T

taifaleo.nation.co.ke

@taifaleo Tue, 14 Jul 2026 02:55:56

Weta ahatarisha adhabu ya korti kwa madai ya kuendelea kupiga siasa za uchaguzi

SPIKA wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang'ula anakabiliwa na kesi ya kudharau mahakama baada ya Shirika la Vocal Africa kumshutumu kwa kukaidi amri zinazomzuia kutumia mamlaka ya afisi yake kumfanyia Rais William Ruto kampeni. Kesi hiyo inategemea zaidi machapisho ya Bw Wetang'ula katika mitandao ya kijamii, picha na matamshi yake ya hadharani yaliyotolewa baada ya Mahakama Kuu kutoa amri za muda. Kwa mujibu wa Vocal Africa, machapisho hayo yanathibitisha kuwa Spika huyo aliendelea kushiriki katika shughuli za kisiasa licha ya marufuku iliyowekwa na mahakama. Jaji David Mburu Jumatatu asema kuwa ombi hilo ni la dharura huku akiratibisha kesi hiyo isikizwe mnamo Julai 16 kwa mwelekeo zaidi. Ombi hilo linafuatia amri za muda zilizotolewa Julai 8 zilizomzuia Bw Wetang'ula na Spika wa Seneti Amason Kingi kutumia mamlaka, hadhi, ushawishi na heshima ya afisi zao za kikatiba kuandaa, kuhamasisha, kuidhinisha au kuongoza kampeni za kisiasa hadi kesi ya msingi itakapoamuliwa. Sasa Vocal Africa inadai kuwa Bw Wetang'ula alipuuza kwa kimakusudi amri hizo. Kwa mujibu wa hati zilizowasilishwa mahakamani, kati ya Julai 10 na Julai 12, Bw Wetang'ula alihutubia mikutano ya hadhara katika Narok Kaskazini, Sirisia, Matungu, Kabuchai na Webuye Mashariki, ambako inadaiwa aliwahimiza wananchi kumuunga mkono Rais Ruto katika uchaguzi wa 2027 huku akielezea mafanikio ya serikali ya Kenya Kwanza.Shirika hilo pia linadai kuwa baadaye Spika huyo alichapisha taarifa kuhusu mikutano hiyo kupitia akaunti yake rasmi ya mtandao wa X (zamani Twitter), jambo ambalo, kwa mujibu wake, linaonyesha wazi kuwa aliendelea na shughuli zilizokatazwa na mahakama.

read more

Other Headlines


T

taifaleo.nation.co.ke

@taifaleo 8 hours ago

Idara ya Usalama, Bodi ya Utalii wazindua ligi ya 'Panga Boys' Lamu

IDARA ya Usalama kupitia Kitengo cha Polisi wa Watalii (TPU) kwa ushirikiano na Bodi ya Utalii Lamu (LTA), Shirikisho la Kandanda Nchini (FKF), tawi la Lamu, na serikali ya kaunti wamezindua ligi maalum inayolenga kukabiliana na uhalifu wa mapanga na dawa za kulevya miongoni mwa vijana eneo hilo. Ligi hiyo ya mpira wa miguu iliyozinduliwa Jumatatu inajumuisha vijana wasiozidi umri wa miaka 18. Jumla ya timu kumi na sita (16) zimeshirikishwa kwenye ngarambe hiyo ya wiki tatu mfululizo. Vilabu hivyo ni Nyundo FC, Crocodile FC, AC Milan, Swafaa FC, Dragon Fly FC, Al Aman, Kashmir City, Real Madrid FC, Rising Stars, Gen 2, Mararani FC, Lamu Boys FC, Home Boys FC, Al Azhar, Riyadha FC na Ukhtein FC. Timu zote ni za kisiwa cha Lamu. Akizungumza kwenye hafla ya kuzindua kiny'anganyiro hicho kwenye uwanja wa Twaif kisiwani Lamu Jumatatu, katibu wa kamati andalizi, ambaye pia ni Mwakilishi wa Vijana katika FKF, Lamu, Bw Athman Farid, maarufu Pirezi, aliwataka vijana kupendana na kuepuka kujiingiza kwenye magenge ya uhalifu na mihadarati. "Ligi yenyewe imeanzishwa madhumuni yakiwa ni kumaliza uhalifu wa mapanga na kuweka amani. Na ndiyo sababu tukaipa jina 'Weka Panga Chini, Chukua Mpira-Jenga Amani na Mustakabali wa Vijana'. Tupendane na kudumisha amani tunapocheza," akasema Bw Farid. Kauli yake iliungwa mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Lamu (LTA) Fridah Njeri, aliyesisitiza kuwa ili Lamu kuvutia wageni zaidi wa kitaifa na kimataifa, lazima amani na utulivu vidumishwe. "Lamu ni kivutio cha watalii na wageni hawawezi kuvutiwa kuja hapa iwapo usalama unadorora. Tutumie ligi hii kuhubiri amani ili Lamu yetu iwe eneo zuri la wageni kuja na uchumi wetu kuimarika," akasema Bi Njeri. Mkurugenzi wa Idara ya Michezo na Vijana wa Kaunti ya Lamu Peter Ndichu, alisema mbali na kukabiliana na mihadarati na 'Panga Boys,' kinyang'anyiro kilichozinduliwa pia kinalenga kutambua vipaji vya kandanda miongoni mwa vijana wanaoshiriki ili kuwatafutia nafasi ya kucheza nje ya Lamu.

