taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 19 Jul 2026 00:55:29
Ol Kalou: Gachagua sasa apaa huku Uhuru, Kindiki wakiyumba Mlimani
USHINDI mkubwa wa mgombea wa Democracy for Citizens Party (DCP), Sammy Kamau Ngotho, katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa Ol Kalou umeibua mjadala mpya kuhusu mwelekeo wa siasa za Mlima Kenya kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Ngotho alipata zaidi ya asilimia 85 ya kura, huku mgombea wa UDA, Samuel Muchina Nyagah, akiambulia asilimia 13 pekee. Wagombea wengine saba waligawana asilimia mbili zilizosalia. Kwa kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua, ushindi huo unampa nguvu mpya kisiasa na kumpatia mbunge wake wa kwanza katika Bunge la Kitaifa. Hata hivyo, aliyekuwa Kamishna wa Mkoa Joseph Kaguthi amesema ushindi huo unaambatana na wajibu mkubwa. "Ol Kalou ilikuwa kura ya maamuzi ya Mlima Kenya. Sasa Gachagua amepewa jukumu la kuongoza eneo hilo kuelekea 2027. Lazima awe kiongozi anayewaunganisha watu na asiwe wa kulipiza kisasi," alisema. Kaguthi alisema Gachagua anapaswa kusawazisha maslahi ya Mlima Kenya na yale ya taifa kwa ujumla. Kwa Rais William Ruto, wachambuzi wanasema matokeo hayo yanatoa onyo kuhusu kupungua kwa ushawishi wake katika ngome iliyompa ushindi mkubwa mwaka 2022. Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya alisema Rais anapaswa kujiuliza iwapo uamuzi wa kuunga mkono kuondolewa kwa Gachagua mamlakani mwaka 2024 ulikuwa sahihi. "Ikiwa Rais atakuwa mkweli, lazima anajutia uamuzi huo kwa sababu ulisababisha mgogoro wa kisiasa unaozidi kukua kila siku," alisema. Mbunge wa Manyatta Gitonga Mukunji alisema ni jambo la kutia wasiwasi kwa UDA kupata asilimia 13 pekee katika eneo lililompa Rais Ruto takriban asilimia 87 ya kura mwaka 2022. "Ukiangalia matokeo hayo, unaweza kudhani hata uungwaji mkono wa Rais katika uchaguzi wa urais unaweza kuwa chini zaidi," alisema. Kwa Naibu Rais Kithure Kindiki, wachambuzi wanasema matokeo hayo yanaonyesha bado hajakubalika kama mrithi wa Gachagua katika Mlima Kenya. Mchambuzi wa siasa Gasper Odhiambo alisema Kindiki aliahidi kumshinda Gachagua Ol Kalou lakini akashindwa vibaya. Alionya kuwa nafasi ya Kindiki kuwa mgombea mwenza wa Rais Ruto mwaka 2027 sasa inaweza kuwa hatarini. Kindiki, hata hivyo, alisema ushindi wa Kenya Kwanza katika uchaguzi mdogo wa Mbeere Kaskazini na kushindwa Ol Kalou unamaanisha ushindani uko sare. "Hii ni sare. Mechi ya mwisho ni mwaka 2027," alisema. Aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta pia amewekwa katika mizani kuhusu ushawishi wake Mlima Kenya baada ya chama chake cha Jubilee kupata kura 198 pekee. Seneta mteule Karen Nyamu alisema Uhuru anapaswa kueleza kwa nini amekuwa akiunga mkono wagombea wa nje ya Mlima Kenya badala ya kukuza viongozi wa eneo hilo.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sat, 18 Jul 2026 23:55:32
Wantam: Sifuna sasa alenga kupambana na Ruto 2027 baada ya kuvuliwa wadhifa
KAULI ya Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna, kwamba yuko tayari kuwania urais mwaka 2027 limepatia sura mpya siasa za upinzani na kuzua mjadala kuhusu mustakabali wa vuguvugu la Linda Mwananchi. Akizungumza katika mkutano wa kisiasa uliofanyika Mwatate, Kaunti ya Taita Taveta, Jumamosi, Sifuna alisema licha ya kupokonywa nyadhifa zote alizopewa ndani ya ODM, vijana wa Kenya wako tayari kumpa nafasi kubwa zaidi ya kuongoza nchi. "Wameninyang'anya kila kitu Baba alinipa. Wameniondoa kama Naibu Kiranja wa Wachache katika Seneti na pia wameniondoa kwenye wadhifa wa Katibu Mkuu wa ODM. Lakini vijana wamesema watanipa cheo cha kuitwa mtukufu," alisema, akimaanisha urais. Kauli hiyo imejiri siku chache baada ya Spika wa