwa vituo visivyoidhinishwa vilianzishwa kinyume cha sheria katika Kaunti ya Mandera na kusimamiwa na maafisa ambao hawakuwa wameteuliwa rasmi. Vilevile, kesi iliyopinga ushindi wa urais wa 2022 ilielezea hitilafu katika upeperushaji wa matokeo, ikidai kuwa matokeo kutoka zaidi ya vituo 11,000 ambavyo havikuwa vimeidhinishwa yalijumuishwa katika hesabu ya mwisho. Kanuni za Uchaguzi za mwaka 2022 zinahitaji IEBC kutangaza rasmi vituo vya kupigia kura, maeneo yake na nambari zinazovitambulisha.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Wed, 14 Oct 2026 03:04:05
Actress Selma Blair faces charges for kicking nurse and officer after plane incident
US actress Selma Blair has been charged with two additional assault counts over allegedly kicking an officer and a nurse after being removed from a flight. Blair was arrested late Sunday in New York after she allegedly attacked flight attendants on a Delta plane travelling from Los Angeles to New York. The FBI issued her [...] The post Actress Selma Blair faces charges for kicking nurse and officer after plane incident appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Wed, 14 Oct 2026 03:06:30
Saudi man charged with planting 'sophisticated' recording device in OpenAI office
A Saudi national has been charged with secretly planting a recording device in one of OpenAIs offices in California, federal prosecutors announced. Abdulrahman Alfozan, who worked at the AI firm as an engineer, was charged federally with using or endeavoring to use an electronic, mechanical, or other device to intercept oral communications. OpenAI said it [...] The post Saudi man charged with planting sophisticated recording device in OpenAI office appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Wed, 14 Oct 2026 03:08:57
Argentina targets UK in legal claim over Falklands oil exploration
The Argentinian government has begun legal action seeking to stop the exploration of oil and gas fields north of the Falkland Islands in an escalating row with the UK. Buenos Aires said in a statement the request lodged with the International Tribunal for the Law of the Sea aimed to block activity authorised illegally by [...] The post Argentina targets UK in legal claim over Falklands oil exploration appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Wed, 14 Oct 2026 03:11:10
Pope diagnosed with lung cancer but had successful surgery, Vatican says
Pope Leo XIV has been diagnosed with lung cancer but had successful surgery to remove a lower lobe of his right lung, the Vatican has said in a medical bulletin. The 71-year-old underwent a 90 minute surgery on Tuesday at Romes Gemelli Hospital and was subsequently diagnosed with lung adenocarcinoma. The operation was successful and [...] The post Pope diagnosed with lung cancer but had successful surgery, Vatican says appeared first on Kahawatungu.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Wed, 14 Oct 2026 03:00:00
Misplaced anger? President Ruto chases 'ghosts', turns Uhuru and Sifuna into bogeymen
Ruto accused Uhuru of breaking their political understanding that each would serve as president for 10 years, claiming the former president turned against him when he sought to succeed him.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Wed, 14 Oct 2026 02:59:00
Ex-gang boss sentenced to 40 years for orchestrating Tupac Shakur's murder
Former gang boss Duane Keffe D Davis has been sentenced to at least 40 years in prison for orchestrating the murder of Tupac Shakur. A jury found Davis, 63, guilty in September of one count of murder with a deadly weapon for the rap superstars death in a drive-by shooting in Las Vegas on 7 [...] The post Ex-gang boss sentenced to 40 years for orchestrating Tupac Shakurs murder appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Wed, 14 Oct 2026 03:01:46
Bank of America hit with $1.2bn fine for money laundering failings
Bank of America has been fined $1.2bn (£910m) for failing to detect potential money laundering and other illegal activity, the US Treasury Department said on Tuesday. The banking giant failed to report over $5bn in suspicious activity to the government, $1bn of which posed national security and illicit finance risks, the Treasury said. Those failures [...] The post Bank of America hit with $1.2bn fine for money laundering failings appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 14 Oct 2026 02:55:06
Gachagua asitasita kuhusu mgombeaji wa upinzani
