kenyans.co.ke
@kenyans Sun, 12 Jul 2026 03:44:43
Gachagua Reveals Final Step Before Unveiling United Opposition Candidate
The opposition has maintained that it will field a single presidential candidate in 2027 to challenge Ruto, but the group is now faced with internal wranglings as realignments emerge from within.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sun, 12 Jul 2026 04:55:12
TSC Issues Warning After Striking off Some Teachers from Register
Under Section 30 of the Teachers Service Commission Act, the TSC can permanently remove a teacher's name from the official register for offenses like gross misconduct, fraudulent registration, or criminal convictions.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sun, 12 Jul 2026 05:26:11
Kofi Annan Foundation Sounds Alarm on Kenya Ahead of 2027 General Elections
The warning comes almost a year to the general election, as President Ruto seeks a second term in office, with the opposition also positioning itself to field a single candidate to face Ruto in 2027.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sun, 12 Jul 2026 07:15:24
Protests Erupt Over Diversion of SGR Route
A fresh dispute over the Standard Gauge Railway has reignited old questions about route changes, with residents warning that one decision could deny an entire region the economic benefits they had long been promised.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sun, 12 Jul 2026 09:55:24
Concern as Hundreds of Families are Displaced for Affordable Housing Project
The Affordable Housing Board is currently facing more than 80 court cases, ranging from unresolved land disputes, the absence of title deeds, lack of public participation, and claims over culturally sacred or community land.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sun, 12 Jul 2026 11:05:44
Lobby Group Piles Pressure on IEBC Ahead of Ol Kalou By-Election
Ol Kalou has become a key interest area owing to the July 16 byelections, an event that has witnessed an interesting turn of events that could shape voters' attitude towards the 2027 general elections.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sun, 12 Jul 2026 12:12:30
CCTV Captures Moment Armed Man Ambushes Women Inside Salon
This year, most parts of the country, especially Nairobi City have faced heightened security breaches, which have not just threatened life nut also resulted into lost into valuables worth millions.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 12 Jul 2026 12:33:10
Kitengo kipya cha matibabu ya figo chafunguliwa Hospitali ya Mama Lucy
Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ametangaza kufunguliwa kwa Kitengo kipya kilichopanuliwa cha huduma za figo (Renal Unit) katika Hospitali ya Mama Lucy Kibaki. Ufunguzi huo unalenga kuboresha upatikanaji wa huduma za kuokoa maisha za usafishaji damu (dialysis) na kuimarisha huduma maalumu za afya katika kaunti hiyo. Kitengo hicho cha kisasa, kilichoko katika Hospitali ya Level 5 ya Mama Lucy Kibaki, Umoja II, Embakasi Magharibi, kimewekewa mashine za kisasa na kina wahudumu wenye uzoefu katika matibabu ya magonjwa ya figo ili kutoa huduma kamili kwa wagonjwa. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Gavana Sakaja alisema kitengo hicho kitatoa matibabu ya kina ya magonjwa ya figo, mipango ya matibabu inayolingana na mahitaji ya kila mgonjwa, ushauri wa lishe na mtindo wa maisha, pamoja na huduma za ushauri nasaha na msaada kwa wagonjwa. "Upanuzi wa huduma zetu za figo unaonyesha dhamira yetu ya kuhakikisha wakazi wa Nairobi wanapata huduma bora na nafuu bila kulazimika kusafiri umbali mrefu. Kituo hiki kitaboresha matokeo ya matibabu kwa wagonjwa wanaoishi na magonjwa ya figo," akasema Gavana Sakaja. Gavana huyo alibainisha kuwa kitengo kipya ni sehemu ya uwekezaji unaoendelea wa Serikali ya Kaunti ya Nairobi katika huduma maalumu za afya, unaolenga kupunguza hali ambapo wagonjwa wanaenda hospitali nyingine na pia kuleta huduma bora za matibabu karibu na wananchi. Hospitali hiyo imewahimiza wagonjwa wanaohitaji huduma za matibabu maalumu ya figo kupanga miadi kupitia Kitengo cha Figo kilichotengwa kwa huduma hizo. Uzinduzi huo ni sehemu ya maboresho yanayoendelea katika Hospitali ya Mama Lucy Kibaki, yakiwemo upanuzi wa huduma za wagonjwa mahututi, kumbi za