read more
T

taifaleo.nation.co.ke

@taifaleo 11 hours ago

Korti yaagiza EABL kuweka kando Sh10m kabla kusikiza kesi ya zogo na mwanahabari Willis Raburu

MAHAKAMA ya Biashara iliyoko Milimani, Nairobi, imeamuru kampuni ya East African Breweries PLC (EABL) iweke Sh10 milioni katika akaunti ya pamoja inayosimamiwa na mawakili wa pande zote kusubiri kusikizwa kwa kesi ya kibiashara iliyowasilishwa na mwanahabari na mshawishi wa mitandao ya kijamii Willis Raburu. Hakimu Mkuu Mwandamizi A. Nyoike alitoa agizo hilo huku akitupilia mbali ombi la Raburu la kusimamisha au kufuta leseni ya EABL kutokana na madai ya kutolipwa ada za mkataba. Mahakama ilisema kuwa ombi hilo lilikuwa sawa na kuomba amri ya lazima, ambayo Raburu hakufikia kiwango cha kisheria kinachohitajika ili kutolewa. Kupitia kampuni yake ya Steizon Limited, Raburu alishtaki Game Changer Marketing Limited pamoja na EABL akidai aliajiriwa kutoa huduma za ushawishi wa kidijitali, kuvumisha chapa, kuratibu hafla na matangazo ya mitandaoni katika tamasha la Furaha City Festival lililofanyika Desemba 2024. Alidai kuwa pande hizo zilikubaliana malipo Sh10 milioni, lakini hadi sasa hajalipwa. Raburu alisema alitekeleza kikamilifu wajibu wake, ikiwa ni pamoja na kutengeneza zaidi ya video 60 fupi za mitandaoni, machapisho zaidi ya 100, kuratibu washawishi wa mitandao ya kijamii na kusimamia shughuli za hafla hiyo. Aliongeza kuwa aliwasilisha ripoti baada ya tamasha na mara kadhaa kudai malipo, lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda. Kwa upande wake, Game Changer Marketing ilikana kumwajiri Raburu kwa shughuli za Furaha City Festival. Kampuni hiyo ilisema ushirikiano wake na Raburu ulihusu tu kampeni ya awali ya Chrome Wabebe Campus Caravan, ambayo ilisema tayari alilipwa baada ya EABL kuidhinisha gharama na kutoa agizo rasmi la ununuzi. Nayo EABL ilikana kuwajibika ikisema tamasha la Furaha City lilikuwa sehemu ya mwisho ya kampeni ya Wabebe na si mradi mpya uliostahili malipo mengine. Aidha, ilisema hakukuwa na agizo jipya la ununuzi wala mkataba uliotiwa saini unaounga mkono madai ya Raburu ya Sh10 milioni. Katika uamuzi wake, Hakimu Nyoike alisema Raburu ameibua masuala yanayostahili kusikilizwa wakati wa kesi kamili. Hata hivyo, alisema ushahidi uliowasilishwa na pande zote mbili unakinzana na hawezi kutolewa uamuzi wa mwisho kupitia ombi la awali. "Ushahidi unaokinzana lazima uchunguzwe wakati wa kusikiliza kesi," alisema hakimu. Aliongeza kuwa Raburu hakuthibitisha kuwepo kwa "haki iliyo wazi na isiyoweza kutiliwa shaka" inayohitajika ili apewe amri ya lazima aliyoomba. Mahakama pia ilikataa hoja ya EABL kwamba kesi hiyo ilizimwa kwa kuwa kulikuwa na kesi nyingine inayohusu suala hilo katika Mahakama Kuu. Hakimu alisema kampuni hiyo haikuthibitisha kuwa kesi hiyo ilikuwa bado inaendelea baada ya Raburu kuonyesha kwamba ilikuwa imeondolewa. Hata hivyo, licha ya kukataa kuamuru EABL imlipe Raburu mara moja Sh10 milioni zinazodaiwa, mahakama iliagiza kampuni hiyo kuweka kiasi hicho katika akaunti ya pamoja inayosimamiwa na mawakili wa pande zote kama dhamana hadi kesi hiyo itakapoamuliwa.

read more
T

taifaleo.nation.co.ke

@taifaleo 13 hours ago

Wadau wa utalii wahofia bima ya afya ya Sh6.5 milioni kwa kila mtalii itaua biashara

