taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 27 Sep 2026 16:43:56
Kenya na Tanzania kumenyana katika vita vya kufuzu AFCON 23
TIMU ya taifa ya soka ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23, Emerging Stars, leo itaanza kampeni yake ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana (U23 AFCON) 2027 itakapokutana na Tanzania leo, katika mechi ya raundi ya kwanza katika uwanja wa Kitaifa wa Nyayo jijini Nairobi kuanzia saa tisa mchana. Tiketi za mechi zilikuwa zikiuzwa kwa Sh 200 kwa watu kawaida na Sh 500 kwa watu mashuhuri. Kocha wa Kenya Antony Kimani, Jumapili alitangaza kikosi cha mwisho cha wachezaji 27 kwa ajili ya mechi hiyo, huku timu hiyo ikilenga kuanza kampeni kwa matokeo mazuri dhidi ya watani wake wa Afrika Mashariki. Mechi hiyo itakuwa ya kwanza kwa Kenya na Tanzania kukutana katika kiwango hiki, huku timu hizo zikitafuta tiketi ya kushiriki fainali za U23 AFCON zitakazofanyika Misri mwakani. Kenya bado haijawahi kufuzu kwa fainali za mashindano hayo, huku Tanzania pia ikiwa haijawahi kufikia hatua hiyo. Kenya iliingia uwanjani mara ya mwisho mwaka 2021 wakati wa michuano ya CECAFA, ambapo ilipoteza 1-0 dhidi ya Sudan Kusini katika mechi ya mchujo. Tangu ianze kushiriki katika kiwango cha U23 mwaka huo, Kenya imecheza mechi saba katika mashindano mbalimbali, ikishinda mbili, kutoka sare mbili na kupoteza tatu. Tanzania, kwa upande wake, mara ya mwisho ilishiriki mechi za kufuzu U23 AFCON mwaka 2022, ilipoondolewa na Nigeria 3-1 kwa jumla ya mabao. Kwa jumla, Tanzania imecheza mechi nane tangu ilipoanza kushiriki katika kiwango hiki mwaka 2021, ikishinda tatu, kutoka sare nne na kupoteza moja. Kabla ya mechi hiyo, Kenya imekumbwa na pigo baada ya mshambuliaji Humphrey Aroko kuachwa nje ya kikosi kutokana na jeraha alilopata akiwa katika majukumu ya klabu yake, Rosengård ya Uswidi. Kiungo Aldrine Kibet anayeipigia RC Celta ya Uhispania naye hakusafiri kwa ajili ya mechi hiyo kutokana na suala la kibali chake cha kazi, ambacho muda wake wa matumizi unakaribia kumalizika na kwa sasa anashughulikia. Mshindi wa jumla kati ya Kenya na Tanzania atakutana na Ivory Coast katika raundi ya pili ya mchujo. Raundi ya kwanza inashirikisha timu 28 katika mikondo 14 ya mechi mbili, huku mechi za kwanza zikichezwa Septemba 20 na marudiano Oktoba 6, 2026. Mechi za raundi ya pili zimepangwa kuchezwa Novemba 9 na 17, kabla ya raundi ya tatu na ya mwisho kufanyika Machi 2027. Mshindi wa jumla katika kila mchujo saba ya raundi ya tatu atafuzu kwa fainali za U23 AFCON nchini Misri pamoja na wenyeji ambao wamepata tiketi moja kwa moja. Mashindano hayo yana umuhimu wa ziada kwa sababu yatatumika kama njia ya Afrika kupata wawakilishi katika Mashindano ya Soka ya Olimpiki ya Los Angeles 2028. Timu za Afrika zina historia nzuri katika soka ya wanaume la Olimpiki. Nigeria ilitwaa dhahabu Atlanta mwaka 1996 na kuwa taifa la kwanza la Afrika kushinda medali hiyo, kabla ya Cameroon kutwaa dhahabu Sydney mwaka 2000. Nigeria pia ilishinda fedha Beijing 2008 na shaba Rio 2016, na kuwa taifa la Afrika lililopata mafanikio mengi zaidi katika mashindano hayo. Ghana iliweka historia Barcelona mwaka 1992 kwa kuwa taifa la kwanza la Afrika kushinda medali katika soka la wanaume la Olimpiki baada ya kutwaa shaba. Kikosi cha Mwisho Walinda lango Caleb Kramer (Ado Den Haag, Uholanzi) Mateo Ochieng (Providence College, Uingereza) Collins Omondi (Kariobangi Sharks) Mabeki Ian Onyango (Mathare United) Collins Ochieng (Tusker FC) Francis Okoth (Kenya Police) Baron Ochieng (Unattached) Wycliffe Omondi (Tusker FC) Joseph Bate (Nairobi United) Price Omenda (Murang'a Seal) Viungo wa Kati Omar Ateek (Mathare United) Kevin Wangaya (Nairobi United) Kelly Madada (Afc Leopards) Oliver Machaka (Kenya Police) Andreas Odhiambo (Enkopings SK, Uswidi) Jack Onganya (Cadiz, Uhispania) Irad Mshindi (Leipja, Latvia) Washambuliaji Dancan Oluoch (Nairobi United) Lawrence Okoth (Bandari FC) Syphas Owuor (Nairobi United) Collins Okello Jeremy Bisau (Sd Huesca, Uhispania) Telena Ochieng (Tusker FC) Brooklyn Kazungu (MK Dons, Uingereza) Paul Osama (Enkopings SK, Uswidi) Henry Omollo (Mufurila Wanderers, Zambia) Hassan Beja (Red Castleue SC, UAE)
read moreOther Headlines
taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo 18 minutes ago
Vyama 94 vya kisiasa hatarini kukosa kushiriki uchaguzi wa 2027
Vyama 94 vya kisiasa nchini vimepewa hadi Desemba 7, 2026 kurekebisha kanuni zao za uteuzi wa wagombeaji, la sivyo vikose kushiriki uchaguzi mkuu wa Agosti 10, 2027. Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imesema ni vyama 11 pekee vilivyotimiza masharti ya kisheria kuhusu kanuni za uteuzi, huku vingine 94 vikihitajika kufanya marekebisho. Miongoni mwa vyama vikuu vilivyotakiwa kurekebisha kanuni hizo ni United Democratic Alliance (UDA) ya Rais William Ruto, Orange Democratic Movement (ODM), Democracy for the Citizens Party (DCP) ya aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na Linda Mwananchi Movement, iliyokuwa ikijulikana kama The Equitable Party. Hata hivyo, Wiper Patriotic Front ya Kalonzo Musyoka, Jubilee Party na The Mwananchi Party ya Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino ni miongoni mwa vyama 11 vilivyotimiza masharti. Vyama vingine vilivyofaulu ni Kenya Moja Movement, Safina, Liberal Democratic Party, Grand Dream Development, Democratic National Alliance, Chama ya Mapatano of Kenya, Vision for Development Alliance na Forward Kenya. Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon alisema tume ilikagua kanuni zilizowasilishwa na vyama ili kuhakikisha zinafuata Katiba, Sheria ya Uchaguzi na kanuni husika. Alisema tathmini hiyo ilichunguza muundo na mamlaka ya kamati za uchaguzi za vyama, taratibu za kutambua na kuteua wagombeaji, masharti ya wanaotaka kuwania nafasi za uongozi na jinsi kura za mchujo zinavyopaswa kuendeshwa. Pia, tume ilikagua jinsi vyama vinavyoshughulikia malalamishi ya ndani, ukiukaji wa kanuni za uchaguzi na masuala yanayohusu maadili ya uchaguzi. Bw Ethekon alisema vyama vilivyopatikana na kasoro vimearifiwa maeneo yanayohitaji kurekebishwa na vinapaswa kuwasilisha kanuni mpya kabla ya tarehe ya mwisho. Hata hivyo, alifafanua kuwa kutotimiza masharti katika tathmini ya kwanza hakumaanishi moja kwa moja kuwa chama kimeondolewa kwenye uchaguzi wa 2027. Alisema hatua hiyo inalenga kuvipatia vyama nafasi ya kurekebisha dosari huku tume ikihakikisha uteuzi unafanyika kwa uwazi, haki na kufuata sheria. IEBC ilitangaza ratiba muhimu za uchaguzi Agosti 25. Vyama vilitakiwa kuwasilisha majina ya maafisa walioidhinishwa na sampuli za sahihi zao kufikia Oktoba 15, huku kanuni za uteuzi zikitarajiwa kuthibitishwa na Msajili wa Vyama vya Kisiasa kufikia Oktoba 30 na kuwasilishwa kwa tume kufikia Novemba 6. Vyama pia vinapaswa kuwasilisha orodha za wanachama na majina ya wagombeaji wa kura za mchujo kufikia Machi 16, 2027, pamoja na tarehe na maeneo ya uchaguzi huo. Kura zote za mchujo zinapaswa kukamilika na mizozo ya ndani kutatuliwa kufikia Mei 8, 2027. Uteuzi wa wagombeaji unatarajiwa kuwa mtihani mkubwa kwa vyama vikuu kutokana na ushindani wa kisiasa na maslahi yanayokinzana ndani yake. ODM, chini ya Oburu Oginga, inakabiliwa na changamoto ya kudumisha ushawishi wake Nyanza katika kipindi cha baada ya kifo cha Raila Odinga. Wanasiasa wenye uzoefu wanawania nafasi mbalimbali huku baadhi wakipinga mapendekezo ya chama kugawana maeneo ya kisiasa kwa misingi ya kanda. Chama hicho pia kinakabiliwa na ushindani kutoka kwa vyama vingine, vikiwemo Movement for Democracy and Growth na Peoples' Prosperity Party ya aliyekuwa Waziri Eliud Owalo. Kwa upande wake, Bw Gachagua anajaribu kuimarisha DCP katika eneo la Mlima Kenya, ambako wanasiasa waliokuwa wameegemea UDA wanazidi kuelekea makazi yake ya kisiasa Wamunyoro kutafuta ushirikiano mpya. Hivyo, mbali na kurekebisha kanuni, vyama hivyo vinakabiliwa na jukumu la kuhakikisha kura zao za mchujo hazitazua migawanyiko inayoweza kudhoofisha nafasi zao katika uchaguzi ujao
