kahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 11 Aug 2026 05:24:22
Man found dead inside food kiosk in Uasin Gishu
Police in Kesses, Uasin Gishu County, are investigating murder after a 50-year-old man was found dead inside a makeshift food kiosk. The deceased was identified as Mike Shikaro, a resident of Sukunanga Village. His body was discovered on Monday morning, August 10, 2026, by a woman who had gone to open her makeshift kiosk along [...] The post Man found dead inside food kiosk in Uasin Gishu appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 11 Aug 2026 05:26:53
70-year-old man hacked to death during land clearing in Migori
A 70-year-old man was hacked to death by his nephew while clearing a piece of land for planting in Kuria East, Migori County. Police identified the deceased as Peter Barante Mogesi, who was attacked at Kogori Village on Sunday, August 9, 2026. According to police, Mogesi was clearing the land with his 13-year-old grandson, William [...] The post 70-year-old man hacked to death during land clearing in Migori appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 11 Aug 2026 05:27:29
NOCK advertises CEO position; here's how to apply
The National Oil Corporation of Kenya (NOCK) has advertised the position of Chief Executive Officer (CEO), with applications set to close on August 28, 2026. NOCK announced the vacancy in a notice issued on Tuesday, August 11, 2026, inviting qualified candidates to apply for the position. The successful candidate will succeed Duncan Waziri, who has [...] The post NOCK advertises CEO position; here's how to apply appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 11 Aug 2026 05:37:35
TAWWDA Invites Suppliers and Contractors to Register for 2026-2028
The Tanathi Water Works Development Agency (TAWWDA) has invited suppliers and contractors to apply for registration to provide goods, services and works during the 2026/2027 and 2027/2028 financial years. In a notice issued on Tuesday, August 11, 2026, TAWWDA said it was seeking sealed applications from eligible candidates for registration under various categories. The agency [...] The post TAWWDA Invites Suppliers and Contractors to Register for 2026-2028 appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 11 Aug 2026 02:55:46
Ruto: Kushinda ni lazima, hatuna hiari; nikifikiria jinsi nchi itakuwa mikononi mwao nashtuka
RAIS William Ruto na Kinara wa ODM Dkt Oburu Oginga jana walibuni kamati ya watu watano kutoka kila upande ili kuibuka na rasmi na manifesto ambayo watatumia kujivumisha kuelekea uchaguzi wa 2027. Wawili hao jana waliwaambia viongozi wa Serikali Jumuishi kwamba hawana hiari ila tu kushinda Uchaguzi Mkuu 2027, huku zikibuni ushirikiano ambao utahakikisha Rais anatetea wadhifa wake. Akizungumza jana kwenye warsha ya siku tatu ya viongozi wa muungano wa Serikali iliyofanyika Naivasha, Kaunti ya Nakuru, Rais Ruto alisema muungano mpya sio tu kwa sababu ya kuimarisha mamlaka bali kuamua mustakabali wa nchi. Alionya kuwa ushindi wa upinzani utahujumu manufaa ambayo usimamizi wake unadai umefanikisha hadi leo. Rais aliwahimiza viongozi wa vyama hivyo viwili kufanya kazi pamoja na kuuzia wapigakura sera yao, akisawiri upinzani kuwa usio na mpangilio na unaokosa ajenda bayana. "Katika uchaguzi ujao ni sharti tushinde, kwa neema ya Maulana, kwa sababu hatuna hiari. Ni vigumu kutafakari kuhusu uwezekano kinyume. Inshallah, hatuna budi kushinda uchaguzi ujao sio kwa sababu yenu bali kwa maslahi ya Kenya," akasema Rais Ruto. Kiongozi wa nchi alisema Serikali Jumuishi ina ajenda dhahiri ya maendeleo na rekodi ya kutetea kinyume cha upinzani alioshutumu kwa kukosa maono na rekodi ya utendakazi. "Nikiangalia chaguo mbadala ninashtuka. Kundi la watu wasio na maono wala ajenda ni hatari kwa nchi. Chaguo mbadala ni vigumu kutafakari. Upande huo ni tafrani na wanachoweza tu kufanya ni kutapatapa