taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sat, 08 Aug 2026 04:55:58
Umoja: Kalonzo ateua washirika wa Gachagua katika uongozi wa Wiper
KIONGOZI wa Wiper Patriotic Front , Kalonzo Musyoka Ijumaa alitangaza mabadiliko katika uongozi wa chama hicho kwa kuwateua washirika wa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, huku akilenga kuonyesha umoja wa upinzani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Bw Musyoka alimteua aliyekuwa waziri, Jamleck Kamau kuwa mwenyekiti wa chama, Mbunge wa Nyali, Mohamed Ali kuwa naibu kiongozi wa chama, na wakili wa masuala ya Katiba Ndegwa Njiru kuwa msemaji wa chama. Uteuzi huo ulianza kutekelezwa mara moja na unaashiria upanuzi mkubwa wa uongozi wa Wiper vyama vya upinzani vinapoendelea na mashauriano kuhusu muungano w kukabiliana na Rais William Ruto mwaka 2027. Bw Kamau, ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Kigumo, amewahi kuhusishwa kisiasa na Bw Gachagua, huku Bw Njiru akiwa mmoja wa mawakili mashuhuri waliowahi kumtetea kiongozi huyo wa DCP. Bw Musyoka alisema uteuzi huo ulitokana na jukumu alilopewa na wajumbe wa chama wakati wa Kongamano la Kitaifa la Wajumbe la Oktoba 10 mwaka jana. "Jukumu la kwanza nililopewa na wajumbe lilikuwa kutafuta urais wa Jamhuri ya Kenya mnamo Agosti 2027. Jukumu la pili lilikuwa kupanua na kujenga uongozi wa chama hiki hadi kiwe sura ya Kenya," alisema. Alisema mabadiliko hayo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha Wiper pamoja na muungano mpana wa upinzani kuelekea uchaguzi wa 2027. Bw Musyoka alisema mashauriano yanaendelea kuunganisha vyama vinavyopinga utawala wa Rais Ruto chini ya mwavuli mmoja wa kisiasa. "Huu si uteuzi wa kujipendekeza, bali ni uteuzi wa imani. Kila mmoja wao anafaa kikamilifu katika chama ambacho ajenda yake pekee ni 'Komboa Kenya'," alisema. Kando na mabadiliko hayo ya uongozi, Bw Musyoka alisema hataruhusu tofauti kati ya viongozi wa upinzani kuvuruga juhudi za kuunda muungano mmoja dhidi ya Rais Ruto. Alisema viongozi wa upinzani wanaendelea na mashauriano ya kuleta pamoja Wakenya na akaonya kuwa mgawanyiko utawanufaisha viongozi wa Kenya Kwanza. "Tunapoendelea na kazi hii, mashauriano yanaendelea ili kuleta upinzani chini ya mwavuli mmoja wa kuaminika. Tumekubaliana kuwa mgawanyiko ndiyo mkakati pekee wa utawala huu," alisema. Bw Musyoka pia aliwataka Wakenya kutotafsiri tofauti zinazojitokeza kati ya viongozi wa upinzani kama ishara kwamba mchakato wa kuunda muungano umevunjika. "Hata mkiona tofauti kati ya viongozi wa vyama ndani ya muungano, tafadhali msizichukulie kwa uzito sana. Tumeungana kwa sababu tukigawanya upinzani, William Ruto atapata muhula wa pili," alisema. Alisema mashauriano yataendelea hadi vyama na viongozi wote wanaopinga serikali waungane. "Mashauriano hayo yanaendelea na hayatasitishwa hadi kila chama na kila kiongozi anayepinga serikali awe chini ya paa moja, tayari kuunda serikali moja inayosubiri kuchukua uongozi," alisema.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 08 Aug 2026 04:34:30
Barron Hilton Net Worth
Barron Hilton was an American businessman, hotel executive, pilot and sports entrepreneur who had an estimated net worth of $4.5 billion at the time of his death in 2019. He was the son of hotel pioneer Conrad Hilton, the founder of Hilton Hotels, and played a major role in transforming the family business into one [...] The post Barron Hilton Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 08 Aug 2026 04:40:56
Francesca Hilton Net Worth
Francesca Hilton was an American actress, comedienne and writer who had a net worth of $10,000 at the time of her death in January 2015. Despite being the only child of actress and socialite Zsa Zsa Gabor and hotel magnate Conrad Hilton, Francesca Hilton experienced significant financial difficulties during the later years of her life. [...] The post Francesca Hilton Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 08 Aug 2026 04:47:38
Zsa Zsa Gabor Net Worth
Zsa Zsa Gabor was a Hungarian-born actress and socialite who had an estimated net worth of $20 million at the time of her death in December 2016. She died at the age of 99 after a long career in Hollywood and decades as one of the worlds most recognizable socialites. Gabor first attracted attention in [...] The post Zsa Zsa Gabor Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sat, 08 Aug 2026 04:14:50
Dangote Sets Construction Date for Lamu Oil Refinery, Cuts Project Cost