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo 50 minutes ago
Hali si shwari ODM kuimarika kwa chama cha MDG Nyanza kukiibua wasiwasi
MVUTANO unaendelea kutokota ndani ya chama cha ODM kuhusu ushirikiano wake na chama tawala cha UDA, huku ushindani wa tiketi za uchaguzi na kuimarika kwa chama cha MDG vikiibua wasiwasi kuelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027. Hali hii inajiri huku kiongozi wa ODM Oburu Oginga akisisitiza kuwa chama hicho kitabaki imara na kuendeleza ushirikiano na Rais William Ruto, lakini baadhi ya viongozi wanataka hakikisho kuwa ODM haitapoteza uhuru wake wala maslahi ya kisiasa. Katika mkutano wa Kamati Kuu ya ODM jana, chama hicho kiliweka Januari 31, 2027 kuwa tarehe ya mwisho ya kukamilisha mazungumzo na UDA kuhusu manifesto ya pamoja itakayoweka msingi wa muungano unaopendekezwa. Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa Junet Mohamed alisema pande hizo mbili zinapaswa kukubaliana kuhusu sera na masuala yatakayowaunganisha kabla ya uchaguzi. "Tunataka kupokea ripoti ifikapo Januari 31 kuhusu masuala na sera zitakazotuunganisha iwapo tutaunda muungano na UDA. Tutashirikiana kuendeleza ajenda ya Wakenya," alisema. Oburu, ambaye alikuwa akimpokea aliyekuwa Mbunge wa Bureti Paul Sang aliyejiunga na ODM kutoka Kanu, alisisitiza kuwa chama hicho hakitaruhusu watu wa nje kukivuruga. Alisema waliohama vyama vingine na kujiunga na ODM hawatapewa tiketi za moja kwa moja, bali watashindana na wanachama wengine katika kura za mchujo. "Hakuna mtu aliye na upendeleo maalumu ndani ya ODM. Kila mtu atashindana na mwenzake. Tutafanya kura za mchujo huru na haki," alisema. Pia aliwaonya maafisa wa chama wanaodaiwa kupokea hongo ili kuwapa wagombeaji tiketi kuwa watachukuliwa hatua. Hata hivyo, wasiwasi mkubwa unahusu ushindani wa kisiasa katika ngome za ODM, hasa Nyanza, ambako MDG inayoongozwa na Mbunge wa Ugenya, David Ochieng inajijenga. "Tunajua mahali tunakotoka na kule tunakoelekea; hatutakubali kuvurugwa na mtu yeyote... MDG ni chama cha mtu mmoja wala hakiwezi kudai kutufundisha jinsi vyama vya kisiasa vinavyoendeshwa," akasema Dkt Oburu kuhusu ushindani kutoka kwa MDG. Katika Kaunti ya Kisumu, tetesi kuwa ODM inaweza kuunga mkono Mbunge wa Kisumu Magharibi Rosa Buyu kuwania ugavana na Mbunge wa Nyakach Aduma Owuor kuwa naibu wake zimezua malalamishi miongoni mwa wagombeaji wengine. Naibu Gavana Mathews Owili alisema baadhi ya viongozi tayari wanapendelea wagombeaji fulani badala ya kusubiri kura za mchujo. "Baadhi ya viongozi wa chama wanaegemea upande mmoja na kuonyesha wazi kuwa wanaunga mkono tiketi hiyo. Tumeahidiwa kura za mchujo huru na za haki, na hilo ndilo tunalopaswa kufuata," alisema. Owili alikataa uwezekano wa kujiunga na MDG, akisema anashikilia misingi na uongozi wa marehemu Raila Odinga. MDG pia imekuwa ikivutia wanasiasa wenye uzoefu katika eneo hilo. Miongoni mwao ni aliyekuwa Katibu wa Kaunti ya Homa Bay Isaiah Ogwe, anayemezea mate kiti cha ubunge cha Homa Bay Mjini, na aliyekuwa Katibu Mkuu katika Wizara Julius Jwan, anayelenga ubunge Ndhiwa. Ochieng mwenyewe anawania ugavana wa Siaya na chama chake kinasema kimejenga miundo katika wadi zote 30 za Siaya na kinalenga kushinda angalau viti 20 vya bunge la kaunti. Mwenyekiti wa kitaifa wa ODM Gladys Wanga hivi majuzi alitangaza Nyanza kuwa ngome ya ODM na kuonya vyama pinzani dhidi ya kujaribu kujijenga katika eneo hilo. Aidha, baadhi ya wanachama wanashuku kuwa UDA inatumia vyama vingine kudhoofisha ODM katika ngome zake. Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu aliambia Taifa Leo kuwa matamshi ya Katibu katika Wizara ya Usalama wa Ndani Raymond Omollo kuhusu upinzani wake kwa mfumo wa kugawana maeneo ya kisiasa yamezidisha hofu hiyo. Omollo aliwaonya viongozi wa ODM dhidi ya kuwatenga wanasiasa wa vyama vingine kupitia madai ya kugawana maeneo, akisema hatua hiyo inaweza kuishia kudhoofisha wote. Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa ODM wanasisitiza kuwa chama kinapaswa kupata mgao wa asilimia 50 kwa 50 katika mpango wowote na UDA, pamoja na kuhakikishiwa maeneo yake ya kisiasa. Wakati huohuo, Kamati Kuu imeidhinisha ziara ya kuhamasisha wanachama wake katika eneo la Pwani kuanzia Desemba 6 hadi 22, ambapo viongozi watatembelea maeneo bunge na wadi kuimarisha miundo ya chama.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo 1 hours ago
Sababu za Wakatoliki kuwaombea wafu mwezi Novemba
Kwa Wakatoliki, mwezi Novemba ni kipindi maalumu cha kuwakumbuka na kuwaombea waumini waliofariki, wakiamini kuwa kifo hakikatishi uhusiano wa kiroho kati ya walio hai na waliotangulia mbele ya haki. Katika kipindi hiki, waumini huombea jamaa, marafiki na watu wengine waliofariki, wakiomba Mungu awasamehe dhambi zao na kuwapa pumziko la milele. Wengine huagiza Misa maalumu, kutembelea makaburi na kutoa sadaka kwa nia ya kuwaombea wapendwa wao. Ibada hii huanza Novemba 1, Siku ya Watakatifu Wote, ambapo Kanisa huwaheshimu wale wanaoaminiwa kuwa tayari wako mbinguni. Novemba 2 ni Siku ya Waumini Wote Waliokufa, ambapo sala hutolewa kwa marehemu, hasa wale wanaoaminika kuwa katika toharani wakisubiri utakaso kabla ya kuingia mbinguni. Siku hizi mbili zinaakisi kile Kanisa Katoliki linachokiita Umoja wa Watakatifu. Hii ni imani kwamba kuna uhusiano wa kiroho kati ya waumini walio hai duniani, roho zinazopitia utakaso na wale ambao tayari wako mbinguni. Ingawa Novemba 2 ndiyo siku rasmi ya kuwakumbuka marehemu, jumuiya nyingi za Wakatoliki huendeleza ibada hiyo katika mwezi mzima kupitia Misa, sala na ziara kwenye makaburi. Desturi hii inahusishwa na Mtakatifu Odilo, kiongozi wa watawa wa Benedicto, ambaye takriban mwaka 998 alihimiza makao ya watawa aliyokuwa akisimamia kufanya sala, kufunga na Misa kwa ajili ya wafu. Baadaye desturi hiyo ilisambaa katika Kanisa la Magharibi. Lakini kwa nini Wakatoliki huwaombea watu waliokufa? Je, Misa inayotolewa kwa wafu ina umuhimu gani? Na je, sala za walio hai zinaweza kusaidia roho za waliotangulia? Askofu Cleophas Oseso wa Dayosisi ya Nakuru alitoa maelezo kuhusu umuhimu wa kuwaombea wafu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Waumini Wote Waliokufa Novemba 2. Alisema marehemu wanahitaji sala kwa sababu roho ya binadamu haifi. "Wafu wanahitaji sala zetu kwa sababu kuna kitu ndani ya kila binadamu kinachobaki milele, nacho ni roho," alisema. Askofu huyo alionya dhidi ya kutumia fedha nyingi kwenye mazishi huku familia zikisahau mahitaji ya kiroho ya marehemu. Alisema wafu hawawezi kula chakula, kutumia fedha wala kufurahia majeneza ya kifahari yanayonunuliwa kwa ajili yao. Badala yake, alisema, wanachohitaji zaidi ni sala za walio hai. Aliongeza kuwa sala zinazotolewa sasa zina umuhimu mkubwa kwa waliotangulia, huku akiwataka waumini kuwaombea wafu kwa matumaini kwamba siku zao zikifika, kutakuwa na watu watakaowaombea pia. Mafundisho haya yanatokana na imani ya Kanisa Katoliki kuhusu toharani. Hii ni hali ya utakaso wa roho za watu wanaokufa wakiwa katika neema ya Mungu lakini bado hawajatakaswa kikamilifu kabla ya kuingia mbinguni. Toharani, kulingana na Wakatoliki, si jehanamu wala nafasi ya pili ya kupata wokovu. Ni hatua ya mwisho ya utakaso wa roho kabla ya kuingia katika uwepo wa Mungu. Kwa mfano, mtu anaweza kuwa ameishi maisha ya kumwamini Mungu na kufanya mema, lakini kama binadamu akawa na udhaifu, makosa na dhambi ambazo hazijashughulikiwa kikamilifu. Kanisa linafundisha kuwa mtu huyo anaweza kuhitaji utakaso kabla ya kuingia mbinguni. Ndiyo maana Wakatoliki huhimizwa kuwaombea marehemu, kutoa sadaka na kuwatolea Misa. Imani hii inatofautiana na mafundisho ya madhehebu mengi ya Kiprotestanti na Kiinjilisti, ambayo husisitiza kuwa hatima ya roho ni mbinguni au jehanamu. Wanamageuzi wa Kanisa wa karne ya 16, akiwemo Martin Luther na John Calvin, walipinga fundisho la toharani. Padre Ron Rolheiser, kasisi na mwanatheolojia kutoka Canada, anaeleza kuwa toharani haipaswi