taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Thu, 22 Oct 2026 05:55:52
Biashara ya mitihani bandia yazidi kuwaumiza wazazi
WAZAZI wanaendelea kutumia maelfu ya pesa kununua karatasi za mazoezi na mitihani ya kutabiri maswali yanayoweza kutokea katika mitihani ya kitaifa, hali inayoongeza mzigo kwa familia zinazokabiliwa na gharama kubwa ya maisha. Biashara hiyo inahusisha karatasi za kutabiri maswali, mitihani ya majaribio, majibu na vikundi vya WhatsApp vinavyotoza ada kwa wanafunzi wanaotaka kujiandaa kwa mitihani. Uchunguzi umebaini kuwa baadhi ya wauzaji huchapisha karatasi wakidai zimetoka shule maarufu kama Alliance High School, Maranda High School na The Kenya High School, wakitumia sifa za shule hizo kuwashawishi wazazi kuzinunua. Hata hivyo, si rahisi kuthibitisha uhalisi wa karatasi hizo, huku baadhi ya mazoezi yakiwa hayajaidhinishwa na Taasisi ya Ukuzaji Mitaala nchini (KICD). Zaidi ya wanafunzi 3.6 milioni wanatarajiwa kufanya tathmini na mitihani ya kitaifa mwaka huu. Kati yao, 1,380,463 watafanya tathmini ya shule za msingi (KPSEA), 1,206,028 tathmini ya Sekondari Msingi (KJSEA), huku 1,048,355 wakifanya mtihani wa KCSE. Wauzaji hutangaza karatasi za mazoezi kwa bei ya kuanzia Sh100 hadi maelfu ya shilingi, kutegemea muda wa usajili na aina ya nyenzo zinazotolewa. Baadhi ya majukwaa ya mtandaoni hutoza Sh290 kwa saa 24 za matumizi, Sh590 kwa mwezi, Sh940 kwa miezi sita na Sh1,480 kwa mwaka. Mzazi mmoja ambaye mtoto wake anafanya KCSE alisema gharama inaongezeka kila anaponunua kifurushi kipya cha karatasi hizo. "Kila unapofikiria kuwa umemaliza kulipia mahitaji yote, kifurushi kingine cha mazoezi kinatokea. Unaambiwa hiki kina maswali bora zaidi au wanafunzi wengine wanakitumia. Unaogopa kumnyima mtoto wako kitu kinachoweza kumsaidia," alisema. Mzazi mwingine alisema tayari alikuwa amenunua vitabu na mitihani ya zamani, lakini mtoto wake aliendelea kuomba karatasi zinazosambazwa katika vikundi vya WhatsApp. Wadau wa elimu wanaonya kuwa baadhi ya wauzaji wanatumia hofu ya wazazi kwa kuahidi kutabiri maswali yatakayotokea katika mitihani halisi. Mkuu wa Baraza la Mitihani nchini (KNEC), Dkt David Njengere, amewahi kuwaonya wazazi dhidi ya kununua karatasi hizo, akisema ni kupoteza muda na pesa. Mwalimu mkuu mmoja alisema kununua vifurushi vingi hakumaanishi mwanafunzi atapata alama za juu. "Mwanafunzi aliyejiandaa vizuri kwa kutumia mitihani ya zamani, vitabu na nyenzo zinazotolewa na walimu anaweza kufanya vizuri bila kununua karatasi nyingi zizothibitishwa," alisema. Alionya kuwa biashara hiyo inawafanya wanafunzi kuamini kuwa hawawezi kufaulu bila kununua karatasi fulani, jambo linaloongeza wasiwasi kwa watoto ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuzilipia. Wakati huo huo, Waziri wa Elimu Julius Ogamba ameonya kuwa watahiniwa na maafisa watakaopatikana wakijihusisha na udanganyifu wa mitihani watachukuliwa hatua kali za kisheria. KNEC pia imewaonya wazazi dhidi ya matapeli wanaodai kuwa na mitihani iliyovuja kabla ya kufanywa, ikisema wengi huuza karatasi bandia kwa familia zisizokuwa na habari.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 22 Oct 2026 05:23:47
Two men die in Tana River shooting as father and son arrested
Police in Tana River County have arrested a man and his son in connection with a shooting incident in Wolesorea area that left two men dead. The second victim, Maulid Yussuf Dayib, who had fled the scene during the initial shooting, was later found hiding in a nearby bush with two gunshot wounds to the [...] The post Two men die in Tana River shooting as father and son arrested appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 22 Oct 2026 05:28:24
Alison Arngrim Net Worth
Alison Arngrim has an estimated net worth of $1 million. She is an American actress, comedian, author and activist best known for playing Nellie Oleson on the NBC television drama Little House on the Prairie. Arngrim joined the series in 1974 at the age of 12 and appeared in more than 100 episodes before the [...] The post Alison Arngrim Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 22 Oct 2026 05:35:50
EACC recovers Sh12.57 million from former Homa Bay Assembly Clerk, two others
The Ethics and Anti-Corruption Commission (EACC) has secured a court order compelling former Homa Bay County Assembly Clerk Bob Kephas Otieno and two others to pay back Sh12.57 million in public funds fraudulently transferred from the Assembly's salary suspense account between 2015 and 2017. In a judgment delivered on October 16, 2026, Justice Benjamin Musyoki [...] The post EACC recovers Sh12.57 million from former Homa Bay Assembly Clerk, two others appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 22 Oct 2026 05:40:11
One dead, two rescued as landslide hits Meru quarry, three trapped
One person died, two others were rescued, and three are feared trapped after a landslide struck a mining quarry in Mutonga Village, Igoji, Meru County. The incident occurred on Wednesday, October 21, 2026, at Mutonga One quarry. According to police, the landslide was reported, prompting officers from Igoji Police Station and the Directorate of Criminal [...] The post One dead, two rescued as landslide hits Meru quarry, three trapped appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 22 Oct 2026 05:41:52
Karen Grassle Net Worth
Karen Grassle has an estimated net worth of $1.5 million. She is an American actress and author best known for portraying Caroline Ingalls, also known as Ma, on the NBC television series Little House on the Prairie. She starred alongside Michael Landon for eight seasons, becoming one of the most recognisable television mothers of the [...] The post Karen Grassle Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 22 Oct 2026 05:45:06
Woman drowns in Kirinyaga stream after suspected epileptic seizure
A 22-year-old woman drowned in a stream in Karuru Village, Kirinyaga East Sub-County, after she reportedly suffered an epileptic seizure while washing clothes. The deceased, identified as Faith Wanjiru Kithinji, was found dead in the stream in Kianjiru Sub-location, Baragwi Location, on Wednesday, October 21, 2026. According to police, Wanjiru, who had a history of [...] The post Woman drowns in Kirinyaga stream after suspected epileptic seizure appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content