Seneti, Amason Kingi kutangaza mabadiliko ya uongozi wa wachache, yaliyomwondoa Sifuna kama Naibu Kiranja wa Wachache na nafasi yake kuchukuliwa na Seneta wa Migori Eddy Oketch. Sifuna alisema nyadhifa zinaweza kuondolewa lakini haziwezi kufuta uungwaji mkono anaopata kutoka kwa Wakenya. "Vyeo wanaweza kuninyang'anya, lakini hawawezi kuninyang'anya akili yangu wala uungwaji mkono wa wananchi. Uongozi unatokana na wananchi," alisema. Aidha, alisema Linda Mwananchi inalenga kurithi kura pamoja na viti vya ODM katika uchaguzi mkuu wa 2027. Kauli hiyo imezua hisia kwamba vuguvugu hilo linaanza kujigeuza kutoka kundi la kushinikiza mabadiliko hadi jukwaa la kisiasa linaloweza kusimamisha mgombea wa urais. Hata hivyo, wachambuzi wa siasa wanasema Linda Mwananchi bado inakabiliwa na changamoto nyingi kabla ya kuwa nguvu ya kitaifa. Changamoto kubwa ni kwamba haijasajiliwa kama chama cha kisiasa, hivyo haiwezi kusimamisha wagombeaji katika uchaguzi. Msajili wa Vyama vya Kisiasa aliwahi kukataa ombi la kukisajili. Wanaweza kuendelea kushinikiza kisajiliwe, kujiunga na chama kilichosajiliwa au kurejea ODM na kujaribu kukidhibiti kutoka ndani. Vuguvugu hilo pia linawakutanisha viongozi kutoka vyama tofauti kama ODM, Wiper, Jubilee pamoja na wanasiasa huru ambao wameunganishwa zaidi na upinzani wao dhidi ya serikali ya Rais William Ruto. Tofauti hiyo ya kisiasa imeonekana kuwa nguvu yake, lakini pia inaweza kuwa chanzo cha migogoro kuhusu uongozi na mgombeaji wa urais. Gavana wa Siaya James Orengo, ambaye ni mmoja wa vinara wa Linda Mwananchi, pia amedokeza kuwa vuguvugu hilo lina mgombea wake wa urais. "Nani amesema Linda Mwananchi haina mgombeaji wa urais?" aliwauliza wafuasi katika mkutano huo. Kauli hiyo imezua maswali iwapo Orengo naye ana azma ya kuwania urais au atamuunga mkono Sifuna. Awali, Orengo amekuwa akisisitiza kuwa bado yeye na wenzake ni wanachama wa ODM na wanapigania kukirejesha katika misingi yake ya awali. Msemaji wa Linda Mwananchi Caroli Omondi amesema ODM imekufa kisiasa na kuwahimiza wanachama wake kuhamia Linda Mwananchi. Pia amewataka viongozi wa upinzani akiwemo Kalonzo Musyoka, Rigathi Gachagua, Fred Matiang'i, Martha Karua, James Orengo na Edwin Sifuna kukubaliana kuhusu mgombea mmoja wa urais ili kumpa ushindani mkali Rais Ruto katika uchaguzi mkuu mwaka 2027. Kwa upande wake, Sifuna amekuwa akisisitiza kuwa ushindi dhidi ya Rais Ruto utawezekana tu ikiwa upinzani utaweka kando maslahi binafsi na kuungana. Tayari msemaji wa muungano wa upinzani Mukhisa Kituyi amesema timu ya Sifuna ni sehemu ya mazungumzo yanayoendelea ya kuunda muungano mpana wa upinzani. Hata hivyo, wachambuzi wanasema bado haijulikani iwapo Sifuna atakuwa tayari kuacha azma yake ya urais ikiwa muungano huo utakubali mgombeaji mwingine. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Multimedia Profesa Gitile Naituli anaamini Sifuna ameibuka kama mmoja wa viongozi wakuu wa kizazi kipya cha upinzani na anaweza kubadilisha mwelekeo wa siasa za mwaka 2027. Lakini wengine wanahoji iwapo eneo la Mlima Kenya litamuunga mkono mgombea ambaye hatoki eneo hilo, wakisema hilo linaweza kuwa changamoto kubwa kwa muungano wowote wa upinzani utakaoundwa kuelekea uchaguzi mkuu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sat, 18 Jul 2026 22:55:36
Maswali tele kuhusu wamiliki wa magari ya Prado yanayotumiwa na wahuni
WALITUMIA kasi, vurugu na barakoa kutekeleza operesheni yao walipovamia mji wa Ol Kalou wakati wa uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika Alhamisi. Baada ya kuchanganua video zilizothibitishwa, msururu wa matukio na taarifa kutoka vyanzo vya wazi, Taifa Jumapili ilifuatilia baadhi ya mambo ambayo wanaume hao waliovaa barakoa na kufunika nyuso walitaka kuficha walipokuwa wakirushia wakazi vitoa