kueleweka kama eneo maalumu lililotenganishwa na mbinguni, bali kama hali ya utakaso wa mwisho. Katika makala yake What is Purgatory? iliyochapishwa na Catholic Outlook Agosti 28, 2026, anafafanua toharani kwa kutumia mfano wa punje ya ngano inayoanguka ardhini na kufa ili kuzaa matunda mapya. Katika Biblia, Wakatoliki hutaja kitabu cha Wamakabayo wa Pili 12:38-46, kinachoeleza jinsi Yuda Makabayo alivyoomba na kutoa sadaka kwa ajili ya wanajeshi waliokuwa wamekufa, akiamini kuwa wangeweza kusamehewa dhambi zao. Kifungu hicho kinahitimisha kwa kueleza kuwa kuwaombea wafu ni jambo takatifu na jema. Imani hii pia inahusishwa na Umoja wa Watakatifu, unaoeleza uhusiano wa kiroho kati ya waumini walio hai, roho zinazotakaswa na wale ambao tayari wako mbinguni. Kwa mujibu wa mafundisho hayo, kifo hakikatishi kabisa uhusiano wa waumini katika Kanisa. Askofu Peter Kimani Ndung'u wa Dayosisi ya Embu anahimiza waumini kuendelea kuwaombea marehemu, akisema kifo si mwisho bali ni mpito kuelekea maisha ya milele na Mungu. Katika maadhimisho ya Siku ya Waumini Wote Waliokufa, mamia ya Wakristo, mapadri na watawa walikusanyika katika Kanisa Kuu la St Peter and Paul, Karurina, Embu, kwa Misa maalumu ya kuwaombea maaskofu na mapadri waliozikwa katika makaburi ya kanisa hilo. Katika mahubiri yake, Askofu Kimani aliwaomba waumini kumuomba Mungu awahurumie wafu, hasa wale wanaoaminika kuwa katika toharani. Aliwahimiza pia kuishi maisha ya haki huku wakijiandaa kwa maisha ya baadaye. Kwa Wakatoliki, Misa inayotolewa kwa ajili ya mtu aliyefariki si ibada ya kumkumbuka tu, bali ni sherehe ya Ekaristi ambapo waumini humuomba Mungu ampokee wafu katika rehema zake. Familia zinaweza kuomba Misa kwa ajili ya marehemu mara tu baada ya mazishi, siku ya 40, katika kumbukumbu ya kifo, siku ya kuzaliwa au Novemba 2. Baadhi ya familia huendeleza desturi hiyo kwa miaka mingi, hata baada ya kipindi cha maombolezo kupita. Mchakato wa kuomba Misa ni rahisi. Familia inaweza kufika katika ofisi ya parokia ambako hupewa bahasha ya kuandika jina la marehemu na nia ya Misa. Bahasha hiyo hurudishwa pamoja na sadaka ya fedha ambayo kwa kawaida hutolewa kulingana na uwezo wa familia. Padre anaweza kulitaja jina la marehemu wakati wa Sala ya Ekaristi, kabla ya waumini kupokea Komunyo. John Otiso, muumini wa Kanisa Katoliki la St Catherine of Siena, Kitusuru, anasema huwaombea jamaa zake waliokufa kila mwaka kupitia Misa. "Chini ya sala, ninawakabidhi jamaa zangu waliokufa kwa Mungu kila mwaka. Ninawatolea Misa ili popote walipo wapate msamaha na rehema za Mungu, na Mungu awapokee katika mwanga wa uso wake," anasema. Otiso anasema desturi hiyo humfariji kwa sababu sala ndiyo njia pekee aliyobaki nayo ya kuwaonyesha upendo wapendwa wake. Anaamini kuwa roho haifi na kwamba roho za jamaa zake zinanufaika kutokana na sala anazowatolea. Askofu Kevin C Rhoades wa Amerika anaeleza kuwa kuwaombea marehemu ni tendo la upendo na wajibu wa kiroho. Katika mahubiri yake ya Siku ya Waumini Wote Waliokufa ya mwaka 2016, yenye kichwa Devotion to the Memory of the Dead in November, alisema waumini wana wajibu wa kuwaunga mkono waliotangulia kwa sala na sadaka ili nao wafikie ufalme wa mbinguni. Hata hivyo, kuwaombea marehemu hakumaanishi kujaribu kuwasiliana nao, kuwaita mizimu au kutafuta ujumbe kutoka kwao. Mafundisho ya Kanisa Katoliki hayaelekezi waumini kuitisha roho za marehemu. Badala yake, sala hizo huelekezwa kwa Mungu, wakimuomba awahurumie waliokufa, awasamehe na kuwapa uzima wa milele. Tofauti hii ni muhimu hasa barani Afrika ambako imani za Kikristo kuhusu kifo huishi sambamba na tamaduni mbalimbali zinazohusiana na waliotangulia. Kwa Wakatoliki, kuwaombea marehemu ni tendo la kiroho linalolenga kuomba rehema za Mungu, si kutafuta mawasiliano na waliokufa. Utafiti kuhusu historia ya desturi hii unaonyesha kuwa kuwaombea marehemu si jambo lililoanza baada ya kuanzishwa rasmi kwa fundisho la toharani. Katika utafiti wake Purgatory in Historical Perspective, uliochapishwa na St Andrews Encyclopaedia of Theology mwaka 2023, Isabel Moreira anaeleza jinsi desturi ya kuwaombea marehemu ilivyoendelea ndani ya historia ya Ukristo. Anasema Wakristo walikuwa wakiwaombea waliokufa tangu nyakati za kale, binafsi na katika jumuiya zao. Hata hivyo, wanahistoria wanaeleza kuwa neno la Kilatini purgatorium lilianza kutumika katika karne ya 12.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo 1 hours ago
Viongozi wa makanisa wakataa kusitisha kutangaza ibada kwenye runinga na mitandao
ONYO la Kamishna wa Ulinzi wa Data anayeondoka, Immaculate Kassait, kwa makanisa kwamba lazima yapate idhini ya waumini kabla ya kutangaza picha zao mubashara, limezua hasira miongoni mwa viongozi wa kidini. Agizo hilo linataka makanisa kupata ridhaa ya wazi kutoka kwa waumini kabla ya kutangaza ibada mubashara au kuchapisha video na picha zao kwenye mitandao ya kijamii. Hata hivyo, viongozi wa makanisa wamelipinga wakisema linalenga taasisi za kidini pekee huku shughuli nyingine zinazohusisha upigaji picha na video zikiachwa. Mwenyekiti wa kitaifa wa Church and Clergy Association of Kenya, Askofu Hudson Ndeda, amehoji kwa nini tume hiyo imeelekeza nguvu zake kwa makanisa pekee ilhali wanasiasa pia hutangaza mikutano yao mubashara. "Tutatii agizo hilo pale watakapofanya vivyo hivyo kwa mikutano ya kisiasa na maeneo mengine yote ambako video na picha hunaswa, ikiwemo sherehe na vyombo vya habari," alisema Askofu Ndeda. Ingawa agizo hilo linalenga kuhakikisha taasisi zinafuata Sheria ya Ulinzi wa Data ya mwaka 2019, makanisa yamehoji muda ambao limetolewa. V iongozi hao wanataka kujua kwa nini kamishna ameamua kutekeleza masharti hayo mwishoni mwa muhula wake. Askofu Ndeda ameyashauri makanisa kupuuza agizo hilo licha ya hatari ya kutozwa faini ya Sh5 milioni kwa kukosa kupata ridhaa ya waumini. "Kwa sasa, turuhusiwe kukaidi sheria hiyo ya kibaguzi inayolenga kuingilia tunavyoendesha ibada. Je, kanisa ndilo eneo pekee ambako matangazo mubashara na upigaji picha hufanyika?" alihoji. Kwa mujibu wake, hatua hiyo inaweza kuchochea umma dhidi ya makanisa. "Tunapanga kuwasiliana na tume hiyo na ikikataa kusikiliza hoja zetu, tutaenda mahakamani. Tunaamini tutashinda kesi hiyo kwa urahisi. Kwa nini wanalenga makanisa, na ni nani amewahi kulazimishwa kuhudhuria kanisa ambako ibada hutangazwa mubashara? Hatua hiyo inaweza kusababisha vurugu zisizo za lazima," alisema.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo 2 hours ago
Sababu za Wakatoliki kuwaombea wafu mwezi Novemba
KWA Wakatoliki, mwezi Novemba ni kipindi maalumu cha kuwakumbuka na kuwaombea waumini waliofariki, wakiamini kuwa kifo hakikatishi uhusiano wa kiroho kati ya walio hai na waliotangulia mbele za haki. Katika kipindi hiki, waumini huombea jamaa, marafiki na watu wengine waliofariki, wakiomba Mungu awasamehe dhambi zao na kuwapa pumziko la milele. Wengine huagiza Misa maalumu, kutembelea makaburi na kutoa sadaka kwa nia ya kuwaombea wapendwa wao. Ibada hii huanza Novemba 1, Siku ya Watakatifu Wote, ambapo Kanisa huwaheshimu wale wanaoaminiwa kuwa tayari wako mbinguni. Novemba 2 ni Siku ya Waumini Wote Waliokufa, ambapo sala hutolewa kwa marehemu, hasa wale wanaoaminika kuwa katika toharani wakisubiri utakaso kabla ya kuingia mbinguni. Siku hizi mbili zinaakisi kile Kanisa Katoliki linachokiita Umoja wa Watakatifu. Hii ni imani kwamba kuna uhusiano wa kiroho kati ya waumini walio hai duniani, roho zinazopitia utakaso na wale ambao tayari wako mbinguni. Ingawa Novemba 2 ndiyo siku rasmi ya kuwakumbuka marehemu, jumuiya nyingi za Wakatoliki huendeleza ibada hiyo katika mwezi mzima kupitia Misa, sala na ziara kwenye makaburi. Desturi hii inahusishwa na Mtakatifu Odilo, kiongozi wa watawa wa Benedicto, ambaye takriban mwaka 998 alihimiza makao ya watawa aliyokuwa akisimamia kufanya sala, kufunga na Misa kwa ajili ya wafu. Baadaye desturi hiyo ilisambaa katika Kanisa la Magharibi. Lakini kwa nini Wakatoliki huwaombea watu