SERIKALI sasa inakabiliwa na kesi mahakamani kupinga agizo jipya linalowataka wageni wote wanaoingia Kenya kuwa na bima ya afya ya usafiri. Agizo hilo limezua upinzani mkali kutoka kwa wadau wa sekta ya utalii wanaosema litaongeza gharama za kusafiri na kupunguza ushindani wa Kenya kama kivutio cha watalii. Chama cha Watumiaji Bidhaa Nchini (COFEK) limewasilisha kesi katika Mahakama Kuu likitaka utekelezaji wa agizo hilo usimamishwe, likidai serikali ililitangaza bila ushirikishaji wa umma na bila kuzingatia Katiba kuhusu uwazi na utawala bora. Agizo hilo lilichapishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali la Julai 30, 2026 na kutiwa saini na Waziri wa Afya Aden Duale. Linawataka wageni wote wanaoingia nchini kuwa na bima ya afya yenye kiwango cha chini cha fidia cha dola 50,000 (Sh6.5 milioni). Serikali inasema bima hiyo itawawezesha wageni kupata matibabu ya dharura bila kutegemea hospitali za umma. Hata hivyo, COFEK inahoji kuwa haijabainishwa jinsi kampuni za bima zitakavyoidhinishwa, jinsi ada zitakavyotozwa wala usimamizi wa fedha utakavyofanywa. Katibu Mkuu wa COFEK Stephen Mutoro alisema shirika hilo halipingi bima ya afya kwa wageni, bali linapinga namna sera hiyo ilivyoanzishwa bila kufuata taratibu za kikatiba. Wakati huo huo, wadau wa utalii wameonya kuwa agizo hilo litafanya Kenya kuwa ghali zaidi kwa watalii ikilinganishwa na mataifa jirani kama Tanzania, Rwanda na Afrika Kusini. Mkurugenzi Mkuu wa Muungano wa Wafanyakazi wa Hoteli na Wapishi (KAHC) Dkt Sam Ikwaye, alisema sekta hiyo inapinga hatua hiyo kwa sababu inawaongezea watalii gharama nyingine wakati serikali inapaswa kuhamasisha wageni wengi zaidi kutembelea nchi. Alisema serikali inapaswa kuboresha usafiri wa ndege za moja kwa moja, hasa kuelekea Pwani, badala ya kuongeza ada mpya. Mshauri wa masuala ya utalii Tony Kirimi alihoji kwa nini wageni walazimishwe kununua bima ya Kenya ilhali wengi tayari husafiri wakiwa na bima kutoka nchi zao. Wadau hao pia wanataka serikali ifafanue iwapo bima za kimataifa zitatambuliwa na ni kampuni zipi zitakazoruhusiwa kutoa huduma hiyo. Mzozo huo umeibuka wakati sekta ya utalii nchini inaonyesha dalili za kuimarika, huku Shirika la Huduma kwa Wanyamapori Kenya (KWS) likiripoti zaidi ya ziara milioni 3.5 katika hifadhi za taifa mwaka huu. Wadau sasa wanaitaka serikali kusitisha utekelezaji wa agizo hilo hadi mashauriano ya kina yafanyike.

read more
T

taifaleo.nation.co.ke

@taifaleo 15 hours ago

Magenge ya ulanguzi wa bangi yazidisha ujanja kuificha kwa ndizi, biskuti kuhepa polisi

MISAKO mikali ya Idara ya Upelelezi Nchini (DCI) dhidi ya dawa za kulevya katika kipindi cha miezi sita iliyopita imefichua mbinu mpya zinazotumiwa na walanguzi kusafirisha na kusambaza bangi nchini wakikwepa mtego wa polisi. Uchunguzi umebaini kuwa walanguzi wamebadili njia za usafirishaji, aina ya magari wanayotumia na hata mbinu za kuficha mzigo ili usigunduliwe. Baadhi yao sasa hupanda bangi katikati ya mashamba ya mahindi na mazao mengine ili kuficha mimea hiyo. Baada ya kuvunwa, huifunga kwa ustadi na wakati mwingine kuificha ndani ya bidhaa kama vile ndizi, biskuti au marobota ya nguo kabla ya kuisafirisha. Aidha, badala ya kutumia malori makubwa, sasa wanatumia magari madogo ya kibinafsi kama Toyota Probox na Toyota Wish, ambayo hayushukiwi kwa urahisi. Kutoka mpakani Sirare, bangi husafirishwa kwa pikipiki ikiwa imefichwa kama mizigo ya kawaida kabla ya kukabidhiwa kwa mawakala wanaoipakia upya kwenye magari yanayoelekea Nairobi na miji mingine. Mashambani Walanguzi pia hutumia barabara za mashambani zisizo na vizuizi vya polisi, hasa usiku, alfajiri au jioni, ili kukwepa ukaguzi. Wakati mwingine bangi husafirishwa kwa mabasi na matatu ikiwa imefichwa pamoja na mizigo halali katika hifadhi za mizigo. Katika visa vingine, maafisa wa DCI wamekuta bangi ikiwa imefichwa ndani ya magunia ya ndizi, marobota yaliyofungwa kwa karatasi maalumu na hata masanduku ya chuma. Mkurugenzi wa DCI Mohamed Amin alisema magenge ya kisasa ya dawa za kulevya sasa yanafanya kazi kama mitandao ya kimataifa inayotumia teknolojia na mbinu mpya za usafirishaji. "Ufanisi wa vita dhidi ya dawa za kulevya haupimwi kwa idadi ya waliokamatwa bali kwa ubora wa uchunguzi, kufanikiwa kwa mashtaka na kuvunjwa kabisa kwa mitandao ya uhalifu," akasema. Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen naye alisema serikali itaendelea kuimarisha operesheni za kijasusi ili kuwafuatilia walanguzi na kuvunja mitandao yao. Katika miezi ya hivi karibuni, DCI imekamata shehena kadhaa za bangi zenye thamani ya mamilioni ya pesa katika maeneo mbalimbali nchini, huku ikiwataka wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kukomesha biashara hiyo haramu inayozidi kuhatarisha jamii, hasa vijana na wanafunzi.

read more
T

taifaleo.nation.co.ke

@taifaleo 16 hours ago

Wakora sasa watawala kituo cha mabasi cha Green Park Terminus kilichogharimu Sh250 milioni