na kunungúnika wanapoulizwa kuhusu rekodi yao ya utendakazi," akaongeza. Matamshi hayo yalijiri huku Rais akiashiria kuwa uhusiano kikazi kati ya UDA, ODM huenda ukageuka kuwa muungano rasmi kabla ya kinyang'anyiro cha 2027. Rais alisema mwongozo na ajenda ya kampeni ya muungano utajikita kwenye nakala inayotarajiwa kuibuka kutokana na warsha ya Naivasha. Kongamano hilo lilijumuisha wabunge 250, maseneta 46, magavana 20, manaibu magavana 20 na mawaziri, akiwemo Naibu Rais Kithure Kindiki, Kinara wa Mawaziri Musalia Mudavadi, Kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Kimani Ichung'wah na kiongozi wa wengi katika seneti Aaron Cheruiyot. Rais Ruto alitaja kongamano hilo kuwa moja kati ya mikutano mikubwa zaidi ya viongozi waliochaguliwa katika historia ya nchi, na wa pili baada ya kongamano la muungano mkuu ulioandaliwa na aliyekuwa rais Mwai Kibaki na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga. "Si rahisi kuwaleta pamoja wabunge 250, maseneta 46 na maafisa wengine wakuu serikalini kama tulivyofanya leo. Hii inathibitisha hizi ndizo kambi mbili kubwa zaidi kisiasa nchini na ninaheshimika kuwa kinara wa moja yake," alisema. Rais alisema uamuzi wake kuridhiana na marehemu Raila Odinga baada ya uchaguzi 2022 ulisukumwa na hamu ya kukomesha migawanyiko kisiasa na kutafuta nyanja za kuungana kati ya kambi hizo mbili. Alisema pande hizo mbili ziliafikiana kuhusu mipango ikiwemo nyumba za gharama nafuu, mpango wa afya kwa wote na kuimarisha uchumi. Rais alisema kuingia kwa maafisa wa ODM serikalini kulisaidia kuharakisha utekelezaji wa ajenda yake ya uongozi, akimsifu Waziri wa fedha John Mbadi. Dkt Oginga, aliyeongoza kongamano hilo pamoja na Rais Ruto, alitetea uamuzi wa chama chake kufanya kazi pamoja na serikali, akisema ulihitajika kuwezesha utulivu nchini na kuendeleza ajenda yake ya maendeleo. Bw Oginga alisema ODM hapo awali iliingia kwenye mikataba kisiasa na Serikali Jumuishi lakini akahoji kuwa ushirikiano wa sasa katika ulipatia chama hicho nafasi kubwa zaidi serikalini. "Kabla ya kujiunga na serikali, tulikuwa na 'handisheki' na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta. Hata hivyo, katika mpangilio huo hatukupata nafasi hata moja serikalini isipokuwa tu kuahidiwa kuungwa mkono kwa urais 2022," akasema Dkt Oginga. Bw Oginga alisema ODM ilikuwa imerejea kwenye upinzani kabla ya kujiunga na serikali ambapo wanachama kadhaa waliteuliwa katika baraza la mawaziri. Alisema chama hicho kimejiandaa kupigia debe azma ya Rais Ruto ya kubadilisha Kenya kuwa uchumi ulioendelea duniani. Aliwakabili vilevile viongozi wasiofurahishwa na muungano akiwataka kutangaza hadharani msimamo wao badala ya kubaki fufutende. "Watu wazue masuala kwa ukweli, lakini usiwe fufutende. Ni sharti uamue umesimama wapi, kwa kuwa tunataka kujua ni nani yuko nasi na wale ambao hawako nasi." Bw Oginga alisema muungano unaandaa sera zitakazoongoza ushirikiano kuelekea uchaguzi 2027.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 11 Aug 2026 03:55:54
Wetang'ula, Mudavadi waambia Sifuna bado hajaiva kupata kura kila pembe ya nchi
VITA vya kisiasa vya kung'ang'ania kura za Magharibi vimezidi kushika kasi baada ya Kinara wa Mawaziri Musalia Mudavadi na Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang'ula kupinga azma ya Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kuwania urais 2027. Kwa mara ya kwanza, viongozi hao wawili walimlenga moja kwa moja kiongozi huyo wa Linda Mwananchi, wakisema hana uzoefu wa kutosha kisiasa wala uungwaji mkono wa kitaifa kumwezesha kuingia Ikulu. Mvutano huo unajiri huku eneo la Magharibi likitarajiwa kuwa na zaidi ya wapigakura milioni 3.3 katika uchaguzi wa 2027. Akizungumza nyumbani kwa aliyekuwa mwenyekiti wa ANC Ken Lunani mjini Busia Jumapili, Bw Mudavadi alisema Bw Sifuna anakabiliwa na kazi ngumu kupata kura zinazohitajika kushinda urais. "Ili uwe Rais lazima upate zaidi