waliokufa? Je, Misa inayotolewa kwa wafu ina umuhimu gani? Na je, sala za walio hai zinaweza kusaidia roho za waliotangulia? Askofu Cleophas Oseso wa Dayosisi ya Nakuru alitoa maelezo kuhusu umuhimu wa kuwaombea wafu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Waumini Wote Waliokufa Novemba 2. Alisema marehemu wanahitaji sala kwa sababu roho ya binadamu haifi. "Wafu wanahitaji sala zetu kwa sababu kuna kitu ndani ya kila binadamu kinachobaki milele, nacho ni roho," alisema. Askofu huyo alionya dhidi ya kutumia fedha nyingi kwenye mazishi huku familia zikisahau mahitaji ya kiroho ya marehemu. Alisema wafu hawawezi kula chakula, kutumia fedha wala kufurahia majeneza ya kifahari yanayonunuliwa kwa ajili yao. Badala yake, alisema, wanachohitaji zaidi ni sala za walio hai. Aliongeza kuwa sala zinazotolewa sasa zina umuhimu mkubwa kwa waliotangulia, huku akiwataka waumini kuwaombea wafu kwa matumaini kwamba siku zao zikifika, kutakuwa na watu watakaowaombea pia. Mafundisho haya yanatokana na imani ya Kanisa Katoliki kuhusu toharani. Hii ni hali ya utakaso wa roho za watu wanaokufa wakiwa katika neema ya Mungu lakini bado hawajatakaswa kikamilifu kabla ya kuingia mbinguni. Toharani, kulingana na Wakatoliki, si jehanamu wala nafasi ya pili ya kupata wokovu. Ni hatua ya mwisho ya utakaso wa roho kabla ya kuingia katika uwepo wa Mungu. Kwa mfano, mtu anaweza kuwa ameishi maisha ya kumwamini Mungu na kufanya mema, lakini kama binadamu akawa na udhaifu, makosa na dhambi ambazo hazijashughulikiwa kikamilifu. Kanisa linafundisha kuwa mtu huyo anaweza kuhitaji utakaso kabla ya kuingia mbinguni. Ndiyo maana Wakatoliki huhimizwa kuwaombea marehemu, kutoa sadaka na kuwatolea Misa. Imani hii inatofautiana na mafundisho ya madhehebu mengi ya Kiprotestanti na Kiinjilisti, ambayo husisitiza kuwa hatima ya roho ni mbinguni au jehanamu. Wanamageuzi wa Kanisa wa karne ya 16, akiwemo Martin Luther na John Calvin, walipinga fundisho la toharani. Padre Ron Rolheiser, kasisi na mwanatheolojia kutoka Canada, anaeleza kuwa toharani haipaswi kueleweka kama eneo maalumu lililotenganishwa na mbinguni, bali kama hali ya utakaso wa mwisho. Katika makala yake What is Purgatory? iliyochapishwa na Catholic Outlook Agosti 28, 2026, anafafanua toharani kwa kutumia mfano wa punje ya ngano inayoanguka ardhini na kufa ili kuzaa matunda mapya. Katika Biblia, Wakatoliki hutaja kitabu cha Wamakabayo wa Pili 12:38-46, kinachoeleza jinsi Yuda Makabayo alivyoomba na kutoa sadaka kwa ajili ya wanajeshi waliokuwa wamekufa, akiamini kuwa wangeweza kusamehewa dhambi zao. Kifungu hicho kinahitimisha kwa kueleza kuwa kuwaombea wafu ni jambo takatifu na jema. Imani hii pia inahusishwa na Umoja wa Watakatifu, unaoeleza uhusiano wa kiroho kati ya waumini walio hai, roho zinazotakaswa na wale ambao tayari wako mbinguni. Kwa mujibu wa mafundisho hayo, kifo hakikatishi kabisa uhusiano wa waumini katika Kanisa. Askofu Peter Kimani Ndung'u wa Dayosisi ya Embu anahimiza waumini kuendelea kuwaombea marehemu, akisema kifo si mwisho bali ni mpito kuelekea maisha ya milele na Mungu. Katika maadhimisho ya Siku ya Waumini Wote Waliokufa, mamia ya Wakristo, mapadri na watawa walikusanyika katika Kanisa Kuu la St Peter and Paul, Karurina, Embu, kwa Misa maalumu ya kuwaombea maaskofu na mapadri waliozikwa katika makaburi ya kanisa hilo. Katika mahubiri yake, Askofu Kimani aliwaomba waumini kumuomba Mungu awahurumie wafu, hasa wale wanaoaminika kuwa katika toharani. Aliwahimiza pia kuishi maisha ya haki huku wakijiandaa kwa maisha ya baadaye. Kwa Wakatoliki, Misa inayotolewa kwa ajili ya mtu aliyefariki si ibada ya kumkumbuka tu, bali ni sherehe ya Ekaristi ambapo waumini humuomba Mungu ampokee wafu katika rehema zake. Familia zinaweza kuomba Misa kwa ajili ya marehemu mara tu baada ya mazishi, siku ya 40, katika kumbukumbu ya kifo, siku ya kuzaliwa au Novemba 2. Baadhi ya familia huendeleza desturi hiyo kwa miaka mingi, hata baada ya kipindi cha maombolezo kupita. Mchakato wa kuomba Misa ni rahisi. Familia inaweza kufika katika ofisi ya parokia ambako hupewa bahasha ya kuandika jina la marehemu na nia ya Misa. Bahasha hiyo hurudishwa pamoja na sadaka ya fedha ambayo kwa kawaida hutolewa kulingana na uwezo wa familia. Padre anaweza kulitaja jina la marehemu wakati wa Sala ya Ekaristi, kabla ya waumini kupokea Komunyo. John Otiso, muumini wa Kanisa Katoliki la St Catherine of Siena, Kitusuru, anasema huwaombea jamaa zake waliokufa kila mwaka kupitia Misa. "Chini ya sala, ninawakabidhi jamaa zangu waliokufa kwa Mungu kila mwaka. Ninawatolea Misa ili popote walipo wapate msamaha na rehema za Mungu, na Mungu awapokee katika mwanga wa uso wake," anasema. Otiso anasema desturi hiyo humfariji kwa sababu sala ndiyo njia pekee aliyobaki nayo ya kuwaonyesha upendo wapendwa wake. Anaamini kuwa roho haifi na kwamba roho za jamaa zake zinanufaika kutokana na sala anazowatolea. Askofu Kevin C Rhoades wa Amerika anaeleza kuwa kuwaombea marehemu ni tendo la upendo na wajibu wa kiroho. Katika mahubiri yake ya Siku ya Waumini Wote Waliokufa ya mwaka 2016, yenye kichwa Devotion to the Memory of the Dead in November, alisema waumini wana wajibu wa kuwaunga mkono waliotangulia kwa sala na sadaka ili nao wafikie ufalme wa mbinguni. Hata hivyo, kuwaombea marehemu hakumaanishi kujaribu kuwasiliana nao, kuwaita mizimu au kutafuta ujumbe kutoka kwao. Mafundisho ya Kanisa Katoliki hayaelekezi waumini kuitisha roho za marehemu. Badala yake, sala hizo huelekezwa kwa Mungu, wakimuomba awahurumie waliokufa, awasamehe na kuwapa uzima wa milele. Tofauti hii ni muhimu hasa barani Afrika ambako imani za Kikristo kuhusu kifo huishi sambamba na tamaduni mbalimbali zinazohusiana na waliotangulia. Kwa Wakatoliki, kuwaombea marehemu ni tendo la kiroho linalolenga kuomba rehema za Mungu, si kutafuta mawasiliano na waliokufa. Utafiti kuhusu historia ya desturi hii unaonyesha kuwa kuwaombea marehemu si jambo lililoanza baada ya kuanzishwa rasmi kwa fundisho la toharani. Katika utafiti wake Purgatory in Historical Perspective, uliochapishwa na St Andrews Encyclopaedia of Theology mwaka 2023, Isabel Moreira anaeleza jinsi desturi ya kuwaombea marehemu ilivyoendelea ndani ya historia ya Ukristo. Anasema Wakristo walikuwa wakiwaombea waliokufa tangu nyakati za kale, binafsi na katika jumuiya zao. Hata hivyo, wanahistoria wanaeleza kuwa neno la Kilatini purgatorium lilianza kutumika katika karne ya 12.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo 3 hours ago
IEBC yakana kufungulia Gachagua mlango kugombea urais 2027
TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imekanusha madai kwamba imemfungulia njia aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2027. Katika taarifa, tume hiyo ilisema bado haijatoa uamuzi wowote kuhusu iwapo Bw Gachagua anastahili kugombea urais au la, ikisisitiza kuwa suala hilo litashughulikiwa wakati mwafaka wa mchakato wa uchaguzi. "Tume haijamuidhinisha wala kutoa uamuzi kuhusu ufaafu wa Mheshimiwa Rigathi Gachagua kuwania urais katika uchaguzi wa 2027. Uamuzi kuhusu ufaafu wa mgombeaji yeyote utafanywa katika hatua inayofaa ya mchakato wa uchaguzi kwa kuzingatia Katiba na sheria husika," ilisema IEBC. Ufafanuzi huo ulitolewa baada ya Mkurugenzi wa Sheria wa IEBC, Chrispine Owiye, kueleza Jumanne kwamba tume haina mamlaka ya kumzuia mtu kuwania kiti cha kisiasa kwa misingi ya masuala ya uadilifu ikiwa bado ana kesi mahakamani. Bw Owiye alikuwa akifafanua masharti ya Katiba kuhusu watu wanaostahili au wasiostahili kugombea uchaguzi. Alisema Mahakama Kuu, kupitia Jaji Anthony Mrima mwaka 2018, iliamua kuwa IEBC haina mamlaka ya kumzuia mtu kuwania uchaguzi kwa misingi hiyo. Hata hivyo, tume ilikata rufaa dhidi ya uamuzi huo na bado inasubiri hukumu. 'Tuna matumaini kwamba tutapata uamuzi utakaotupendelea,' alisema. Bw Owiye alirejelea Kifungu cha 99(3) cha Katiba kinachosema mtu hawezi kuzuiwa kugombea ubunge hadi uwezekano wote wa kukata rufaa au kuomba mapitio ya hukumu au uamuzi husika uwe umemalizika. Alisema mtu anayechunguzwa au anayekabiliwa na mashtaka mahakamani hawezi kuzuiwa kugombea kwa sababu bado anachukuliwa kuwa hana hatia hadi mahakama ithibitishe vinginevyo. 