kahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 19 Jul 2026 03:48:28
One killed, suspected bicycle thief injured in police shooting in Embu
A police operation to recover a stolen bicycle turned deadly after the officers came under attack from a group of youths in Mbeere South Sub-County, Embu County. The incident occurred on Saturday night at Mutuobare Shopping Centre, where police had tracked a suspect, who was alleged to have stolen a bicycle. According to police, a [...] The post One killed, suspected bicycle thief injured in police shooting in Embu appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 19 Jul 2026 03:19:46
Russians turn to cash, putting more strain on slowing wartime economy
Russians are returning to cash, as mobile internet shutdowns disrupt card payments, and more businesses seek to dodge tax under mounting financial pressure more than four years into the war with Ukraine. Russia has added 1.56tn roubles (£14.8bn; $20bn) in cash into circulation since the start of the year the biggest rise for the [...] The post Russians turn to cash, putting more strain on slowing wartime economy appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 19 Jul 2026 02:55:43
Aliyekuwa mfungwa Mwendwa, 35 hatimaye ajiunga na chuo kikuu
MFUNGWA wa zamani ambaye juma lililopita aliwashangaza wengi alipomtafuta hakimu aliyemhukumu kifungo cha miaka minne gerezani ili kumshukuru sasa amejiunga na chuo kikuu. Mwendwa Kilatya Nthenge,35, Ijumaa alijiunga na chuo kikuu cha Africa Nazarene kilichoko eneo la Ongata-Rongai, kaunti ya Kajiado. Jaji aliyemhukumu, Bw Eugene Pascal Nabwana ndiye aliyemsafirisha kwa gari lake la kibinafsi kutoka eneo la Syokimau, kaunti ya Machakos hadi Africa Nazarene University kujiunga rasmi na chuo hicho. Bw Nabwana pia alikuwa wa kwanza kumsaidia kwa kumlipia sehemu ya karo yake ya muhula wa kwanza chuoni anakosomea cheti cha masuala ya Biashara na Usimamizi. Akizungumza na Taifa Leo, Bw Nabwana alimtaja Bw Kilatya kuwa mtu aliyebadilika na kwamba furaha yake ni kumuona ametimiza ndoto yake ya masomo, kupata kazi nzuri na kujiendeleza maishani. "Kwanza kabisa nashukuru shirika la habari la Nation Media Group kwa kuangazia taarifa ya Kilatya. Nimeonelea vyema nimfikishe hapa angalau asajiliwe rasmi chuoni. Nimelipa sehemu ya karo ila deni bado ni kubwa. Ningeomba sana wahisani zaidi wajitokeze ili kuchangia Bw Kilatya asome chuoni bila kutatizwa," akasema Bw Nabwana. Taifa Leo pia iliona barua ya usajili ya Bw Kilatya ya chuo cha Africa Nazarene ambapo nambari yake ya usajili ni CBM2027/083. Ili kufanikisha masomo yake, nambari maalum ya kumchangishia karo ilitolewa kama Paybill Number 7291071 ilhali akaunti yake ikiwa ni CBM2027/083. Katika mahojiano na Taifa Leo, Bw Kilatya hakuficha furaha yake kujiunga na chuo cha Africa Nazarene ambacho kimekuwa ndoto yake ya muda mrefu. "Nimefurahi. Nashukuru Nation Media Group. Zaidi ninamshukuru jaji Nabwana. Amedhihirisha moyo wa upendo. Yeye ni zaidi ya mzazi wangu sasa. Mungu ambariki kwa msaada wake," akasema Bw Kilatya. Aliahidi kutia bidii masomoni. "Nitasoma kwa bidii na punde nikikamilisha na kuhitimu cheti, nitajikaza nifanye Diploma kabla ya kusomea Digrii. Wote waliochangia na watakaochangia kufaulu kwangu wabarikiwe," akasema Bw Kilatya. Naibu Chansela anayehusika na masuala ya wanafunzi na masomo katika chuo kikuu cha Africa Nazarene, Prof Simon Obwatho, alimtaja Bw Kilatya kuwa mtu aliyebadilika kikweli kutoka kwa 'mui hadi kuwa mwema." Prof Obwatho pia alimshukuru Bw Kilatya kwa kuchagua taasisi ya Africa Nazarene alikosajiliwa kuanza muhula wake wa 2026. "Tutashirikiana naye kwa karibu. Twataka awe kielelezo cha