kisasa za upasuaji, idara ya dharura iliyoboreshwa na uwezo ulioimarishwa wa uchunguzi wa magonjwa. Maboresho hayo yanadhihirisha dhamira ya Serikali ya Kaunti ya Nairobi ya kuimarisha miundombinu ya huduma za afya ya umma. Gavana Sakaja pia aliwahimiza wakazi wanaohitaji huduma za matibabu ya figo kutembelea Kitengo kipya cha Figo katika Hospitali ya Mama Lucy Kibaki, iliyoko Kangundo Road, Umoja II. Alisema huduma hizo zinapatikana chini ya mpango wa Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA), hatua itakayorahisisha upatikanaji wa huduma nafuu na bora za dialysis pamoja na matibabu maalumu ya magonjwa ya figo kwa wakazi wa Nairobi.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 12 Jul 2026 11:57:04
Junior Starlets yafuzu kombe la dunia
Timu ya Kenya ya vichuna chini ya miaka 17, Junior Starlets, imefuzu Kombe la Dunia la Mwaka huu, baada ya kuichabanga Afrika Kusini 3-1 katika mechi ya marudiano ya hatua ya mwisho jana ugani Nyayo. Kenya ilifuzu kwa jumla ya mabao 5-1 baada ya pia kushinda mechi ya kwanza 2-0 mjini Pretoria wiki iliyopita. Ushindi huo umeihakikishia Kenya tiketi ya kushiriki fainali zitakazoandaliwa nchini Morocco kuanzia Oktoba 17 hadi Novemba 8, 2026. Hii ni mara ya pili kwa Junior Starlets kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia baada ya kushiriki kwa mara ya kwanza katika makala ya 2024 yaliyofanyika nchini Jamhuri ya Dominika chini ya ukufunzi wa Mildred Cheche. [caption id="attachment_190028" align="alignnone" width="1296"] Wachezaji wa Junior Starlets wakisherehekea baada ya kufunga bao dhidi ya Afrika Kusini na kufuzu Kombe la Dunia la wachezaji chini ya miaka 17 katika uga wa Nyayo jijini Nairobi jana. PICHA |HISANI[/caption] Mechi hiyo ilianza kwa dakika moja ya ukimya kumuenzi mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Jayden Adams, aliyefariki dunia Ijumaa akiwa na umri wa miaka 25. Kocha Cheche alianzisha kikosi kilekile kilichoibuka na ushindi wa mabao 2-0 mjini Pretoria. Mishel Ng'ono alianza langoni huku safu ya ulinzi ikiongozwa na Brendah Awuor, Fleviah Khatenje, Sylvia Namisi na Berveline Awuor. Kiungo kilikuwa na Noelina Akuku, Mwanakombo Bakari na Gaudencia Maloba huku Lindey Weey Atieno na Faith Boke wakimsaidia mshambuliaji Brenda Achieng. Afrika Kusini ilianza kwa kasi na kupata bao la mapema katika dakika ya tano kupitia kwa nahodha Katleho Malebana baada ya safu ya ulinzi ya Kenya kufanya makosa. Dakika tatu baadaye, Kenya ilikaribia kusawazisha baada ya Faith Boke kumpasia Brenda Achieng aliyebaki ana kwa ana na kipa, lakini shuti lake halikulenga lango. Kenya iliendelea kushinikiza na kupata mpira wa adhabu katika dakika ya 15 baada ya Achieng kuchezewa visivyo nje ya eneo la hatari, lakini mpira wa Lindey Weey ulipaa nje. [caption id="attachment_190027" align="alignnone" width="2560"] Kiungo wa Junior Starlets Gaudencia Maloba akisherehekea baada ya kufunga bao dhidi ya Afrika Kusini katika uga wa Nyayo jijini Nairobi jana. PICHA |HISANI[/caption] Afrika Kusini ilipoteza nafasi nzuri ya kuongeza bao katika dakika ya 18 wakati Pilate Moloi alipompita kipa Ng'ono na mabeki wawili kabla ya shuti lake kupita nje kidogo ya lango. Licha ya Kenya kutawala mchezo katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza, ilishindwa kutumia vyema nafasi ilizopata na kwenda mapumzikoni ikiwa nyuma 1-0. Mwanzoni mwa kipindi cha pili, Cheche alimleta Emily Adhiambo kuchukua nafasi ya Lindey Weey, mabadiliko yaliyoongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya Kenya. Starlets waliendelea kulisakama lango la wageni huku Achieng akikaribia kusawazisha katika dakika ya 54, lakini shuti lake liligonga wavu. Shinikizo la Kenya lilizaa matunda dakika ya 70 wakati Gaudencia Maloba aliposawazisha. Kenya iliongeza bao la pili kupitia kwa Awuor aliyefunga kwa mkwaju wa penalti baada ya wenyeji kutunukiwa adhabu hiyo. Mshambuliaji wa akiba Elizabeth Alizeba Achieng alihitimisha ushindi huo katika dakika za nyongeza kwa kufunga bao la tatu na kuiwezesha Kenya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kufuzu kwa jumla ya mabao 5-1. Sasa Junior Starlets wataelekeza macho yao nchini Morocco wakilenga kufanya vizuri zaidi kuliko walivyofanya katika ushiriki wao wa kwanza wa Kombe la Dunia mwaka 2024
read moreRight Column Content