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 18 Jul 2026 19:03:04
Social media influencers Andrew and Tristian Tate arrested in Miami, US Marshals Service tells AP
Influencer brothers Andrew and Tristan Tate were arrested by federal authorities Saturday in Miami, according to the U.S. Marshals Service. The charges against the pair were not immediately announced. Brady McCarron, a spokesperson for the Marshals Service, told The Associated Press that the warrant was sealed. They were arrested on an extradition request from the [...] The post Social media influencers Andrew and Tristian Tate arrested in Miami, US Marshals Service tells AP appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 18 Jul 2026 17:44:17
Meet Nguyen The Hoang: The Creator Building a Digital Community Through Authenticity
In a social media landscape dominated by trends, algorithms, and constant competition for attention, authenticity has become one of the most valuable qualities a creator can possess. For Vietnamese content creator Nguyen The Hoang, authenticity is not simply a content strategy. It is the foundation of a growing digital community built on trust, transparency, and [...] The post Meet Nguyen The Hoang: The Creator Building a Digital Community Through Authenticity appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 18 Jul 2026 17:54:07
Two US service members killed, one missing following Iranian strikes in Jordan
Two US service members were killed and one is missing in action, US Central Command announced Saturday, marking the first American military fatalities in the Iran war since March, as attacks between the two countries have escalated. "On July 17, two U.S. service members in Jordan were killed in action as U.S. Central Command (CENTCOM) [...] The post Two US service members killed, one missing following Iranian strikes in Jordan appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 18 Jul 2026 17:57:14
Venice protesters clash with police as Trump envoy's mega yacht crashes their party
Around 300 protesters clashed with riot police in Venice on Friday evening over the arrival of US ambassador to Italy Tilman Fertitta's $450 million mega yacht Boardwalk during the city's annual Redentore (Redeemer) festival, police said. Fertitta, a close ally of and donor to US President Donald Trump, has been cruising around Italy this summer [...] The post Venice protesters clash with police as Trump envoy's mega yacht crashes their party appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 18 Jul 2026 17:58:52
German politician resigns over surrogacy child controversy
German centre-right politician Jens Spahn has resigned as parliamentary group leader of the countrys governing coalition after being accused of hypocrisy over his use of a surrogate mother in the US to have a child. Surrogacy is prohibited in Germany a policy backed by his Christian Democrat party (CDU) and, several years ago, by [...] The post German politician resigns over surrogacy child controversy appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 18 Jul 2026 18:09:01
Hungary's president agrees to stand down after parliament backs removal
Hungarian President Tamás Sulyok has agreed to step down, signing an amendment to the countrys constitution which will end his presidency at midnight on Sunday. Prime Minister Péter Magyars Tisza party had used its majority to steamroll the law change through parliament to oust Sulyok widely seen as a loyalist of former prime minister [...] The post Hungarys president agrees to stand down after parliament backs removal appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content