The refinery is expected to become one of the largest private-sector investments in Kenya and will create thousands of jobs across construction, engineering, and logistics.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 08 Aug 2026 04:16:58
Connie Francis Net Worth
Connie Francis was an American singer who had an estimated net worth of $25 million at the time of her death in 2025. She was one of the most successful female pop singers of the late 1950s and early 1960s, known for hits including "Who's Sorry Now?," "Everybody's Somebody's Fool," "My Heart Has a Mind [...] The post Connie Francis Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 08 Aug 2026 04:24:16
Bobby Darin Net Worth
Bobby Darin was an American singer, songwriter, musician and actor who had an estimated net worth of $700,000 at the time of his death in 1973. Adjusted for inflation, that amount would be worth approximately $5 million today. Darin rose to international fame in the late 1950s with songs including "Splish Splash," "Dream Lover," "Mack [...] The post Bobby Darin Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sat, 08 Aug 2026 03:55:01
Hofu virusi vya ukimwi vikizidi kukosa kusikia dawa muhimu
WANASAYANSI wamegundua hali mpya ya kutisha ya virusi vya Ukimwi kuanza kustahimili dawa muhimu inayotumika katika matibabu ya ugonjwa huo katika nchi nne za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Utafiti uliowasilishwa katika mkutano wa International Aids Society (IAS) mjini Rio de Janeiro, Brazil, umeonyesha hali hiyo miongoni mwa watu wanaoishi na Ukimwi nchini Kenya, Tanzania, Msumbiji na Lesotho. Watafiti wameonya kuwa hali hiyo ikiendelea, maambukizi mapya ya Ukimwi yanaweza kuongezeka. Kinga ya mwili ya wagonjwa ambao virusi vyao vitakuwa vimekuwa sugu kwa dawa hiyo inaweza pia kudhoofika na kuwa katika hatari ya kupata magonjwa mengine ambayo yanaweza kusababisha kifo. Dawa inayohusika ni dolutegravir, inayojulikana kwa kifupi kama DTG. Tangu 2018, dawa hiyo imekuwa chaguo la kwanza na la pili katika matibabu ya Ukimwi. Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema DTG ina ufanisi mkubwa, ni rahisi kutumia na husababisha madhara machache ikilinganishwa na baadhi ya dawa nyingine zinazotumika. Dawa hiyo pia inajulikana kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia virusi vya Ukimwi kuzoea na kustahimili matibabu. Daktari Loice Ombajo, mtafiti mkuu wa utafiti huo na mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza, alisema sampuli za kwanza za utafiti zilikusanywa kutoka kwa watu 2,994 katika vituo 131 nchini Kenya. Washiriki hao walikuwa wametumia matibabu yenye DTG kwa angalau miezi sita. Baadhi ya washiriki waliopatikana kuwa na mabadiliko ya virusi yanayohusishwa na usugu wa DTG waliingizwa katika utafiti maalumu ili kupata ushahidi wa kusaidia kuboresha matibabu ya wagonjwa ambao dawa hiyo imeshindwa kuwasaidia. "Bado kuna ushahidi mdogo kuhusu namna ya kuwahudumia watu wanaoishi na Ukimwi ambao virusi vyao vimekuwa sugu kwa dolutegravir," alisema Dkt Ombajo. Alisema utafiti huo unalenga kutoa ushahidi utakaosaidia wataalamu kufanya maamuzi bora kuhusu matibabu ya wagonjwa hao. Takriban watu tisa kati ya 10 wanaotumia DTG hufikia kiwango ambacho virusi vya HIV havionekani kwa wingi katika damu. Hata hivyo, baadhi yao hushindwa kufikia kiwango hicho. Dkt Ombajo alisema sababu kubwa ni kutotumia dawa ipasavyo. Alisema baadhi ya wagonjwa huchoka kutumia dawa kila siku, wengine husahau, huku wengine wakikosa hamu ya kuendelea na matibabu kutokana na hali yao. "Usipotumia dawa au ukaitumia mara kwa mara bila kufuata ratiba, virusi vinaweza kubadilika na kuwa sugu kwa dawa hiyo," alisema. Katika utafiti huo, watafiti walifanya kazi na washiriki waliokuwa hawatumii dawa ipasavyo ili kuwasaidia kuendelea na matibabu. Takriban asilimia 70 walifikia kiwango cha kudhibiti virusi, huku asilimia 30 wakishindwa. Watafiti walilenga kundi hilo kubaini iwapo kiwango kikubwa cha virusi kilisababishwa na kuzoea dawa. Waligundua kuwa watatu kati ya kila washiriki 10 katika kundi hilo virusi vilikuwa sugu kwa DTG. Dkt Ombajo alisema hali hiyo ni ya kutia wasiwasi kwa sababu dawa hiyo inaweza kushindwa kufanya kazi hata mgonjwa akiendelea kuitumia. Tatizo jingine ni gharama kubwa ya vipimo vya kubaini hali ya dawa kwa virusi, huku nchi nyingi zikikosa rasilimali za kutosha kufanya vipimo hivyo mara kwa mara. Utafiti pia ulibaini baadhi ya wanawake wajawazito na wanaonyonyesha wanakumbwa na hali hiyo. Alisema hali hiyo inaweza kuongeza hatari ya mama mwenye kiwango kikubwa cha virusi kumwambukiza mtoto au mwenzi wake wa ngono.
read moreRight Column Content