ya asilimia 25 katika kaunti 24. Hata ukipata kura zote katika kaunti hizi tano, bado utahitaji kura kutoka maeneo mengine, kwa sababu Katiba inahitaji kaunti 24," akasema. Alitaja Busia, Kakamega, Vihiga, Bungoma na Trans Nzoia, akisema hata iwapo mgombea angezinyakua zote, bado angehitaji uungwaji mkono mkubwa katika maeneo mengine. Bw Mudavadi aliwakumbusha wapigakura kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga alipata kura milioni 6.5 katika uchaguzi uliopita, huku Rais William Ruto akipata karibu milioni 6.7. Alisema kura za Magharibi pekee hazitoshi kwa mgombea yeyote kuingia Ikulu na akawahimiza wakazi wa eneo hilo kumuunga mkono Rais Ruto katika uchaguzi wa 2027. Kwa upande wake, Bw Wetang'ula alisema mtu hawezi kuamka leo na kutangaza azma ya kuwa Rais bila kuwa na uzoefu wa kisiasa. Alisema viongozi waliowahi kuongoza Kenya walipitia safari ndefu na madhila ya kisiasa yaliyowapa uzoefu wa kuendesha serikali kabla ya kufika Ikulu. Spika huyo alisema nafasi nzuri zaidi kwa Magharibi kupata Rais ni mnamo 2032 badala ya 2027. Kauli hizo zinajiri huku makundi kadhaa ya kisiasa yakipigania ushawishi katika eneo hilo. Kambi ya Linda Mwananchi inayoongozwa na Bw Sifuna inajumuisha Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi, Seneta wa Kakamega Boni Khalwale, Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya na wabunge Wanami Namboka na Oundo Mudenyo. Kambi nyingine inaunga mkono Serikali Jumuishi na inawashirikisha Mabw Mudavadi, Wetang'ula, Waziri wa Vyama vya Ushirika Wycliffe Oparanya na Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli. Pia kuna wabunge wa Kakamega wanaomsukuma Bw Oparanya awe mgombea mwenza wa Rais Ruto, huku kiongozi wa DAP-Kenya Eugene Wamalwa akiongoza kambi nyingine ya upinzani. Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya anahoji ikiwa kambi ya Bw Sifuna inalenga kumng'oa Rais Ruto au inamakinikia kumjenga seneta huyo kuwa kinara wa Waluhya. Umaarufu wa Bw Sifuna umeanza kuwatia hofu baadhi ya viongozi ndani ya Serikali Jumuishi. Utafiti wa TIFA uliofanywa kati ya Juni 13 na 22 na kuwashirikisha watu 2,048 ulimweka Rais Ruto wa kwanza katika asilimia 24, huku Bw Sifuna akiwa wa pili kwa asilimia 15, kutoka asilimia 10 mnamo Mei. Utafiti huo pia ulimweka Bw Sifuna mbele ya wagombea wengine wa urais katika eneo la Magharibi.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 11 Aug 2026 04:55:54
Maandalizi yashika kasi Kenya ikijiandaa kuanzisha kiwanda chake cha kwanza cha nyuklia
KENYA inajiandaa kuanza kuzalisha nishati kwa kutumia nuklia huku kiwanda chake cha kwanza cha nuklia kikipangiwa kuzinduliwa rasmi Machi, mwaka ujao. Machi 25, 2026, Rais William Ruto alitangaza kuhusu mpango wa nuklia nchini katika kongamano la kimataifa kuhusu Nishati ya Nuklia lililoandaliwa jiji kuu la Nairobi. Maandalizi sasa yameshika kasi Kenya ikijiandaa kuanzisha kiwanda chake cha kwanza cha nuklia. Mradi huo uliopendekezwa unakadiriwa kugharimu takriban Sh500 bilioni na umepangiwa kuzinduliwa katika kijiji cha Lenya, Kaunti ya Siaya, eneo lililotambuliwa kuwa mwafaka zaidi, kwa mujibu wa Taasisi ya Nishati na Kawi ya Nuklia (NuPEA). Mradi huo umekadiriwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027, ukitengewa mgao wa Sh80 milioni kufadhili shughuli za "Eneo la Kiwanda cha Kawi ya Nuklia," ikiwemo uhandisi na udadisi kiufundi, yanaashiria makadirio ya bajeti yaliyowasilishwa katika Bunge la Kitaifa. Hata hivyo, maswali tele yamezuka kuhusu Kenya ilivyojiandaa kuhakikisha usalama wa umma, manufaa kijamii, tishio kwa afya na mazingira kutokana na uzalishaji kawi kinuklia. Mwezi uliopita, wabunge na maseneta walitaka ufafanuzi wa kina kutoka kwa NuPEA, katika kikao cha Kamati ya Seneti kuhusu Kawi. Kamati hiyo inayoongozwa na Seneta wa Siaya, Oburu Odinga ilihoji kuwa mchakato wa kutathmini eneo mwafaka pekee unaweza kuchukua karibu mwaka mmoja ikisaili