UCHUNGUZI umeibua madai kuwa Kituo cha mabasi cha Green Park jijini Nairobi, kilichojengwa kwa gharama ya Sh250 milioni ili kupunguza msongamano wa magari katikati mwa jiji, kinadhibitiwa na vijana wanaodaiwa kuwa na uhusiano na viongozi wakuu wa Serikali ya Kaunti ya Nairobi. Duru kutoka City Hall zinadai kuwa vijana hao hukusanya ada za maegesho kutoka kwa mabasi na magari huku maafisa rasmi wa kaunti wakitengwa. [caption id="attachment_190791" align="alignnone" width="2000"] Uharibifu mkubwa waonekana Green Park Terminus baada ya kutelekezwa licha ya kugharimu mamilioni ya pesa kujenga. Picha|Dennis Onsongo[/caption] Inadaiwa kuwa fedha zinazokusanywa haziingii kwenye hazina ya kaunti. Ingawa hivyo, Afisa Mkuu wa Idara ya Mapato Tiras Njoroge, alikanusha madai hayo akisema kituo hicho kinaendelea kuingiza mapato, lakini hakutoa ushahidi. Uchunguzi pia ulibaini kuwa kituo hicho kiko katika hali mbaya, huku baadhi ya huduma zikiwa hazifanyi kazi. [caption id="attachment_190792" align="alignnone" width="2000"] Kituo cha Green Park Terminus kilichojengwa kwa gharama ya Sh250 milioni. Picha|Dennis Onsongo[/caption] Aidha, kaunti imeidhinisha ujenzi wa kituo cha mafuta na inapanga kukodisha sehemu ya eneo hilo kwa kampuni ya China kujenga kituo cha kupasha moto magari ya umeme. Awali, Green Park ilikusudiwa kuwa kituo cha kushusha na kuwachukua abiria wa mabasi ya masafa marefu na matatu, lakini haijatimiza lengo hilo tangu ilipokamilika.

read more
T

taifaleo.nation.co.ke

@taifaleo Mon, 03 Aug 2026 02:55:02

Wadau wapinga hatua ya serikali ya kutaka watalii wanaoingia nchini kuwa na bima ya lazima

WADAU katika sekta ya utalii wamepinga vikali uamuzi wa serikali wa kutaka wageni wote wanaoingia nchi kuwa na bima ya lazima wakionya kuwa hatua hiyo itaathiri nchi kuvutia watalii wa kimataifa. Kulingana na tangazo lililochapishwa kwenye Gazeti Rasmi la Serikali la Julai 30, 2026 na kutiwa sahihi na Waziri wa Afya, Bw Aden Duale, wageni wote wanaoingia humu nchini watalazimika kuwa na bima ya afya yenye kiwango cha chini cha karibu Sh6.45 milioni. Bima hiyo itagharamia hadi Sh2.58 milioni za matibabu, Sh3.22 milioni za usafiri wa dharura wa mgonjwa, Sh38,700 za dawa zilizoagizwa na daktari, Sh129,000 za matibabu ya afya ya akili na Sh645,000 za kusafirisha mwili wa marehemu kurejeshwa nchini kwao. Kulingana na serikali, hatua hiyo inalenga kuhakikisha watalii wanapata huduma wanapokumbwa na dharura za kiafya. Hata hivyo, wadau wa utalii wamejitokeza na kupinga hatua hiyo wakisema itaongeza gharama za kuzuru Kenya. "Hatua hii itaongeza gharama kwa watalii. Kama sekta ya utalii tunapinga hatua hii. Huu si mwelekeo unaofaa, tunafaa kuweka mikakati ya kuvutia watalii si kuwazuia kuzuru nchi yetu," Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha wamiliki wa hoteli na wahudumu (KAHC), Dkt Sam Ikwaye, alisema. Wadau hao walisema bima hiyo ya lazima inaongezwa juu ya ada nyingine ambazo wageni tayari hulipa, ikiwemo ada ya Kibali cha Kielektroniki cha Kusafiri (ETA) na ada za kuingia katika hifadhi za taifa za wanyamapori iliyooongezwa hivi majuzi. Mtaalamu wa utalii, Bw Tony Kirimi alisema watalii wengi tayari huingia nchini wakiwa na bima kamili ya afya walizonunua nchi zao. "Hivyo basi hakuna sababu ya kuwalazimisha kununua nyingine nchini Kenya. Tulikubali ada ya ETA, ada za kuingia kwenye mbuga zilipandishwa na sasa tunaanzisha bima ya afya ya lazima ambayo ni ghali zaidi kuliko ilivyo katika baadhi ya mataifa ya Ulaya. Kulikuwa na maana gani ya kuondoa visa halafu tuanzishe gharama nyingine?" aliuliza. Aliongeza kuwa Kenya bado inapambana kuvutia watalii na kujenga jina lake kama kitovu kikuu cha utalii duniani na hivyo haipaswi kuweka sera zitakazozuia watalii kuchagua mataifa mengine. Wadau wa utalii pia wanaitaka serikali kufafanua ikiwa bima za afya ambazo watalii tayari wanazosafiri nazo kutoka mataifa yao zitatambuliwa, kiwango cha malipo kitakachotozwa na kampuni zitakazoruhusiwa kutoa huduma hiyo. Bw Mohammed Hersi ambaye ni mtaalamu wa utalii alisema sera hiyo itaongeza gharama kwa watalii. "Mtalii analipia bima akiwa kwao kabla ya kuja Kenya, halafu analazimishwa kununua nyingine hapa. Je, ingekuwaje kama kila nchi zingekuwa na sharti kama hilo? Swali si kama ni dola kumi au mia moja, ikiwa malipo hayo hayana msingi, basi ni mzigo usiofaa," alisema kwenye mjadala katika mtandao wa Facebook. Wadau hao sasa wanataka serikali kusitisha utekelezaji wa sera hiyo na kuanza kufanya mashauriano kati ya Wizara za Afya, Utalii, kampuni za bima na wadau wa sekta hiyo. Mjadala huo umeibuka wakati ambapo sekta ya utalii inaendelea kunoga. Hii ni baada ya Kenya kunakili idadi kubwa ya watalii wanaozuru mbuga za kitaifa za Wanyama porini. Kulingana na shirika la huduma ya Wanyamapori nchini (KWS), hifadhi za taifa zimepokea zaidi ya watalii milioni 3.5 huu mwaka ikilinganishwa na milioni mbili mwaka jana. Hata hivyo asilimia 60 ya wageni hao ni watalii wa humu nchini. Mkurugenzi Mkuu wa KWS, Prof Erustus Kanga, alisema mapato ya shirika hilo pia imeongezeka kutoka Sh2.9 bilioni mwaka 2022 alipochukua mamlaka hadi Sh10.5 bilioni mwaka huu kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watalii na uhamasisho. Hata hivyo, wadau wa sekta ya utalii wanaonya kuwa gharama hiyo mpya ya bima ya afya kwa wageni itaathiri utalii.