'Hauwezi kumzuia mtu anayechunguzwa au anayekabiliwa na mashtaka mahakamani. Anachukuliwa kuwa hana hatia hadi atakapopatikana na hatia. Hata aliyepatikana na hatia anaweza kugombea iwapo anaonyesha kuwa amekata rufaa au ameomba mapitio ya uamuzi huo,' alisema. Matamshi hayo yalitafsiriwa na baadhi ya wachambuzi kuwa IEBC imefungua mlango kwa viongozi walioondolewa mamlakani kupitia mchakato wa kumwondoa kiongozi madarakani kuwania uchaguzi wa 2027. Miongoni mwao ni Gachagua, aliyekuwa Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu, aliyekuwa Gavana wa Meru Kawira Mwangaza na aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko. Hata hivyo, IEBC ilisisitiza kuwa maelezo ya Bw Owiye yalihusu tu masharti ya Kifungu cha 99 na 193 kuhusu sifa na vigezo vya kutostahili kugombea ubunge na udiwani. 'Taarifa yake haikuhusu kuondolewa mamlakani chini ya Kifungu cha 75, mchakato wa bunge au ufaafu wa mtu aliyeondolewa mamlakani kugombea uchaguzi,' ilisema tume hiyo. IEBC ilionya vyombo vya habari dhidi ya kutoa taarifa zisizo na muktadha kuhusu masuala nyeti ya kikatiba na uchaguzi, ikivitaka kuhakikisha usahihi na kuthibitisha habari kabla ya kuzichapisha. Mjadala huo pia umeibua tofauti za msimamo kati ya IEBC na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kuhusu nafasi ya watu wanaokabiliwa na tuhuma za ufisadi katika uchaguzi. Kabla ya uchaguzi wa 2022, EACC iliwasilisha majina ya watu 241 ili wazuiwe kugombea kwa misingi ya uadilifu. Hata hivyo, Bw Owiye alisema IEBC ilibaini kuwa ni watu watano pekee walioweza kuzuiwa kwa mujibu wa sheria zilizokuwepo. EACC ililalamika kuwa baadhi ya watu ambao ilitaka wazuiwe baadaye walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi. Mnamo Jumatatu, Mkurugenzi Mkuu wa EACC Abdi Mohamud alisisitiza kuwa tume hiyo haina mamlaka ya kikatiba ya kuwazuia wagombeaji kushiriki uchaguzi, akisema jukumu hilo ni la IEBC. EACC imekuwa ikisisitiza kuwa kanuni ya mtu kuchukuliwa kuwa hana hatia hadi athibitishwe kuwa na hatia haipaswi kutumiwa kuwapa nafasi ya kugombea watu ambao tayari wamehukumiwa kwa makosa ya jinai, hata kama wamekata rufaa.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo 10 hours ago
Mamia kunufaika na mradi wa kiwanda cha Bamburi
KIWANDA kipya cha kuzalisha kemikali ya kuunda saruji kinachojengwa Matuga, Kaunti ya Kwale, kinatarajiwa kuongeza uwezo wa Bamburi Cement kuzalisha kemikali ya Clinker kutoka tani milioni moja hadi milioni 2.6 kwa mwaka. Mradi huo wa Sh250 milioni pia utaongeza uwezo wa kampuni hiyo kuzalisha saruji kutoka tani milioni 1.8 hadi milioni nne kila mwaka, hatua inayolenga kuimarisha sekta ya ujenzi nchini na kupunguza utegemezi wa uagizaji wa bidhaa hiyo. Rais William Ruto aliweka jiwe la msingi la mradi huo, uliohudhuriwa na viongozi wa serikali, wawekezaji na viongozi wa eneo hilo. Miongoni mwa waliohudhuria ni Mawaziri Hassan Joho na Salim Mvurya, Mkurugenzi Mkuu wa Amsons Group Edha Nahdi, Gavana wa Kwale Fatuma Achani, Spika wa Seneti Amason Kingi na Mwenyekiti wa Bodi ya Bamburi Cement Dkt John Simba. Akizungumza katika hafla hiyo, Nahdi alisema uwekezaji huo unaonyesha dhamira ya muda mrefu ya Amsons Group katika kukuza uchumi wa Kenya na kuimarisha uzalishaji wa bidhaa nchini. Kwa upande wake, Dkt Simba alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha jamii zinazoishi karibu na mradi zinanufaika na uwekezaji huo. Alitaja mpango wa kuhamisha wakazi wa Kijiji cha Mwachome, ambao ulihusisha pia mafunzo ya usimamizi wa fedha ili kuwasaidia wakazi walioathiriwa kutumia vizuri rasilimali walizopokea. Gavana Achani alitoa wito kwa wakazi wa Matuga na wafanyabiashara wa eneo hilo kushirikishwa kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huo ili wanufaike na fursa za kiuchumi. Kiwanda hicho kinatarajiwa kuunda zaidi ya nafasi 10,000 za ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, hususan katika sekta za usafirishaji, uchimbaji wa mawe. Mkurugenzi Mkuu wa Wave 360 Africa, Zedd Mukoya, alisema mradi huo ni fursa kwa vijana wa Kwale kushiriki katika maendeleo ya viwanda katika kaunti yao. "Matumaini yangu ni kwamba siku moja kijana kutoka Kwale ataweza kuutazama kiwanda hicho na kusema, 'Nilisaidia kukijenga na kimenipa mustakabali mzuri katika eneo langu,'" alisema Mukoya Kampuni ya Wave 360 Africa ilihusika na maandalizi na uratibu wa hafla hiyo, ikisimamia miundombinu, uwekaji chapa, itifaki na shughuli za uwanjani.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 25 Nov 2026 04:57:18
Askofu Wanjiru aishinikiza IEBC ihakikishe uwazi kwenye kura
UPINZANI nchini umeitaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kushughulikia wasiwasi ulioibuliwa na wadau kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2027. Mwaniaji wa Ugavana Nairobi Askofu Margaret Wanjiru amesema imani ya wananchi kwa tume hiyo inapungua huku wapigakura wakijiuliza iwapo iko tayari kuendesha uchaguzi, mfumo utakaotumiwa na usahihi wa sajili ya wapigakura. Akizungumza Jumanne baada ya kuzindua makao makuu ya chama cha Kenya Moja Movement Party (KMMP) katika Barabara ya Kiambu, Bi Wanjiru, ambaye ni kiongozi wa chama hicho, alisema IEBC inapaswa kuwahakikishia Wakenya kuwa uchaguzi ujao utakuwa huru, wa haki na uwazi. "Tunaitaka IEBC kuonyesha uhuru, kutopendelea upande wowote na kuwa tayari kusimamia uchaguzi mkuu huru, wa haki, wa kuaminika na ulio wazi. Uaminifu wa demokrasia yetu unategemea mchakato wa uchaguzi ambao Wakenya wanaweza kuutegemea," akasema Bi Wanjiru. "Kwa sasa kuna upungufu wa imani nchini. IEBC lazima irejeshe imani hiyo kwa Wakenya," akasema. Alisema tume hiyo inaweza kurejesha imani ya wananchi kwa kuhakikisha kila kura inahesabiwa, wagombeaji wanatendewa kwa usawa na matakwa ya wananchi yanaheshimiwa. Aliongeza kuwa IEBC inapaswa kushughulikia mapema masuala yanayohusu maandalizi ya uchaguzi, uwazi na uadilifu wa mchakato mzima. Matamshi yake yalijiri siku mbili baada ya kiongozi DCP, Rigathi Gachagua, kuipa IEBC hadi Januari 2027 kutatua malalamishi ya upinzani au ikabiliwe na maandamano ya kitaifa. Wakati wa hafla hiyo, Bi Wanjiru alitangaza kuwa chama chake kitahakikisha mchujo unaendeshwa kwa uwazi kinapojitayarisha kushindania viti mbalimbali vya uchaguzi nchini. Pia alimkosoa Gavana Johnson Sakaja, akidai utawala wake haujafanya juhudi za kutosha kuboresha maisha ya wakazi. Alisema akichaguliwa atashughulikia mgao wa maji, mifumo mibovu ya mifereji ya maji, taka zinazotapakaa jijini, msongamano wa magari na hali mbaya ya barabara. "Sisi akina mama ni watu wa usafi na kama ningekuwa gavana wa Nairobi, tusingekuwa na tatizo la taka. Siwezi kuvumilia kuona kaunti chafu. Tuna kiongozi ambaye haelewi maana ya uongozi. Hata akipewa wadhifa bila malipo, ambao hakufanyia kazi, hajui la kufanya nao," akasema. Pia aliutaka utawala wa Rais William Ruto kushughulikia uhaba wa maji jijini Nairobi, akisema hakutakuwa na maana ya kujenga majumba marefu ya makazi ya gharama nafuu bila kuhakikisha wakazi wanapata maji. Alisema upinzani umeungana na kudokeza kuwa baadhi ya viongozi wake watahudhuria uzinduzi rasmi wa chama hicho utakaofanyika katika wiki zijazo.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo 17 hours ago
HABARI ZA HIVI PUNDE: Mackenzie matatani tena akipatikana na hatia ya kutesa watoto kikatili
Mahakama ya Watoto imempata mhubiri tata Paul Mackenzie na hatia katika mashtaka sita ya kuwashambulia na kuwafanyia watoto ukatili. Hata hivyo, washitakiwa wenzake 21 wameachiliwa huru dhidi ya mashtaka yote 17 yaliyokuwa yakiwakabili. Uamuzi huo ni wa kwanza wa kuwaachilia huru baadhi ya washitakiwa katika msururu wa kesi zinazotokana na mauaji ya halaiki ya Shakahola. Mackenzie anatumikia kifungo cha miaka 200 jela kwa mauaji ya watu msituni Shakahola. HABARI ZAIDI KUFUATA..