wengine ambao wanapitia changamoto kama zake kwamba bado unaweza kufungwa jela lakini ukabadilika, kuwakielelezo na kioo cha jamii," akasema Bw Obwatho. Julai 2,2026, Bw Kilatya alimtembelea Bw Nabwana ofisini mwake katika jumba la mahakama ya Wamunyu, kaunti ya Machakos wiki kmfafanulia kuwa baada ya kumfunga miaka minne gerezani kwa kosa la wizi wa mifugo, alitumia muda huo kusoma, kujisajili katika mtihani wa kidato cha nne (KCSE) alioufanya 2025. Alipata alama ya D. Punde alipokamilisha kifungo cha mwaka huu, alionelea amtafute Bw Nabwana kumshukuru na pia kumuomba kabisa msaada wa kuendeleza masomo yake. "Nilitii ushauri wako. Nikasoma kwa bidii nikiwa jela na kupata alama ya D nikiwa gerezani. Bado nina hamu kubwa ya kuendeleza masomo yangu ila sina namna.Nisaidie nipate ufadhili nisome," akasema Bw Kilatya. Hivyo Ijumaa Bw Kilatya alionekana kuwa mwingi wa furaha alipokubaliwa na kusajiliwa chuoni Africa Nazarene kuanza rasmi masomo yake ya juu.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sat, 18 Jul 2026 03:52:10
Supreme Court Rejects Bid to Eliminate Tax Exemptions for Some Foreign Companies
The waivers have faced criticism from opponents who argue that they disproportionately favour Japanese investors without reciprocating the benefits for Kenya.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sat, 18 Jul 2026 23:26:15
Civil Servants Get Pay Rise After SRC Okays New Salaries and Allowances
The revised salary structure forms part of the Fourth Remuneration Review Cycle, which aims to harmonise pay across the public service while aligning government compensation with the country's fiscal framework.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sun, 19 Jul 2026 00:58:46
Court Orders Freeze on Over Ksh 100M Held by Two Kenyans
The court directed an immediate freeze following a request by the Assets Recovery Agency, with the two now unable to withdraw or move the millions held in several bank accounts as well.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sun, 19 Jul 2026 01:18:19
NLC, KeNHA Issue Notice to Landowners Over Airport, Road Expansion
The compulsory acquisition process comes as the government advances plans to improve transport infrastructure in the area, with the expansion of the airstrip expected to enhance regional connectivity.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sun, 19 Jul 2026 01:35:23
Murkomen Faces Fresh Resignation Calls Ahead of 2027 General Elections
Murkomen has faced mounting criticism over rising insecurity linked to suspected criminal gangs and goons, as the country heads into the final year before the next General Election.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 19 Jul 2026 01:55:38
Itakuwa kibarua ODM kuwika ngome ya Mulembe baada ya kumtimua Sifuna
ODM sasa ina kibarua kudumisha umaarufu wake Magharibi mwa nchi baada ya kukamilisha mchakato wa kumwondoa Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kutoka wadhifa wake kama katibu mkuu. Bw Sifuna ambaye anaegemea mrengo wa Linda Mwananchi pia alitimuliwa kama Kiranja wa walio wachache katika Bunge la Seneti wiki. Kando na Bw Sifuna, Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi pia mnamo Mei alifurushwa kama naibu kiongozi wa ODM. Wawili hao walikuwa viongozi wakuu ODM Magharibi hasa baada ya aliyekuwa Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya kujiunga na Baraza la Mawaziri mnamo Julai 2024. Wakati wa uhai wa Kinara wa Raila Odinga, Magharibi ilikuwa ngome yake ya kisiasa huku ODM ikitwaa viti vingi eneo hilo. Chama hicho kilitamba katika siasa za Busia, Vihiga na Kakamega ambako ilitwaa viti vingi huku ikilemewa tu Bungoma na Ford Kenya. Kwenye