taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Fri, 16 Oct 2026 09:55:29
IEBC yaruhusiwa kuendelea na zabuni ya teknolojia ya uchaguzi
TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imepewa ruhusa ya kuendelea na zabuni ya teknolojia ya uchaguzi ya Sh6.5 bilioni baada ya bodi ya ukaguzi wa ununuzi wa umma kutupilia mbali malalamishi ya kampuni iliyoshindwa. Bodi ya Ukaguzi wa Ununuzi wa Umma (PPARB) pia imeamuru kampuni ya Leading Edge Limited kulipa washtakiwa Sh2 milioni kama gharama za kesi. Zabuni hiyo inahusu mfumo jumuishi wa kusimamia uchaguzi, vifaa vyake, usaidizi wa kiufundi na ukarabati, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2027. Leading Edge ilipinga masharti ya zabuni, muda wa kuwasilisha maombi na vigezo vya kifedha, ikisema vilikuwa vikali na vingeweza kunyima nafasi kampuni zenye uzoefu unaofaa. Kampuni hiyo pia ilitaka IEBC kuongeza muda wa zabuni na kutambua uzoefu wa kampuni zilizotekeleza mifumo mikubwa ya kidijitali, ikiwemo hifadhidata za vitambulisho, pasipoti na usajili wa raia. Hata hivyo, IEBC ilisema uzoefu wa mifumo mingine ya kidijitali hauonyeshi moja kwa moja uwezo wa kusimamia teknolojia ya uchaguzi. Pia ilitetea hitaji la kuwa na msambazaji mmoja ili kuweka wazi uwajibikaji wa kimkataba. Bodi ilisema Leading Edge haikutoa ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa mabadiliko yaliyofanywa kwenye stakabadhi za zabuni yaliathiri haki yake kwa kiwango kinachostahili zabuni kusimamishwa. Hata hivyo, ilikosoa IEBC kwa kutotumia lugha iliyo wazi kuhusu upendeleo wa kampuni za humu nchini. Mgogoro huo ulifuatia malalamishi ya awali ya Galadirel Investments Limited, yaliyosababisha IEBC kurekebisha zabuni baada ya bodi kubaini kasoro katika vipimo vya kiufundi na vigezo vya tathmini. Bodi sasa imeagiza afisa msimamizi wa IEBC kuendelea na zabuni hiyo hadi mwisho kwa mujibu wa sheria.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Fri, 16 Oct 2026 10:55:20
Kazi aliyobakisha Raila kabla ya kifo chake
USHIRIKIANO wa kisiasa alioanzisha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga na Rais William Ruto kabla ya kifo chake Oktoba 15 2025, sasa unaingia katika hatua muhimu huku vyama vya UDA na ODM vikijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa Agosti 10, 2027. Kazi kubwa iliyobaki ni kutimiza ahadi za makubaliano yao, kuafikiana kuhusu ugavi wa mamlaka na kuunda muungano utakaoweza kustahimili ushindani wa kisiasa kuelekea uchaguzi ujao. Vyama hivyo vimeunda timu ya wataalamu 10, watano kutoka kila upande, kuandaa manifesto ya pamoja itakayounganisha sera zao na kutathmini utekelezaji wa ahadi zilizotolewa mwaka 2022. Timu hiyo inajumuisha wawakilishi wa UDA na ODM, huku wakurugenzi wakuu wa vyama hivyo, Nicodemus Bore na Oduor Ong'wen, wakishiriki kwa mujibu wa nyadhifa zao. Bw Bore alisema lengo ni kuhakikisha ahadi za awali zinatimizwa na mahitaji ya maeneo yote nchini yanazingatiwa. "Tunataka kuhakikisha kwamba ahadi tulizotoa mwaka 2022 zinatekelezwa kikamilifu," alisema. Hata hivyo, kuandaa manifesto ya pamoja ni sehemu moja tu ya kazi aliyobakisha Raila. Changamoto kubwa ni iwapo vyama hivyo vitaafikiana kuhusu jinsi vitakavyoshiriki uchaguzi na kugawana nafasi za uongozi katika serikali ijayo. Ushirikiano huo ulianza kuimarika baada ya maandamano ya vijana wa Gen Z mwaka 2024, yaliyotoa presha kwa serikali ya Rais Ruto. Rais aliwateua viongozi kadhaa wa ODM katika Baraza la Mawaziri mnamo Julai mwaka huo, kabla ya kutia