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo 22 hours ago
Pato zuri la karakara za zambarau lamfanya 'kujuta kuhangaikia mahindi' miaka mingi
MUSA Kemei ni mkulima wa matunda ya karakara (passion fruit) eneo la Chai-Moto, Mariashoni, Molo katika Kaunti ya Nakuru. Amekuwa akikuza matunda hayo yenye rangi ya zambarau au 'purple passion' kwa muda wa miaka minane. "Nilikuwa nikilima mahindi kwa zaidi ya miaka 10 kabla ya kuamua kubadilisha na kuanza ukulima huu wa matunda. Hii ilitokana na kupanda kwa gharama za pembejeo za kilimo, kama vile mbolea na mbegu huku nikitumia fedha nyingi kuanzia hatua ya kuandaa shamba hadi kuvuna," anasema. Anasema alikuwa akivuna takriban magunia 15-20 ya mahindi kutoka kwa ekari moja huku akiuza kila gunia la kilo 90 kwa kati ya Sh1,800 na Sh2,500, kulingana na hali ya soko mwishoni mwa mwaka. Katika kila msimu, alikuwa akitumia zaidi ya Sh50,000 kwa shughuli zote kuanzia upanzi hadi kuvuna. Mnamo 2018 alipata motisha kutoka kwa moja wa rafiki zake na pamoja na mkewe walikubaliana kubadilisha matumizi ya sehemu moja ya shamba lao la mahindi ili kupanda matunda hayo. Kwa mtaji wa Sh4,000, aliandaa sehemu ya shamba na kununua miche 150 kutoka kwa rafiki yake, ambaye alikuwa ameiandaa kwenye kitalu, kwa Sh20 kwa kila mche. Fedha zilizobaki alizitumia kwa ajili ya shughuli za upanzi na gharama zingine zikiwepo kulipa wafanyi kazi wa vibarua. Shughuli ya upanzi "Nilichimba mashimo yenye ukubwa wa futi moja, yakiwa na nafasi ya mita moja na nusu kati ya shimo moja hadi jingine katika kila mstari, ili kupata nafasi ya kutosha wakati wa kupulizia dawa, kuweka mbolea, kuvuna, na shughuli nyingine muhimu za usimamizi wa shamba. Wakati wa kupanda, nilichanganya udongo na mbolea ya mifugo niliyokusanya kutoka kwa mifugo wangu," anasema Kemei. Anaongeza kuwa baada ya miezi minne, alipulizia dawa za kuua wadudu, akaweka mbolea ya kukuza mimea huku akipalilia miche yake kwa kuwa mvua ilinyesha ya kutosha. Pia alinunua nguzo za ukubwa wa wastani na kuzitumia kusaidia mimea yake ya matunda ili isidondoke chini wakati matawi yanayobeba matunda yanapokua. Miezi minane baada ya kupanda, Kemei aliweka nyaya kwenye nguzo hizo ambazo zilikuwa zimefikia urefu wa mita mbili hadi tatu kwa kuwa mimea ya karakara hutambaa. Baada ya miezi 10 miti hiyo ilianza kutoa maua. Kemei, 52, alivuna kilo 60 katika mavuno yake ya kwanza baada ya mwaka mmoja na kuziuza kwa Sh100 kwa kilo katika soko la eneo hilo. Wiki mbili baadaye, uzalishaji uliongezeka hadi kilo 150, huku bei ya kila kilo ikipanda hadi Sh120, na katika mavuno ya tatu, kiasi kiliongezeka sana hadi kufikia kilo 200. Alivuna matunda yake kila baada ya wiki mbili na kuona ongezeko la uzalishaji katika kila mzunguko wa mavuno, hasa wakati mvua ilikuwa ya kutosha. Mafanikio hayo katika mauzo yalimpa motisha ya kupanua shamba lake hadi kufikia nusu ekari katika mwaka uliofuata. Anasema kuwa hakuhitaji tena kununua miche kutoka kwa rafiki yake au wakulima wengine wa eneo hilo ili kupanda katika sehemu aliyoongezea ya robo ekari, kwani aliandaa miche yake mwenyewe na kuipanda mwaka wa 2019. Anaeleza kuwa hana majuto yoyote ya kuwekeza katika kilimo cha matunda, kwani mafanikio yake yamemwezesha pia kupanda matunda ya 'tree tomatoes', ambayo kwa sasa yako katika hatua ya kutoa maua na matunda yaliyo katika robo ekari. Kupitia mauzo hayo, ameweza kulipa karo ya shule kwa ajili ya watoto wake na kukidhi mahitaji yake mengine ya kifedha kwa urahisi. Mpango wake ni kupanua shamba lake la matunda ya karakara kutoka nusu ekari hadi ekari moja kufikia mwaka ujao. Hata hivyo, kati ya Novemba na Desemba, mkulima huyo hupata mauzo mazuri na kuvuna zaidi ya kilo 500 kila mwezi, kutokana na mvua ya kutosha inayonyesha katika kipindi hicho. Licha ya uzalishaji mzuri, Kemei anataja uvamizi wa wadudu waharibifu kwenye maua na matunda, kuwa jambo linalosababisha kukauka kwake, hasa wakati wa msimu wa kiangazi kama changamoto kubwa inayowakabili wakulima. "Nimechimba kisima shambani ambacho kinanisaidia kumwagilia matunda yangu maji wakati wa kiangazi. Kwenye kila shina, nimetengeneza mfumo wa chombo ambacho huweka maji, yakisaidia kulisha mmea kwa njia ya matone wakati wa kiangazi," anasema Kemei. Ili kuboresha ujuzi wake wa kilimo, mkulima huyu hushirikiana na maafisa wa kilimo ambao humtembelea mara kwa mara shambani mwake. Kupitia maafisa hao, anajifunza jinsi ya kutengeneza mbolea ya asili kwa kutumia nyasi kavu, majani, na mabua ya mahindi, pamoja na kujifunza kuhusu magonjwa ya mimea na njia za kuyadhibiti. Pia, anajifunza kupitia mtandao na kutembelea wakulima wengine wenye uzoefu katika eneo hilo.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo 23 hours ago
Kaunti 10 zilizopokea kitita kikubwa cha Sh5 trilioni tangu ugatuzi uanze
SERIKALI ya kitaifa itakuwa imetuma jumla ya Sh5 trilioni kwa serikali za kaunti kufikia Juni mwakani, miaka 14 tangu mfumo wa ugatuzi kuanzishwa nchini. Takriban theluthi moja ya fedha hizo zimetengewa kaunti 10 ambazo zimenufaika pakubwa na mfumo huo, zikipokea jumla ya Sh1.6 trilioni kufadhili shughuli za serikali zao na miradi ya maendeleo. Nairobi imepokea kiasi kikubwa zaidi cha fedha hizo, jumla ya Sh240 bilioni, ikiimarisha nafasi yake kama kaunti yenye mgao mkubwa zaidi nchini. Hata hivyo, kwa kuzingatia maeneo ya kijiografia, Kaskazini mwa Kenya ndiyo eneo lililonufaika zaidi, huku kaunti tatu zikiingia katika orodha ya 10 zilizopokea fedha nyingi zaidi. Turkana imepokea Sh167.4 bilioni na kushika nafasi ya pili baada ya Nairobi. Mandera imepokea Sh150.5 bilioni, huku Wajir ikipokea Sh129 bilioni na kushika nafasi ya kumi. Kwa pamoja, kaunti hizo tatu zimepokea Sh447 bilioni, sawa na takriban asilimia tisa ya fedha zote zilizotengewa kaunti. Fedha hizo ni karibu mara mbili ya mgao wa Nairobi, licha ya kaunti hizo tatu kuwa na jumla ya wakazi milioni 2.99 mwaka 2025, ikilinganishwa na milioni 4.9 wa Nairobi, kulingana na takwimu za Shirika la Kitaifa la Takwimu (KNBS). Mkoa wa Magharibi pia umefaidika, huku Kakamega ikipokea Sh164 bilioni na Bungoma Sh140 bilioni. Kaunti nyingine zilizoingia kwenye orodha hiyo ni Nakuru iliyopokea Sh165.7 bilioni, Kilifi (Sh157.3 bilioni), Kiambu (Sh157 bilioni) na Kitui (Sh135.4 bilioni). Kwa jumla, Bunge limetenga Sh5.016 trilioni kwa kaunti zote katika kipindi cha miaka 14. Takriban asilimia 60 ya fedha hizo zimetolewa katika miaka saba iliyopita. Wizara ya Fedha ilisema kaunti zilipokea Sh2.5 trilioni katika kipindi cha miaka sita ya kifedha kuanzia 2020/21 hadi 2025/26. Katika mwaka huu wa kifedha, kaunti zimetengewa takriban Sh503 bilioni, zikiwemo Sh428 bilioni kama mgao wa kawaida wa mapato ya kitaifa na Sh75.7 bilioni kama mgao wa masharti. Kaunti pia hukusanya mapato yao wenyewe kufadhili shughuli za kila siku. Kaunti 10 zilizoongoza kwa mgao zinatarajiwa kuwa zimepokea asilimia 32 ya fedha zote kutoka Wizara ya Fedha kufikia Juni 2027. Kaunti hizo zina takriban wakazi milioni 20, sawa na