CHAMA cha Democracy for Citizens Party (DCP) kinakabiliwa na jaribio la kwanza la umoja wake huku baadhi ya wanaowania tiketi katika uchaguzi wa 2027 wakilaumu kiongozi wake Rigathi Gachagua na maafisa wakuu kwa kupendelea washirika wao. Mvutano huo unazua maswali kuhusu ahadi ya chama hicho ya kuwaruhusu wanachama kuamua wagombeaji wao kupitia kura za mchujo zilizo huru na za haki. Hali hii inajiri huku Bw Gachagua akisema mazungumzo ya kuunda muungano wa upinzani yatasubiri hadi viongozi wa vyama husika waimarishe ngome zao za kisiasa kabla ya kuafikiana kuhusu mgombeaji mmoja wa urais. Akizungumza na wafuasi wake mjini Dracut, Massachusetts, nchini Amerika, Bw Gachagua aliwataka wawe na subira akisisitiza kuwa upinzani haujachelewa kujiandaa kwa uchaguzi wa 2027. "Hatuko nyuma kwa wakati. Tuko ndani ya muda unaofaa. Muungano unaweza kuundwa tu baada ya viongozi wenye ushawishi kuimarisha ngome zao," alisema. Alipuuza madai kwamba upinzani umegawanyika au unashindwa kupata mgombeaji mmoja wa urais, akiahidi kuwa DCP itajitolea kuhakikisha vyama vinaungana. "Ninaweza kuwahakikishia kuwa mgombeaji tutakayempata atawafurahisha. Wakenya wanataka mshindi wa uchaguzi apatikane katika awamu ya kwanza. Muungano utakuwa muhimu, lakini si wakati huu kwa DCP. Chama changu na mimi tutajitolea kuhakikisha tunapata mgombeaji mmoja," alisema. Hata hivyo, huku akitoa hakikisho hilo kwa wafuasi wake, malalamishi yalikuwa yakiongezeka ndani ya DCP kuhusu jinsi chama kitakavyowachagua wagombeaji wa viti mbalimbali. Baadhi ya wanaowania tiketi wanamlaumu Bw Gachagua na mwenyekiti wa baraza la watu mashuhuri la chama hicho, Bw Maina Kamanda, kwa kudhoofisha demokrasia ya ndani ambayo DCP ilijivunia wakati wa mchujo kuelekea uchaguzi mdogo wa Ol Kalou. Wanasema kiongozi huyo amekuwa akiwapigia debe wagombeaji anaowapendelea, huku Bw Kamanda akidokeza kuwa baadhi ya washindani wanaweza kunyimwa tiketi hata wakishinda kura za mchujo. Akizungumza katika kituo cha redio cha Inooro FM mnamo Septemba 22, Bw Kamanda alisema chama hakitawapa tiketi baadhi ya wagombeaji licha ya kushinda mchujo. "Hatuwezi kuwaruhusu watu waliokuwa upande wa wanaotusuta waje dakika za mwisho na kuwashinda wale waliosimama imara na chama pamoja na uongozi wake," alisema, akitaja Kaunti ya Kirinyaga kama mfano wa wanaoweza kunyimwa tiketi kwa misingi ya uaminifu wao. Kauli hiyo imewaudhi baadhi ya wanaowania tiketi, ambao sasa wanataka uongozi utoe hakikisho kwamba mchakato huo utakuwa wa haki, wazi na unaozingatia matakwa ya wanachama. Mvutano huo ni muhimu kwa sababu DCP imekuwa ikitumia kura za mchujo za Ol Kalou kuthibitisha kujitolea kwake kwa demokrasia ya ndani. Katika zoezi la Julai, wanachama 23,763 walipiga kura, sawa na asilimia 32.6 ya wapigakura 72,997 waliojiandikisha katika eneo hilo. Bw Sammy Kamau Ngotho alishinda tiketi ya chama kwa kura 12,947, kabla ya kuibuka mshindi wa uchaguzi mdogo kwa kura 35,440 dhidi ya kura 5,450 za mgombeaji wa United Democratic Alliance (UDA). Bw Gachagua alitaja zoezi hilo kuwa la kihistoria, akisisitiza kuwa DCP haina utaratibu wa kutoa tiketi moja kwa moja bila kura za mchujo na kwamba wananchi ndio wanaopaswa kuamua. Hata hivyo, baadhi ya wagombeaji sasa wanahofia kuwa utaratibu huo hautatumika katika maeneo mengine. Wasiwasi huo uliongezeka wakati wa ziara yake nchini Amerika, ambapo Bw Gachagua aliwaambia wakazi wa Spokane kuwa Bi Wambui Nyutu ndiye atakayekuwa mbunge wa Maragua kupitia DCP. Kauli hiyo ilimkasirisha mpinzani wake katika kinyang'anyiro cha tiketi ya chama, Bw Jimmy Mbaki, ambaye alisema ilikuwa ishara kuwa matokeo ya kura za mchujo yalikuwa tayari yameamuliwa. "Ni ushahidi gani mwingine ninaohitaji kujua kuwa ninapoteza muda wangu ndani ya DCP?" alisema. Alilinganisha wagombeaji wanaoendelea kuamini mchakato huo na ng'ombe anayeingia mwenyewe kichinjioni licha ya kuwa na nguvu za kupambana. Bw Mbaki alidai kuwa viti vya ubunge vya Maragua, Kigumo na Gatanga tayari vimetengewa wagombeaji wanaopendelewa na Bw Gachagua. "Kura za mchujo za DCP zitakuwa utaratibu wa kutimiza wajibu tu. Wanaodhani kutakuwa na haki wanajidanganya. Tayari natafuta chama kingine," alisema. Hata hivyo, uongozi wa DCP umepuuzilia mbali madai ya upendeleo, ukisema kila mgombeaji atapata nafasi ya kushindana. Kaimu Katibu mkuu wa chama hicho, Bw John Methu, aliambia gazeti la Taifa Leo kuwa wagombeaji hawapaswi kuchukulia mazungumzo ya kisiasa kama maamuzi rasmi ya chama. "Watu wanapaswa kuepuka kuchukulia mazungumzo ya kisiasa kwa uzito kupita kiasi. Tunafanya mikutano rasmi na wagombeaji na tunachowaambia wote ndicho kitakachotekelezwa," alisema. Bw Methu alisisitiza kuwa hakuna anayehakikishiwa tiketi, hata Bw Gachagua mwenyewe katika kinyang'anyiro cha urais kupitia chama hicho. Alionya kuwa DCP haitakubali ushindi unaopatikana kupitia udanganyifu, hongo au vurugu. "Hakuna tiketi itakayotolewa kwa ushindi uliopatikana kwa udanganyifu. Hakuna atakayeshinda tiketi kwa kutumia vurugu au hongo," alisema. Mchambuzi wa siasa Mixson Gitau alisema wagombeaji wanapaswa kuelewa kuwa vyama vinaweza kuzingatia mambo mengine zaidi ya matokeo ya kura za mchujo. Alitaja uaminifu kwa chama, uwezo wa kushinda uchaguzi na uadilifu kama baadhi ya mambo ambayo yanaweza kuzingatiwa.
read moreRight Column Content