saini makubaliano na Raila katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyatta (KICC) Machi 7, 2025. Makubaliano hayo yalijumuisha ajenda ya vipengele 10, ikiwemo utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati ya Mdahalo wa Kitaifa (NADCO), kuimarisha ugatuzi, kuwawezesha vijana, kupambana na ufisadi, kupunguza matumizi mabaya ya fedha za umma na kulinda utawala wa sheria. Baada ya kifo cha Raila, kiongozi wa ODM Oburu Oginga amesisitiza kuwa serikali inapaswa kutekeleza ahadi hizo ili kuonyesha kuwa ushirikiano huo una manufaa kwa Wakenya. Bw Oginga amesema mazungumzo kuhusu uchaguzi wa 2027 yanapaswa kuzingatia ugavi wa mamlaka kwa uwiano wa asilimia 50 kwa 50. Mnamo Julai, alitangaza kuwa ODM haitawasilisha mgombea wake wa urais, bali itaunga mkono kuchaguliwa tena kwa Rais Ruto. Viongozi wa ODM sasa wanataka chama hicho kiteue mgombea mwenza wa Rais, nafasi inayoshikiliwa na Naibu Rais Kithure Kindiki. Pendekezo hilo limezua wasiwasi miongoni mwa washirika wa Rais wanaotaka Profesa Kindiki aendelee na wadhifa huo. Pia kuna kazi ya kukamilisha mageuzi ya uchaguzi yaliyotokana na mapendekezo ya NADCO. IEBC imeonya kuwa kucheleweshwa kwa sheria muhimu kunaweza kuathiri maandalizi ya uchaguzi, ikiwemo mipango ya kiutendaji na ununuzi wa vifaa. Miswada inayosubiriwa inahusu sheria za uchaguzi, makosa ya uchaguzi na vyama vya kisiasa, pamoja na mapendekezo kuhusu usajili wa wapigakura, teknolojia ya uchaguzi na ufadhili wa kampeni. Hata hivyo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa ODM Edwin Sifuna anapinga dhana kwamba chama hicho kimeachana na azma ya kuwania urais. Anasema ushirikiano huo ulilenga kudumisha utulivu wa kidemokrasia na kuwapa Wakenya nafasi ya kumuondoa Rais Ruto madarakani kupitia kura. Anarejelea matamshi ya Raila wiki chache kabla ya kifo chake, alipouliza kwa nini watu walidhani ODM haitakuwa na mgombea urais mwaka 2027. Hivyo basi, kazi aliyobakisha Raila si kuunganisha vyama viwili pekee, bali pia kuhakikisha ahadi za mageuzi zinatekelezwa na kwamba tofauti kuhusu mamlaka hazivunji ushirikiano huo kabla ya uchaguzi wa 2027.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Fri, 16 Oct 2026 10:48:15
IG has power to hire police officers, Appeals Court deals blow to NPSC
The bench headed by Justice Kiage was of the view that it would be ironic for the IG to command and be held accountable for persons he does not have a say in hiring.
read morekenyanews.go.ke
@kna Fri, 16 Oct 2026 06:36:03
21,000 junior schools targeted for nationwide digital learning drive
The government is expanding access to digital learning in public junior schools nationwide, with 10,382 institutions already equipped with interactive smart boards and teacher laptops in a major push to modernise classroom instruction, bridge the digital divide and prepare learners for an increasingly technology-driven economy. Information Communication Technology Authority (ICTA) Board Chairperson Lily Ngok presided...
read morekenyanews.go.ke
@kna Fri, 16 Oct 2026 06:49:31
Bank reviews urban infrastructure projects in Kiambu
Kiambu Governor Kimani Wamatangi has held talks with a World Bank delegation to review progress in the implementation of urban infrastructure projects, aimed at improving living conditions in informal settlements and upgrading towns and shopping centres across the county. The meeting focused on ongoing and completed projects under the Kenya Informal Settlements Improvement Program Phase...