read more
T

taifaleo.nation.co.ke

@taifaleo Mon, 03 Aug 2026 07:17:53

Iran yanyonga raia wake wawili waliotoa habari za kijasusi kwa Amerika na Israel

TEHRAN, Iran: NCHI ya Iran imewanyonga raia wake wawili baada ya kupatikana na hatia ya ujasusi na kushirikiana na Israel, vyombo vya habari vya serikali viliripoti hapa Jumatatu. Haya yanafanyika huku taifa hilo likiongeza utekelezaji wa hukumu za kifo kwa makosa yanayohusishwa na usalama wa Iran. Walionyongwa ni Omid Behzad na Pouria Safvat, ambao walishtakiwa kwa kuipatia Israel taarifa za kijasusi. Wawili hao wanadaiwa walituma picha na taarifa za siri wakati wa vita vya mwaka jana na katika mzozo unaoendelea sasa kati ya Amerika-Israel na Iran. Taarifa hiyo ilichapishwa na chombo cha habari mahakamani, Mizan. Hukumu hizo zimetekelezwa wakati Iran inaendelea kukabiliwa na hali ya taharuki kutokana na mivutano ya ndani na nje ya nchi. Mapema mwaka huu, serikali ilikabili maandamano makubwa yaliyotikisa taifa hilo na kuyadhibiti kwa nguvu. Baadaye, Amerika na Israel zilianzisha mashambulizi mapya dhidi ya Iran mnamo Februari 28, na kuongeza mvutano katika eneo hilo. Duru ziliarifu kuwa wawili hao walipatia Israel taarifa za kijasusi na kuchangia majeshi yake yalenge vituo vya ukaguzi vilivyokuwa vikilindwa na kikosi cha Iran. Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch lilisema Julai 24 kwamba Iran imewaua kwa kunyongwa watu wasiopungua 50 katika kipindi cha miezi minne iliyopita. Kunyongwa huko kunatokana na madai ya makosa ya usalama wa taifa. Kundi hilo lilisema baadhi ya waliouawa walikuwa vijana wenye umri wa miaka 18 na 19, huku likikosoa ukosefu wa uwazi katika kesi hizo. Ujumbe wa kudumu wa Iran jijini Geneva haukujibu ombi la Reuters la kutoa maoni kuhusu taarifa hiyo. Hata hivyo, Tehran imekuwa ikikanusha mara kwa mara madai ya ukiukaji wa haki za wafungwa. Wakati huo huo, Rais wa Amerika Donald Trump alisema mazungumzo kati ya nchi yake na Iran yangefanyika Jumatatu. Hata hivyo, msemaji wa Wizara ya Masuala ya Nje ya Iran, Esmail Baghaei, alisema hakuna mazungumzo yanayoendelea kwa sasa kati ya mataifa hayo mawili. Vita vya siku 12 vya mwaka jana vilianza katikati ya Juni baada ya Israel kuanzisha mashambulizi ya anga yaliyokuja kuungwa mkono na Amerikan kabla ya kusitishwa baada ya maelewano. Mzozo wa sasa ulianza mwishoni mwa Februari kufuatia mashambulizi ya Amerika na Israel yaliyohusishwa na shinikizo dhidi ya mpango wa nuklia wa Iran, makombora ya masafa marefu na jinsi serikali ilivyoshughulikia maandamano ya Januari. Ingawa pande zote zilikubaliana kusitisha mapigano mnamo Juni, mvutano umeendelea, huku juhudi za mazungumzo zikishindwa kufikia makubaliano ya kudumu.

read more
T

taifaleo.nation.co.ke

@taifaleo Mon, 03 Aug 2026 07:35:55

MAONI: Ruto si mwanasiasa mliyezoea pale kijijini, Upinzani wasipotumia akili watapigwa chobo!