zaidi ya asilimia 37 ya idadi ya watu nchini. Tume ya Ugavi wa Mapato (CRA) imekuwa ikitumia kanuni mbalimbali kuamua kiasi cha fedha kinachopaswa kutolewa kwa kila kaunti. Vigezo vinavyozingatiwa ni pamoja na idadi ya watu, umaskini, afya, kilimo na gharama za kuendesha serikali za kaunti. Katika kipindi cha kwanza, kuanzia 2013/14 hadi 2016/17, idadi ya watu ilikuwa na uzito wa asilimia 45, huku gharama za kuanzisha na kuendesha serikali za kaunti zikiwa na asilimia 25. Katika kipindi hicho, Nairobi ilipokea Sh48 bilioni, Turkana Sh39 bilioni na Mandera Sh33 bilioni. Kanuni ya pili, iliyotumika kati ya 2017/18 na 2019/20, iliendeleza uzito wa idadi ya watu kwa asilimia 45, huku gharama za msingi za kuendesha serikali zikiwa asilimia 26 na umaskini asilimia 18. Kanuni ya tatu, iliyotumika kuanzia 2020/21 hadi 2024/25, ilizingatia vigezo mbalimbali kwa usawa zaidi. Gharama za msingi zilikuwa na asilimia 20, idadi ya watu asilimia 18, afya asilimia 17, umaskini asilimia 14 na kilimo asilimia 10. Kanuni ya nne ilianza kutumika Julai mwaka jana na itaendelea hadi Juni 2030. Imerudisha uzito mkubwa kwa idadi ya watu kwa asilimia 45, huku mgao sawa ukiwa asilimia 22, umaskini asilimia 14 na pengo la mapato asilimia 13. Katika mwaka wa kifedha uliopita, Wizara ya Fedha ilitoa Sh468.9 bilioni chini ya mfumo huo mpya. Kiambu ilinufaika zaidi kwa kupata nyongeza ya Sh1.8 bilioni, huku Kajiado, Kwale, Vihiga na Laikipia kila moja ikipata zaidi ya Sh1 bilioni. Mabadiliko hayo yanaonyesha jinsi kanuni za ugavi wa mapato zinavyoendelea kuathiri uwezo wa kaunti kufadhili huduma na miradi ya maendeleo.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 25 Nov 2026 05:55:00
Serikali ya Nassir yanusurika kuamriwa kurejeshea wakazi kodi iliyowakata mwaka mzima
SERIKALI ya Kaunti ya Mombasa imeponea mzigo wa kuwarejeshea wakazi na wafanyabiashara kodi na ushuru iliyokusanya kwa kipindi cha mwaka mzima chini ya Sheria ya Fedha ambayo Mahakama Kuu imebaini kuwa ilitungwa kinyume na Katiba. Katika hukumu iliyotolewa Novemba 20, Mahakama Kuu mjini Mombasa ilikiri kuwa serikali ya kaunti na Bunge la Kaunti zilikiuka wajibu wao wa kikatiba wa kuwashirikisha wananchi katika utungaji wa sheria. Hata hivyo, mahakama ilisema kubatilisha ukusanyaji wa mapato ya mwaka mzima kungevuruga utoaji wa huduma za umma. Mahakama ilikataa kubatilisha Sheria ya Fedha ya mwaka 2024 (Na. 6 ya 2024) wala kuamuru kurejeshwa kwa fedha zilizokusanywa, ikisema walalamishi walishindwa kuwataja wasafirishaji au wafanyabiashara waliolipa ushuru uliopingwa na kuwasilisha ushahidi wa malipo hayo. "Kasoro niliyoibaini inahusu utaratibu uliofuatwa. Sijabaini kuwa ada yoyote mahususi ilitozwa nje ya mamlaka ya kaunti," mahakama ilisema. Sheria hiyo ilianza kutekelezwa Januari 1, 2025 na kutumika mwaka mzima. Mahakama ilibainisha kuwa kaunti ilikuwa tayari imetumia mapato hayo kutoa huduma za umma, huku wafanyabiashara wakipata vibali, leseni na huduma nyingine badala ya malipo yao. Mahakama pia iliwakosoa walalamishi kwa kusubiri hadi Aprili 2025 kuwasilisha kesi kupinga sheria ambayo tayari ilikuwa imeanza kutekelezwa, ikisema kuwa kufikia wakati huo wafanyabiashara wengi walikuwa tayari wamelipa. Mashirika mbalimbali ya wafanyabiashara yaliwasilisha kesi hiyo Aprili 2025. Walalamishi walidai kuwa serikali ya kaunti iliwanyima wakazi fursa ya kutosha kuchunguza na kuwasilisha maoni yao kuhusu Mswada wa Fedha kabla ya kupitishwa kuwa sheria. Walisema kaunti ilichapisha tangazo la kuwaalika wananchi kuwasilisha maoni yao Septemba 23, 2024, na kuwapa siku mbili pekee, hadi Septemba 25, kuwasilisha mapendekezo yao. Pia walipinga kikao kimoja cha kusikiliza maoni ya umma kilichofanyika katika Ukumbi wa Jamii wa Tononoka Novemba 14, 2024, wakisema mkutano huo wa saa mbili haukufanyika ipasavyo na haukuweza kuwakilisha kwa njia ya kutosha wakazi wa wadi zote 30 za kaunti. Licha ya zoezi hilo kutofaulu, walisema Bunge la Kaunti liliidhinisha ripoti ya ushirikishwaji wa umma na kupitisha Mswada huo wakati wa kikao maalumu kilichofanyika Desemba 23, 2024. Walalamishi pia walipinga madai kuwa Sheria hiyo ilidumisha viwango vya awali vya ushuru, wakitaja ongezeko la gharama za vibali vya biashara. Walitaja ongezeko la ushuru kwa hadi karibu Sh35,000 kwa baadhi ya biashara. Katibu wa Kaunti, Jeizan Faruk, alipinga kesi hiyo akisisitiza kuwa serikali ya kaunti ilizingatia matakwa ya kisheria kuhusu ushirikishwaji wa umma. Hata hivyo, mahakama ilibaini kuwa washtakiwa walishindwa kuthibitisha kuwa wakazi walipewa fursa ya kutosha kushiriki katika mchakato huo. Mahakama ilikataa hoja kuwa vurugu zilizotokea Tononoka zilihalalisha kusitishwa kwa zoezi hilo, ikisema wakazi ambao hawakuhudhuria mkutano huo hawakupaswa kunyimwa haki yao ya kutoa maoni. Jaji alionya kuwa michakato ya baadaye ya ushirikishwaji wa umma lazima iwe ya maana na yenye kuzingatia maoni ya wananchi, akiongeza kuwa kikao cha kusikiliza maoni kinapovunjika au kushindwa kufanyika, Bunge la Kaunti lazima liitishe kikao kingine.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 25 Nov 2026 04:55:18
Serikali yachunguza madai ya udukuzi wa jukwaa la eCitizen
SERIKALI imeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya shambulizi kubwa la kimtandao dhidi ya mfumo wa eCitizen, huku kukiwa na hofu kuwa taarifa binafsi za Wakenya na data za serikali huenda ziliibwa. Kundi la wahalifu wa kimtandao linalojiita ByteToBreach linadai kuwa lilidukua mfumo huo na kuiba gigabaiti 600 za stakabadhi za taarifa za wateja, gigabaiti 100 za data na gigabaiti 40 za misimbo ya programu za kompyuta. Taarifa hizo ziliibuliwa Jumatatu na kampuni ya Amerika inayohusika na usalama wa kimtandao, Vecert. Kundi hilo pia linadai kuwa liliweza kuingilia mifumo inayowaunganisha Wakenya na huduma mbalimbali za serikali. Hata hivyo, Wizara ya Usalama wa Ndani ilisema kikosi chake cha kiufundi na usalama kinafanya uchunguzi kubaini ukubwa wa tukio hilo. Katika taarifa iliyotolewa Jumanne, wizara hiyo ilihakikishia umma kuwa huduma za eCitizen zinaendelea kupatikana kama kawaida. "Tunashirikiana na mashirika husika ya serikali kukabiliana na tukio hili. Huduma za eCitizen zinaendelea kupatikana na umma unaweza kuendelea kuzitumia kama kawaida," ilisema wizara. Kampuni ya Webmasters Kenya Ltd, inayosimamia jukwaa la eCitizen, iliambia 'Taifa Leo' kuwa suala hilo linashughulikiwa na mashirika husika ya serikali. eCitizen ni jukwaa kuu linalowawezesha Wakenya na wakazi wengine kupata huduma za serikali kupitia akaunti moja. Jukwaa hilo linaunganisha zaidi ya huduma 22,000, zikiwemo maombi ya pasipoti, leseni za udereva, vitambulisho, vyeti vya kuzaliwa na ndoa, vyeti vya tabia njema na usajili wa biashara. Wataalamu wanaonya kuwa iwapo madai ya udukuzi yatathibitishwa, mifumo mingine inayotumia teknolojia ya eCitizen inaweza pia kuwa hatarini. Mtafiti wa usalama wa kimtandao na mkuu wa Cyber Guard Africa, Dkt Bright Gameli, alisema kuingiliwa kwa mfumo mkuu wa