kura za urais, Bw Odinga alikuwa akitamba na mnamo 2022 alimbwaga Rais Ruto katika kaunti za Trans Nzoia, Vihiga, Kakamega, Busia akilemewa tu katika Kaunti ya Bungoma. Katika uchaguzi mkuu uliopita ODM ilitwaa viti 10 vya ubunge kati ya 12 Kakamega pamoja na ugavana na mwakilishi wa kike. Kaunti jirani ya Vihiga ODM ilitwaa ugavana na useneta huku kule Busia ikiwahi viti vinne kati ya saba vya ubunge. Pia ODM ilitwaa ugavana na mwakilishi wa kike. ODM ilipata kiti cha ubunge wa Saboti katika Kaunti ya Trans Nzoia. Kushinda viti vingi na kura za urais kulisababisha Raila na ODM itambe kisiasa magharibi mwa nchi. Hata hivyo, baada ya kuondolewa kwa Bw Sifuna na Bw Osotsi katika nyadhifa zao, ODM inaonekana kukosa mnato Magharibi jinsi ilivyokuwa hapo awali. Mnamo Alhamisi Bw Sifuna alidai kuwa ODM imekufa huku pamoja na Gavana wa Siaya James Orengo wakizindua misururu ya mikutano ya kisiasa kote nchini kupitia vuguvugu lao la Linda Mwananchi. "Kwa masikitiko makuu ODM kwa sasa wapo mahali ambapo maamuzi yanayoathiri chama na wanachama wake hayatoki tena Orange House. Maamuzi hayo na yale yaliyosababisha niondolewe kama kiranja wa wa wengi kwenye Bunge la Seneti yalifanyika katika ikulu ya Nairobi," akasema. Pia alifichua kuwa viongozi ambao kwa miaka mingi wamemuunga mkono Kinara wa ODM Raila Odinga wameamua kufanya kazi chini ya vuguvugu la Linda Mwananchi. "Tulifanya kazi kwa miaka mingi kuhakikisha kuwa tunatimiza ndoto ambayo Raila alifanyia kazi. Umaarufu wa chama mashinani umefifia kwa sababu ya tamaa ya baadhi ya viongozi baada ya kifo cha Raila," akaongeza. Kauli ya Bw Sifuna inaashiria kuwa chama cha ODM imekufa huku akitarajiwa kujiunga na chama kipya cha kisiasa. Kuhusu Magharibi, Bw Sifuna anatarajiwa kutawazwa kama msemaji eneo hilo mnamo Julai 26 katika mkutano utakaofanyika uwanja wa Posta Kaunti ya Bungoma. Mkutano huo umechemsha siasa za Bungoma ikizingatiwa kulikuwa na minong'ono kuwa Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa pia alikuwa amepanga mkutano eneo la Musikoma, kilomita chache kutoka eneo hilo. Bw Sifuna na Bw Barasa huwa hawaonani uso kwa macho na wamekuwa na uhasama katika mikutano ya hadhara na hafla za mazishi. Bw Barasa ametangaza kuwa sasa mkutano wake hautafanyika. Kabla ya kutawazwa kama msemaji wa jamii ya Mulembe Julai 26, Bw Sifuna atakuwa kaunti jirani ya Trans Nzoia pamoja na viongozi wa Linda Mwananchi ambao wanaunga azma yake ya kuwahi uongozi wa nchi. Siasa za Bw Sifuna zimeonekana kufunika ODM Magharibi bila Raila baadhi ya viongozi wa chama hicho wakizomewa kwenye mikutano na matanga kila mara wanapomkosoa seneta huyo wa Nairobi. Mwenyekiti wa ODM Kaunti ya Kakamega ambaye pia ni Gavana wa gatuzi hilo Fernandes Baraza anasisitiza kuwa chama ni imara na umaarufu wake bado upo. "Tumekuwa tukifanya mikutano na tunapokolewa vizuri na wanaosema ODM imepoteza umaarufu watashanga chama kikitwaa viti vingi eneo hili. Mtu mmoja akiasi chama hakumaanisha kuwa wengine pia wameenda," akasema Bw Barasa ambaye anaegemea mrengo unaoongozwa na Seneta wa Siaya Dkt Oburu Oginga. Kwa mujibu wa Mchanganuzi wa Masuala ya Kisiasa Lumala Masibo, umaarufu wa Bw Sifuna na kutokwepo kwa Raila kunaiacha ODM na kibarua kigumu cha kudumisha umaarufu wake Magharibi. "Masaibu ya Sifuna na Osotsi yamesawiri viongozi wa sasa wa ODM kama wasiojali uungwaji mkono ambao walikuwa wakiupata Magharibi mwa nchi miaka ya nyuma. Pia wengi wanahisi huu ni wakati wa Nyanza kurejesha mkono kwa kumuunga mkono Bw Sifuna," akasema msomi huyo. Utafiti wa Infotrak uliofanywa wiki hii hata hivyo, ulionyesha ODM kama chama ambacho bado ni maarufu Magharibi kwa asilimia 32.
read moreRight Column Content