KATI ya sasa na mwezi Agosti mwaka ujao, Mkenya hana budi ila kutumia akili sawasawa, na vilevile kumlazimisha mwanasiasa kutumia akili, lau sivyo atemwe kama kikohozi. Umesalia takriban mwaka mmoja ndipo Uchaguzi Mkuu ufanyike, na huu ndio mwaka ambao wanasiasa huingia mashinani kuwakoroga watu akili kana kwamba wana ukiritimba wa hoja. Kwa mfano, fununu za ajabu zimeanza kusambaa kote nchini kwamba kiongozi wa chama cha Wiper (WPF) Kalonzo Musyoka, anaelekea kwenye kambi ya serikali, yaani muungano wa Kenya Kwanza (KK) unaoongozwa na Rais William Ruto. Amekanusha lakini… Sawa na nguruwe ambaye hujikaanga kwa mafuta yake, Kalonzo akithubutu kufanya hivyo atajimaliza mwenyewe kisiasa na hatawahi kupata nafuu tena wala kutamba katika uga wa siasa za nchi hii. Serikali ya KK imewaumiza Wakenya mno hivi kwamba mwanasiasa yeyote aliye katika mrengo wa upinzani akithubutu kuingia serikalini atafanya hivyo peke yake, labda na wajinga wachache wanaomzingira kwa kuwa kila soko lina mwendawazimu wake. Nimesema ni lazima tutumie akili, na tuwashinikize wanasiasa kutumia akili, kwa kuwa enzi ya siasa za tumbo ambapo mwanasiasa kigogo akihongwa na kubadili msimamo wake, na bado kuendelea kuwa maarufu, zimepitwa na wakati. Nimeandika mara si haba katika kurasa hizi kwamba, hata kigogo wa siasa za janibu za Mlima Kenya, Rigathi Gachagua, akiamua kurejea serikalini iliyomtimua kama paka shume atafanya hivyo peke yake. Mlima umeasi na kushupaa shingo; haujali wala kubali itakatika ua la. Sote, wanasiasa na wafuasi wao, tuna lazima ya kutumia akili kwa kuwa mtu tunayejaribu kuondoa mamlakani ana akili tele kichwani. Rais Ruto si mwanasiasa uliyezoea pale kijijini kwenu na ndio sababu anasema atauvuruga muungano wa upinzani na kuutawanya kwa raha zake. Hebu angalia, Ruto, mwanasiasa ambaye anapaswa kuwa akitapatapa kwa kuhofia kuzama kisiasa, ameanzisha gumzo la kusisimua na kuuudhi pia – kwamba Kalonzo anaelekea serikalini. Ruto wa sasa anapaswa kuwa na wasiwasi mwingi kwa kuwa vigogo wa upinzani kutoka kila pembe ya nchi wameungana ili kumwondoa mamlakani, akaibuka na kijana bora nchini, Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, akaapa kuwa hata useneta ukimtoka, na Ruto ang'olewe mamlakani, ni sawa tu. Naamini msomaji ungekuwa katika nafasi ya Ruto ungeanza kutetemeka, lakini mwenyewe haonekani kuogopa chochote, amejibadili ngozi kama nyoka, akajifanya maridadi wa kujadiliwa na labda kupiganiwa na wanasiasa wanaotaka kuwa wagombea wenzi wake. Mara... Ruto anaweza kumtema Naibu Rais Kithure Kindiki wakati wowote; mara... anamtaka Kalonzo; mara… anamtaka Waziri wa Mambo ya Nje Musalia Mudavadi; mara… ODM imempa Gavan awa Homabay Gladys Wanga; mara… Magharibi imempa Waziri wa Ushirika Wycliffe Oparanya; mara… kipenzi chake ni Waziri wa Madini, Uchumi wa Bluu na Masuala ya Bahari Hassan Joho. Nchi nzima, badala ya kumcheka Ruto kwa kuwa yupo katika nafasi hatari ya kupoteza urais, inazungumzia jinsi alivyo na watu wengi waliotunga foleni kujaribisha bahati ya kuwa manaibu wake. Ghafla weusi umekuwa weupe! Uvundo umekuwa manukato! Ajabu! Kwa kubuni mazingira yanayoonyesha kwamba nafasi ya naibu rais inaweza kuwa wazi wakati wowote, Ruto ametukoroga akili nusra tusahau kwamba ana madhaifu yake, wanaisasa walafi nao wakaaza kuimezea mate nafasi ile, wanaotamani kumng'oa wakasahau kufanya kampeni dhidi yake, wakaanza kujiona kama washirika wake. Kalonzo, aliyeonekana kama mpinzani wake mzito, ambaye alikuwa na nafasi ya kumshinda mwakani, ameshushwa thamani na kuwa mmoja wa hao wanaotaka kuwa watu wa mkono wa Ruto. Unahitaji akili nyingi ili kuwavuruga na kuwapanga watu hivyo. Na ndio maana nasisitiza: tusipotumia akili, Ruto atatupanga sote, kufumba na kufumbua tumpate ikulu akihudumu kwa muhula wa pili. Ikiwa humtaki Ruto, hakikisha unatumia akili zako saa zote ili asikupige chobo.Douglas Mutua ni mwanahabari Mkenya anayeishi Amerika (mutua_muema@yahoo.com)

read more
T

taifaleo.nation.co.ke

@taifaleo Mon, 03 Aug 2026 08:17:29

MAONI: Mbona Rais Ruto hutukumbusha mara kwa mara kuwa 'yeye si mwendawazimu'?