habari kama eCitizen kunaweza kuwapa wahalifu njia ya kufikia huduma nyingine zilizounganishwa nao. Kundi hilo limetaja Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA), Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI), Safaricom na Huduma ya Kitaifa ya Polisi kuwa miongoni mwa taasisi zinazoweza kuathirika. Hata hivyo, hakuna taasisi yoyote kati ya hizo iliyothibitisha kudukuliwa. Dkt Gameli alionya kuwa taarifa zilizoibwa zinaweza kutumiwa kufanya wizi wa utambulisho, utapeli na mashambulizi yanayowalenga watu binafsi. Aliwataka Wakenya kuwa waangalifu dhidi ya ujumbe wa ghafla unaodai kuwa nywila zao zimefichuliwa na kuwaelekeza kubofya viunzi ili kuzibadilisha. Kenya imekumbwa na ongezeko la mashambulizi ya kimtandao. Takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano nchini zinaonyesha kuwa mashambulizi dhidi ya mifumo ya tovuti yaliongezeka kwa asilimia 163 hadi milioni 27.4 katika miezi mitatu hadi Septemba 2026, kutoka milioni 10.4 katika kipindi kama hicho mwaka uliotangulia. Wataalamu pia wanaonya kuwa matumizi ya Akili Unde (AI) yanarahisisha wahalifu kubaini mianya ya usalama katika mifumo ya kompyuta. ByteToBreach inaripotiwa kuwa kundi linalolenga kuiba taarifa na kuzitumia kutishia taasisi ili zilipwe fedha, la sivyo taarifa hizo zitangazwe au kuuzwa.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 25 Nov 2026 03:55:22
Sifuna ataka aondolewe kwenye kesi ya kubadilisha jina la chama
SENETA wa Nairobi Edwin Sifuna ameomba Jopo la Kutatua Migogoro ya Vyama vya Kisiasa kumuondoa katika kesi inayopinga kubadilisha jina la chama cha The Equitable Party (TEP) kuwa Linda Mwananchi Movement. Katika pingamizi lake, Sifuna anasema hahusiki moja kwa moja na maamuzi yanayopingwa na mwanachama Emmanuel Willyngtone Khamala, wala mlalamishi hajaomba amri yoyote dhidi yake. Anataka mahakama kutupilia mbali malalamishi hayo dhidi yake pamoja na gharama za kesi. Khamala anapinga hatua za viongozi wa chama kubadilishwa bila kuwashirikisha wanachama ipasavyo. TEP ilizinduliwa katika Hoteli ya Serena jijini Nairobi Oktoba 4, 2026, huku Sifuna akitangazwa kuwa kiongozi wake. Siku nne baadaye, Kamati Kuu ya Kitaifa ya chama hicho iliidhinisha azimio la kubadilisha jina kuwa Linda Mwananchi Movement. Khamala anasema uamuzi huo ulifanywa bila kuwashirikisha wanachama waliosajiliwa, licha ya kuwaathiri moja kwa moja. Pia, anapinga kutangazwa kwa kikosi kipya cha uongozi Oktoba 30, akisema wanachama hawakushauriwa wala kupewa taarifa.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 25 Nov 2026 02:55:55
Wanasiasa washangaza kutoa zawadi zisizo za kawaida ikiwemo chupi
WANASIASA nchini wameanza kutumia mbinu za kipekee kuwavutia wapigakura, huku baadhi ya zawadi wanazotoa zikizua mjadala kuhusu maadili na kampeni za mapema. Ikiwa imesalia chini ya miezi tisa kabla ya uchaguzi huo, wanasiasa hao wanatoa fedha taslimu, vyakula, fulana na kofia zenye majina yao hadi zawadi zisizo za kawaida kama chupi, magodoro na sare za shule, katika harakati zao za kujijenga kisiasa. Ingawa kutoa zawadi kwa wapiga kura si jambo geni nchini, baadhi ya wanasiasa wamevuka mipaka ya kawaida kwa kutoa bidhaa ambazo hazikutarajiwa kuwa sehemu ya kampeni za kisiasa. Tukio la hivi punde lilitokea Novemba 23, wakati mgombeaji wa ugavana wa Kaunti ya Kisii, Kevin Nyamari, alipogawa chupi zenye chapa yake kwa wanawake, hatua iliyozua gumzo kwenye mitandao ya kijamii. Bw Nyamari alitetea hatua hiyo akisema, ilikuwa njia ya kuunga mkono utu na heshima ya wanawake. "Kumpa mtu chupi kunaweza kuonekana kama jambo dogo, lakini hakuna mchango mdogo linapojiri suala la utu. Kujiamini kunakotokana na hilo ni kubwa," alisema. Aliongeza kuwa kujitolea kwake kusaidia watu walio katika mazingira magumu, hasa wasichana na wanawake kumechochewa na huruma na wajibu wa kijamii. Hata hivyo, hatua hiyo ilikosolewa na baadhi ya Wakenya, ambao walitilia shaka ufaafu wa zawadi hizo kwa mwanasiasa anayetarajia kuwania kiti cha ugavana. Mtaalamu wa utawala bora na mwanasiasa, Dkt Peter Mbae, alisema viongozi wanapaswa kuheshimu mipaka ya maadili na badala yake kutoa msaada wenye manufaa ya kudumu. "Wanasiasa wanapaswa kuheshimu mipaka ya maadili na kutoa msaada wa vitendo au kuwawezesha wananchi kiuchumi badala ya kutoa bidhaa za nguo za ndani," alisema. Profesa Tom Nyamache wa Chuo Kikuu cha Turkana, pia alisema wanawake wanahitaji mipango yenye manufaa ya muda mrefu badala ya chupi. Hata hivyo, baadhi ya wakazi walimtetea Bw Nyamari, wakisema kutoa zawadi hizo ni njia bunifu ya kuwafikia wapigakura. Bi Mary Nyanchera, mkazi wa Kisii, alisema hatua hiyo ililenga kuonyesha upendo na kuleta mabadiliko, hata kama mchango huo ulikuwa mdogo. Miezi michache iliyopita, Mbunge wa Ndia, George Kariuki, pia alizua mjadala baada ya kuwagawia wanafunzi sare za shule zilizokuwa na jina lake. Mbunge huyo alisema sare hizo zilinunuliwa kwa pesa zake binafsi baada ya kuguswa na hali ya wanafunzi waliokuwa wamevaa nguo zilizochakaa. Alitetea uamuzi wa kuweka jina lake kwenye sare hizo, akisema hata mashirika ya kimataifa huweka majina yao kwenye misaada wanayotoa. Hata hivyo, wakosoaji walisema hatua hiyo ilikuwa na sura ya kampeni za kisiasa. Mjadala huu unaibua kumbukumbu za uchaguzi mdogo wa Ol Kalou, Kaunti ya Nyandarua, ambapo wanasiasa waligawa mitungi ya gesi iliyopakwa rangi ya zambarau, viatu, magodoro na zawadi nyinginezo zenye chapa zao. Maafisa wakuu wa serikali pia walimiminika eneo hilo, huku miradi mbalimbali ya maendeleo ikitekelezwa kabla ya uchaguzi huo. Hata hivyo, mgombeaji wa UDA alishindwa na Sammy Kamau Ngotho wa chama cha DCP. Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na wakili, Steve Kabita alisema Wakenya wanapaswa kutarajia mbinu zaidi zisizo za kawaida uchaguzi unapokaribia. "Wanasiasa wanajua kuwa hakuna umaarufu mbaya. Tarajieni mbinu nyingine za kushangaza kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka ujao. Watatumia kila kitu kinachoweza kuwapa manufaa ya kisiasa," alisema. Huku hayo yakijiri, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imesema zawadi zenye chapa za wanasiasa si haramu, lakini imewaonya viongozi dhidi ya kuanzisha kampeni kabla ya wakati. Mwenyekiti wa IEBC, Erastus Ethekon, alisema kipindi rasmi cha kampeni kitaanza Mei 29, 2027. "Shughuli rasmi za kampeni zitaanza Mei 29, 2027. Kushiriki kabla ya kipindi rasmi cha kampeni ni kinyume cha sheria," alisema. Katika warsha ya Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) mjini Mombasa, Profesa Patrick Lumumba pia alikosoa mikutano ya kisiasa inayoendelea nchini, akisema viongozi tayari wameanza kampeni kinyume na sheria. Mkurugenzi wa EACC anayesimamia maadili na uongozi, Pascal Mweu, naye alionya maafisa wa umma dhidi ya kujihusisha na kampeni za mapema, akisema hatua hiyo inaweza kukiuka Sheria ya Migongano ya Maslahi. Alisema watakaopatikana na hatia watachukuliwa hatua za kisheria, ikiwemo kushtakiwa mahakamani.
read moreRight Column Content