tarehe ya uzinduzi. Seneta wa Kakamega Bonni Khalwale alisaili mikakati ya dharura inayohitajika kwa mradi kama huo ikiwemo kusaidia serikali ya Siaya kuanzisha Hospitali ya Level 5 na kuboresha miundomsingi kijamii. Mbunge wa Rarieda, Otiende Amollo alisisitiza haja ya kuangazia kikamilifu masuala ya kisayansi yanayohusiana na kawi ya nuklia, akisema bado hajajua eneo hasa la mradi huo. Alihoji kuwa mikakati ya kulinda mazingira ni sharti ipatiwe kipaumbele ikizingatiwa Ziwa Victoria linakidhi maelfu ya wanajamii eneo hilo. "Kihistoria, kawi ya nuklia haijahusishwa na matokeo bora. Masuala ya kisayansi yanahitaji kujibiwa kikamilifu," alisema Mbunge Amollo. Mkurugenzi wa NuPEA, Justus Wabuyabo aliwahakikishia kwamba sekta ya nuklia duniani imeboresha mikakati yake ya usalama. Alisema Kenya imepiga hatua kupitisha mikataba minne ya kimataifa kuhusu usalama wa nuklia iliyoidhinishwa na Baraza la Mawaziri Juni 30,2026, akifichua kuwa taasisi hiyo inasubiri uamuzi wa Bunge la Kitaifa. "Leo hii, kiwanda cha nuklia hakiwezi kuvuja kwa sababu ya mikakati ya usalama iliyowekwa," alisema Bw Wabuyabo.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 10 Aug 2026 20:18:03
How to Respond When an Auto Insurer Lowballs Your Injury Claim
Missouri roadways saw 961 traffic deaths in 2024, and St. Louis was not spared. The city recorded a 187% jump in pedestrian fatalities that year, with 23 lives lost, while St. Louis County saw 36 pedestrian deaths, both record highs. When you add speeding, distraction, and impaired driving into the mix, it is no surprise [...] The post How to Respond When an Auto Insurer Lowballs Your Injury Claim appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 10 Aug 2026 20:26:52
Ultimate Guide To Choosing The Perfect Pearl Necklace
When it comes to picking a pearl necklace, it seems a far more complex task than imagined. With so many pearl types, lengths, colors, and designs available, it can be difficult to know which one truly suits your style and needs. What may seem like a beautiful necklace online might not have the same appearance, [...] The post Ultimate Guide To Choosing The Perfect Pearl Necklace appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 10 Aug 2026 20:33:11
7 Benefits Of Choosing A Foldable Wheelchair For Everyday Use
It shouldnt be a logistics puzzle to get through an entire day that is completely normal. But for anyone stuck with a bulky, rigid wheelchair, thats exactly what happens. It wont fit in the trunk. It will not pass through a small doorway. A simple errand becomes a two-person task, and frustration levels begin to [...] The post 7 Benefits Of Choosing A Foldable Wheelchair For Everyday Use appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 10 Aug 2026 20:37:43
Top 6 Direct Mail Automation Platforms For Marketers
Marketing teams have to manage lots of data, remember multiple deadlines, and coordinate with multiple vendors simultaneously. Direct mail has declined but still uses many manual processes, even in the era of digital marketing tools. Maintaining mailing lists for export, working with print vendors, and monitoring delivery can take precious time that may be better [...] The post Top 6 Direct Mail Automation Platforms For Marketers appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 10 Aug 2026 20:57:32
ODM, UDA constitute two committees for coalition framework
The United Democratic Alliance (UDA) and the Orange Democratic Movement (ODM) have resolved to constitute two committees, one that will help establish a coalition framework and the other to prepare a joint manifesto in preparation for the August 2027 General Election. Making the announcement after a two-day retreat of the ODM-Kenya Kwanza/UDA retreat in Naivasha [...] The post ODM, UDA constitute two committees for coalition framework appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content