KAULI ya Rais William Ruto: I am not a mad man (Mimi si wazimu) inaibua miangwi ya tamthilia za mwandishi wa Nigeria, Ola Rotimi. Kazi hizo ni: Our Husband Has Gone Mad Again (OUP, 1977), na The Gods Are Not to Blame (OUP, 1971). Our Husband Has Gone Mad Again (Mume Wetu ni Mwendawazimu) ni kazi ya kitashtiti, inayoangazia maudhui ya ubarakala wa kisiasa, migongano kati ya ukale na usasa, na mafarakano ya ndoa na ya kijinsia. Kuhusiana na ubarakala wa kisiasa, mhusika mkuu, Major (Mstaafu) Lejoka-Bwown anaona siasa kuwa ulingo wa kujitajirisha, badala ya wenzo wa kuhudumia umma. Rotimi anawakejeli watawala wa mataifa ya Afrika baada ya uhuru wasiozingatia misingi ya demokrasia. Mbona Rais Ruto anatukumbusha mara kwa mara kuwa 'yeye si mwendawazimu'? Halikadhalika, Rais amesisitiza mara nyingi kuwa 'yeye si mlevi' wala 'mpumbavu', hasa anapotetea hatua zake za utekelezaji wa sera tata – ambazo aghalabu hupingwa na wananchi. Baadhi ya sera hizo ni pamoja na mpango wa Bima ya Matibabu (SHA), ujenzi wa nyumba za bei nafuu na mpango wa ufadhili wa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu. Tathmini inaonesha kwamba, anapolinganishwa na marais waliomtangulia – Mzee Jomo Kenyatta, Daniel arap Moi, Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta, Ruto ndiye rais wa pekee aliyetekeleza kijasiri sera zilizovuruga (disruptive policies) maisha ya Wakenya jinsi tunavyoyafahamu. Hata pale anapofahamishwa na wataalamu kuhusu athari hasi ya sera hizo, Rais Ruto hupuuzilia mbali ushauri huo – kushadidia kuwa anajua analolifanya. Je, mbona sasa amekiri, baada ya miaka mitatu – kwamba mfumo wa ufadhili wa elimu ya juu hautekelezeki kamwe? Aidha, mnamo Juni 25, 2024, kulizuka mageuzi ya vijana (Gen-Z) yaliyochochewa na Mswada wa Fedha wa Mwaka 2024, uliopendekeza nyongeza ya ushuru. Baada ya vijana wengi kuuawa, Rais Ruto aliamua kutoutia saini mswada huo. Kulikuwa na mantiki gani kuchukua hatua hiyo baada ya maafa kutokea? Je, huku uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 ukikaribia kwa kasi, kuna uwezekano kwamba rais 'atalegeza misimamo yake mikali' kuhusiana na mipango, na sera ambazo wananchi wanahisi kwamba zinawakandamiza? Kuna mafunzo yotote kutokana na mikabala ya utawala wa Rais Ruto? Ndio. Kwanza, utekelezaji wa sera za kimajaribio zinazodhulumu na kuwakandamiza wananchi ni hatari. Pili, uongozi wa nchi unapaswa kuwa wa kikoa. Rais Mwai Kibaki aliwateua wataalamu (technocrats), akawapa uhuru wa kulielekeza dau la uongozi. Kazi yake ikawa unahodha, huku wataalamu wakipiga makasia. Bitugi Matundura ni mhadhiri (mwagechure@gmail.com)