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 16 Oct 2026 06:55:31
Epileptic man found dead in Bungoma stream
A 44-year-old man was found dead in Kisiwa Stream in Bungoma Central Sub-County after he reportedly left home to take a bath. The deceased, identified as Titus Muhadia Shioso, was discovered floating in the stream at Namosi Village, Kisiwa Sub-location, on Thursday evening, October 15, 2026. According to police, the man's brother told police that [...] The post Epileptic man found dead in Bungoma stream appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Fri, 16 Oct 2026 06:55:46
Wanasiasa wa upinzani na serikali washindana hafla ya Raila
HAFLA ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha aliyekuwa kiongozi wa ODM Raila Odinga iligeuka uwanja wa ushindani wa kisiasa kati ya viongozi wa upinzani na wale wanaounga mkono serikali jumuishi ya Rais William Ruto. Sherehe hizo zilifichua tofauti kuhusu urithi wa kisiasa wa Raila na mwelekeo ambao ODM inapaswa kuchukua kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Viongozi wanaounga mkono serikali walisisitiza kuwa ushirikiano na Rais Ruto ndio njia bora ya kuendeleza miradi ya maendeleo Nyanza, huku wapinzani wakitaka kuungana ili kumwondoa madarakani mwaka ujao. Waziri wa kawi Opiyo Wandayi alisema serikali ya Rais Ruto imeleta maendeleo katika eneo hilo na kutabiri kuwa upinzani utapata wakati mgumu kumshinda rais. Naibu kiongozi wa ODM Simba Arati aliwaonya wanaofikiria kuondoka chama hicho kuwa wako huru kufanya hivyo, akisisitiza kuwa ODM bado ina nguvu katika eneo la Nyanza. Hata hivyo, Gavana wa Siaya James Orengo, Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka walisisitiza kuwa kumuenzi Raila kunamaanisha kuendeleza mapambano ya kisiasa dhidi ya serikali. Orengo alisema upinzani utaungana nyuma ya mgombea mmoja ili kumwondoa Rais Ruto madarakani, akitaja ukosefu wa ajira kama mojawapo ya changamoto zinazowakabili Wakenya. Mvutano huo ulijitokeza pia miongoni mwa wafuasi waliokutana Migwena, ambapo vijana waliokuwa wameegemea mirengo tofauti walizozana na kuvuruga baadhi ya shughuli. Kumbukumbu ya Raila iligeuka kuwa jukwaa la ushindani wa kisiasa, huku pande hizo zikijaribu kuonyesha ni nani anayefaa kuendeleza urithi wake kuelekea uchaguzi wa 2027.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 16 Oct 2026 05:54:05
Lovince Mckenzie taps Joshua Baraka, Ayo Maff for new single 'Locked In'
Kenyan-American musician Lovince Mckenzie is expanding his international music ambitions with the release of "Locked In," a collaboration featuring Ugandan singer Joshua Baraka and Nigerian artist Ayo Maff ahead of his forthcoming EP, Dance and Soul. The new single brings together artists from different corners of Africa's contemporary music scene, underscoring Mckenzie's ambition to build [...] The post Lovince Mckenzie taps Joshua Baraka, Ayo Maff for new single 'Locked In' appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 16 Oct 2026 06:11:39
House Committee Urges Prisons Service to Address Ethnic Imbalance in Recruitment
A National Assembly committee has urged the Kenya Prisons Service (KPS) to use its nationwide presence to comply with legal requirements on ethnic diversity and provide equal employment opportunities to disadvantaged groups. The National Assembly Committee on Cohesion and Equal Opportunities raised the concerns during a meeting with Prisons Service Commissioner General Patrick Aranduh, noting [...] The post House Committee Urges Prisons Service to Address Ethnic Imbalance in Recruitment appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Fri, 16 Oct 2026 05:55:38
Oburu amkumbuka Raila katika siku ya kuzaliwa kwake
KIONGOZI wa ODM Oburu Oginga jana alimkumbuka kakake mdogo Raila Odinga akisema uhusiano wao wa kindugu hauwezi kuvunjwa na kifo. Katika ujumbe katika maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kifo cha Raila Oburu alisema kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa katika tarehe ambayo Raila aliaga dunia kulimkumbusha uhusiano wa kipekee waliokuwa nao. Oburu alikosa hafla ya kumbukumbu iliyofanyika Migwena, Bondo, kaunti ya Siaya, kwa sababu ya maagizo ya madaktari ya kupumzika. "Kuadhimisha mwaka mwingine wa kuzaliwa kwangu siku hii kunanifanya kutafakari kwa furaha na huzuni, nikikumbuka kuwa pia ndiyo siku kaka yangu mdogo mpendwa, Baba Raila Amolo Odinga, aliondoka kwenda kuwa na Bwana," alisema. Aliongeza kuwa kuzaliwa kwake na kifo cha Raila kutokea siku moja ni ishara ya uhusiano wa kipekee kati yao. "Kutengana kimwili hakuwezi kuvunja undugu ulioandikwa mbinguni," alisema, huku akimtakia Raila pumziko la amani. Picha za Oburu akikata keki