read more
T

taifaleo.nation.co.ke

@taifaleo Mon, 03 Aug 2026 10:53:55

T

taifaleo.nation.co.ke

@taifaleo 20 hours ago

Uhuru aagiza Azimio ifanyiwe mabadiliko, iwatafute Sifuna na Gachagua

MUUNGANO wa Azimio la Umoja One Kenya umeanza mchakato wa kujijenga upya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027 kwa kuvikaribisha vyama vipya na kuanzisha mazungumzo na makundi ya kisiasa yanayoongozwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna. Katika mkutano wa Baraza la Azimio ulioongozwa kwa njia ya mtandao na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, viongozi hao walikubaliana kuufanyia muungano huo mabadiliko makubwa. Muungano huo sasa utapewa jina jipya na mawanda yake kutanuliwa ili kuunganisha vyama vyote vya upinzani kabla ya kumteua mgombea mmoja wa urais atakayemenyana na Rais William Ruto. Katika mabadiliko hayo, vinara Fred Matiang'i wa Jubilee, Peter Munya wa PNU na Seneta wa zamani wa Embu Lenny Kivuti walijumuishwa katika Baraza la Muungano, asasi cha juu zaidi inayofanya maamuzi ndani ya Azimio. Aidha, vyama vya DP yake aliyekuwa Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi, PDP na UMP yake aliyekuwa Gavana wa Meru Kawira Mwangaza vilikubaliwa rasmi kujiunga na Azimio. Muungano huo pia uliikaribisha tena DAP-K inayoongozwa na Eugene Wamalwa, baada ya chama hicho kusitisha mchakato wa kujiondoa Azimio. Hata hivyo, Narc-Kenya cha Martha Karua, ambacho sasa kinajulikana kama People's Liberation Party (PLP), kilijiondoa rasmi mnamo 2024. Katibu Mkuu wa Azimio Caroli Omondi alisema viongozi wameamua kuanzisha mazungumzo rasmi na chama cha DCP cha Rigathi Gachagua, pamoja na vuguvugu la Linda Mwananchi la Seneta Edwin Sifuna, kwa lengo la kuunda muungano mkubwa zaidi wa upinzani. Alisema pia Azimio inaendelea kufanya mazungumzo na aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga, ambaye ni Kiongozi wa UGM huku Linda Mwananchi ikitarajiwa kujiunga rasmi mara kitakapokamilisha usajili wake kama chama cha kisiasa. Kwa mujibu wa Bw Omondi, Linda Mwananchi ndiyo itachukua nafasi ya ODM ndani ya Azimio, kufuatia mgawanyiko ulioikumba chama hicho. "Tumeamua kupanga upya muungano na kuanza mchakato wa kubadilisha sura na jina la Azimio ili liwe jukwaa linalowakutanisha washirika wote wa upinzani," akasema Bw Omondi. Alisisitiza kuwa jukumu la Bw Kenyatta ni kutekeleza wajibu wake kama mwenyekiti wa muungano, akikanusha madai kuwa rais huyo mstaafu ndiye anayepanga mikakati ya kisiasa ya upinzani. Miongoni mwa sababu za kubadilisha Azimio ni kuhakikisha unaendelea kuwavutia wafuasi wa aliyekuwa Waziri Mkuu marehemu Raila Odinga, huku pia ukivutia vijana wa kizazi cha Gen Z na washirika wapya wa kisiasa. Inaelezwa kuwa Bw Kenyatta anasukuma ajenda ya upinzani kuwa na mgombea mmoja wa urais ili kuepusha mgawanyiko ulioshuhudiwa mnamo 1992, ambapo wagombea wengi wa upinzani waligawana kura na kumwezesha Rais wa wakati huo Daniel arap Moi kushinda. Mchanganuzi wa masuala ya kisiasa anayeishi Amerika, Profesa David Monda, alisema mafanikio ya mpango huo yatategemea kujiandaa kwa viongozi wengine wa upinzani kufanya kazi chini ya muungano wa Azimio. Alisema kufufuliwa kwa Azimio kunaweza kuwa mikakati ya kumweka mbele kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka kama mgombea wa urais, huku ukiwalazimu viongozi wengine wa upinzani kuamua ikiwa wataendelea kushirikiana ndani ya muungano huo au watafuata mkondo tofauti. Kwa mujibu wa Profesa Monda, upinzani ukiendelea kugawanyika utampa Rais Ruto nafasi kubwa zaidi ya kutetea kiti chake 2027, ilhali muungano mmoja wenye mgombea mmoja unaweza kuongeza ushindani dhidi ya serikali ya Kenya Kwanza. "Ni wazi Wakenya wanamjua yule mgombeaji ambaye hawatampigia kura lakini bado hawajui watamchagua nani. Hii ndiyo maana lazima upinzani uweke juhudi za kuhakikisha wanaungana," akasema Profesa Monda.

read more
T

taifaleo.nation.co.ke

@taifaleo 19 hours ago

Kindiki: Kalonzo hana ajenda, na hawezi kumshinda Ruto 2027

NAIBU Rais Profesa Kithure Kindiki wikendi alimshambulia vikali Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka, akisema hana ajenda mpya ya kuwaongoza Wakenya baada ya kuhudumu serikalini kwa zaidi ya miaka 40. Akizungumza katika ziara ya maendeleo Kaunti ya Tharaka Nithi, Profesa Kindiki aliwataka viongozi wa upinzani kuwasilisha sera mbadala badala ya kutegemea siasa za chuki, migawanyiko na ukabila. "Wale wasioamini maono yetu ya Kenya mpya walete maono yao. Hawawezi kushindana nasi kwa sababu muda wao mwingi wameutumia kuhubiri chuki, migawanyiko na ukabila," akasema. Kauli hiyo inajiri huku Bw Musyoka akijitokeza kama mmoja wa vinara wa upinzani wanaolenga kumng'oa Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa Agosti 2027. Profesa Kindiki alisema Bw Musyoka ameshindwa kuonyesha mafanikio makubwa licha ya kushikilia nyadhifa mbalimbali serikalini kwa miongo kadhaa. "Huyo Kalonzo mnayetaka kutuuzia, mlete hapa. Tunamfahamu vizuri kwa sababu alisoma hapa shule ya upili ya Meru. Kama baada ya miaka 40 ya uongozi hajafanya chochote, hana jipya la kutoa sasa," akasema Profesa Kindiki. "Aende nyumbani apumzike. Tutamjengea barabara na atuombee kwa sababu huu ni wakati wetu," akaongeza. Aidha, Naibu Rais aliwashutumu viongozi wa upinzani kwa kutumia vijana kuzua vurugu badala ya kuwatafutia ajira au kuunga mkono miradi ya serikali ya kuwafaa. "Kazi ya kiongozi ni kuwasaidia vijana wapate ajira, si kuwalipa Sh200 warushe mawe na kuharibu biashara za wenzao," akasema. Profesa Kindiki pia alitoa wito wa amani na umoja, hasa katika eneo la Mlima Kenya, akisema siasa hazipaswi kugawa jamii. Aliongeza kuwa Kenya Kwanza itatafuta kura kwa kuonyesha rekodi yake ya maendeleo ikiwemo barabara, umeme, maji na miradi mingine badala ya matusi na siasa za migawanyiko.

read more