ya siku yake ya kuzaliwa akiwa amezungukwa na familia na marafiki pia zilisambazwa. Seneta huyo wa Siaya aliwashukuru wake zake, Dkt Ann Oburu na Mama Judith Oburu, wafanyakazi wa Nairobi Hospital, wanachama wa ODM, wafanyakazi wake wa nyumbani na timu ya Pawaa Centre kwa kumwandalia sherehe ya kushtukiza. Pia aliwashukuru wanachama wa chama na wafuasi waliomtembelea na kumfariji katika siku hiyo yenye maana mbili kwake. Kutokuwepo kwake katika kumbukumbu ya Raila kulizua maswali miongoni mwa waliohudhuria, lakini mjane wa Raila, Mama Ida Odinga, aliwahakikishia wananchi kuwa Oburu alikuwa akiendelea vizuri na alikuwa ameshauriwa kupumzika. "Oburu yuko sawa. Madaktari wamemwambia apumzike na ajiepushe na mkutano wenye vurugu kama huu," alisema Ida. Katika hotuba iliyosomwa na Gavana wa Kisii Simba Arati, Oburu alisema alikuwa akifuata maagizo ya madaktari ya kupumzika kitandani na kuepuka shughuli za umma kwa muda ili apone kikamilifu. Hata hivyo, alisisitiza kuwa mawazo na moyo wake zilikuwa pamoja na wanachama wa ODM waliokusanyika Migwena. Alimshukuru mdhamini wa ODM, Mzee Joshua Kawino, kwa kumwakilisha katika hafla hiyo na kuwasilisha salamu zake kwa familia na wafuasi wa chama. Oburu alisema upendo na usaidizi aliopokea ulimfariji katika siku hiyo iliyokuwa na umuhimu mkubwa kwake na kwa familia yake. Raila aliaga dunia Oktoba 15, 2025, na kifo chake kikafunga ukurasa muhimu katika siasa za Kenya, ambako alijulikana kwa mchango wake katika mapambano ya demokrasia na mageuzi ya kisiasa.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 16 Oct 2026 05:13:55
How to Become a Lecturer in Kenya
Becoming a lecturer in Kenya is a career path for people who enjoy teaching, research, and sharing knowledge with others. If you want to know how to become a lecturer in Kenya, you need to understand the academic qualifications, professional skills, and experience required by universities or colleges. The process depends on the institution and [...] The post How to Become a Lecturer in Kenya appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 16 Oct 2026 05:17:35
How to Become Rich at a Young Age
Learning how to become rich at a young age starts with developing good financial habits, building valuable skills, and making smart decisions with money. Although becoming wealthy takes time and effort, starting early gives you more opportunities to save, invest, and grow your income. Whether you are a student, a young professional, or an aspiring [...] The post How to Become Rich at a Young Age appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 16 Oct 2026 05:18:50
Body of man found in drainage channel in Kirinyaga
Police in Kirinyaga County have launched investigations after the body of a 32-year-old man was found in a feeder drainage channel in Muthaiga B, Mwea West Sub-County. The body was discovered on Thursday, October 15, 2026, at the Muthaiga B feeder drainage, prompting officers from Thiba Police Station and detectives from the Directorate of Criminal [...] The post Body of man found in drainage channel in Kirinyaga appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 16 Oct 2026 05:21:23
Nairobi woman found dead after sleeping for nearly a day
A 49-year-old woman was found dead in her bedroom in Kibra, Nairobi, after reportedly returning home heavily intoxicated and going to sleep. The deceased, identified as Kasty Becky Chizi Nduku, was discovered unresponsive at around 12:30pm on October 15, 2026, after her family noticed she had not woken up since the previous morning. According to [...] The post Nairobi woman found dead after sleeping for nearly a day appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 16 Oct 2026 05:23:14
How to Become a Pilot in Kenya
Becoming a pilot in Kenya is an exciting career path for people interested in aviation, travelling, and operating aircraft. If you want to know how to become a pilot in Kenya, you need to understand the required qualifications, medical examinations, flight training, and licensing process. Whether your goal is to fly privately, work for a [...] The post How to Become a Pilot in Kenya appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 16 Oct 2026 05:27:54
How to Become a YouTuber as a Kid
Becoming a YouTuber as a kid can be an exciting way to share your talents, creativity, and interests with the world. Whether you enjoy gaming, drawing, cooking, storytelling, dancing, or educational activities, YouTube gives you a platform to create videos and connect with viewers. Learning how to become a YouTuber as a kid starts with [...] The post How to Become a YouTuber as a Kid appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content