taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 06 Sep 2026 00:55:15
Trump aokoa maelfu ya ajira Kenya kwa kuongeza muda wa Agoa
MAELFUya wafanyakazi katika sekta ya nguo nchini Kenya wamepata afueni mpya baada ya Rais wa Amerika Donald Trump kutia saini sheria ya kuongeza muda wa Mpango wa Fursa na Ukuaji wa Afrika (Agoa) kwa miaka miwili zaidi, hatua inayohakikisha bidhaa za Kenya zinaendelea kuingia katika soko la Amerika bila ushuru hadi Desemba 31, 2028. Uamuzi huo unaokoa takriban ajira 6,600 zilizokuwa katika hatari kutokana na kutokuwa na uhakika kuhusu mustakabali wa mpango huo wa kibiashara. Vilevile, unapatia kampuni zinazouza bidhaa Amerika muda zaidi wa kupanga uzalishaji na kuendelea kuhifadhi wafanyakazi wao. Hatua hiyo inatarajiwa kurejesha imani katika eneo la bidhaa za kuuza nje (EPZ), ambako wawekezaji wamekuwa wakiahirisha maamuzi ya kupanua viwanda na kuwekeza zaidi kutokana na wasiwasi kuhusu hatima ya Agoa. Sekta ya nguo na mavazi nchini Kenya inasaidia ajira zaidi ya 66,000 moja kwa moja katika uzalishaji, usafirishaji, masoko na shughuli nyinginezo. Pia hunufaisha mamia ya maelfu ya watu kupitia ajira zisizo za moja kwa moja na mapato ya familia. "Tulikuwa na wasiwasi na tulikuwa tunafikiria kuwaachisha kazi baadhi ya wafanyakazi wetu kama sheria hiyo isingetiwa saini kwa wakati. Hii ndyio nafuu mkubwa zaidi kwetu," alisema John Mwangu, mfanyabiashara wa mavazi Mombasa anayeuza bidhaa Amerika. Waziri wa Biashara Lee Kinyanjui alikaribisha uamuzi huo akisema umetoa uhakika unaohitajika kwa wauzaji wa bidhaa nje ya nchi na wafanyakazi wanaotegemea soko la Amerika. "Uamuzi wa Rais Donald Trump wa kuongeza muda wa Agoa hadi Desemba 31, 2028 ni wa kupongezwa sana," alisema Kinyanjui. Katika mwaka wa kifedha uliopita, Kenya ilipoteza ajira 5,337 katika maeneo ya EPZ huku nafasi zaidi ya 5,000 za ajira zilizotarajiwa kupatikana kupitia upanuzi wa viwanda zikikwama kutokana na kucheleweshwa kwa maamuzi ya uwekezaji. Agoa ilianzishwa mwaka 2000 ili kuruhusu nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuingiza maelfu ya bidhaa katika soko la Amerika bila ushuru. Mpango huo uliwahi kuongezewa muda mara kadhaa, ikiwemo mwaka 2015 ulipoongezwa kwa miaka 10. Mpango huo uliisha muda wake Septemba 2025 baada ya Bunge la Amerika kukosa kuuongeza kwa wakati, lakini ulirejeshwa kwa muda mwezi Februari mwaka huu hadi Desemba 2026. Sheria mpya sasa imeongeza muda huo hadi mwisho wa mwaka 2028.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sun, 06 Sep 2026 00:20:54
Kenyan Embassy Issues Notice to Kenyans Living or Travelling to Three Countries
The move comes amid growing safety concerns for Kenyan citizens in the three countries, with reports of Kenyans falling victim to job scams and facing other challenges while abroad.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sat, 05 Sep 2026 23:55:13
Uhuru aibuka mwiba kwa Gachagua Mlimani
VITA vya kisiasa vya kudhibiti Mlima Kenya vinaingia awamu mpya huku aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua akijaribu kuimarisha ushawishi wake katika eneo hilo kuelekea uchaguzi wa 2027. Hata hivyo, uwepo wa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta unatatiza juhudi za Gachagua kujitawaza msemaji mkuu wa Mlima Kenya. Mchuano huo unatokea baada ya kuvunjika kwa muungano wa kisiasa uliomsaidia Rais William Ruto kupata uungwaji mkono mkubwa eneo hilo mwaka 2022. Miaka minne baadaye hali imebadilika. Ruto anakabiliwa na malalamishi katika baadhi ya maeneo kufuatia mzozo wake na Gachagua. Gachagua, aliyekuwa naibu wa Ruto hadi alipoondolewa mamlakani Oktoba 2024, amejaribu kutumia masaibu yake kujijenga kisiasa. Lakini safari yake ya kuwa kiongozi asiyepingwa mlimani bado ina vikwazo. Katikati ya hesabu hizo ni Uhuru Kenyatta ambaye ushawishi wake bado ni mkubwa licha ya kujiondoa katika siasa za uchaguzi. Rais huyo mstaafu bado anaongoza Jubilee na ana mtandao pana aliojenga katika miaka yake kumi ikuluni. Uwezo wake wa kuathiri miungano, kuidhinisha wagombeaji na kutoa uhalali kwa makundi mapya unamfanya mhusika muhimu katika siasa za Mlimani na taifa kwa jumla. Ruto aliongeza joto la mzozo huo Alhamisi alipomshambulia Kenyatta akiwa jijini Eldoret. Alimlaumu kwa kufadhili upinzani ili ushindane naye 2027, akidai rais huyo mstaafu alishindwa kutekeleza ahadi zake alipokuwa mamlakani. "Mnajua mfadhili wao (upinzani) na jinsi nilimsaidia alipokuwa mamlakani. Lakini hakutekeleza mpango wa nyumba za bei nafuu, huduma ya afya kwa wote na ufadhili wa elimu kwa watoto wetu. Sasa anafadhili vibaraka wake wa kisiasa dhidi yangu, lakini nitawashinda kwa kishindo!" akasema Ruto. Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba Kenyatta anafadhili Gachagua, ambaye naye hajatangaza vita dhidi ya rais huyo mstaafu. Hata hivyo, kauli za baadhi ya washirika wa Gachagua na ushindani kati ya chama chake cha Democracy for Citizens Party (DCP) na Jubilee ya Kenyatta zimeibua wasiwasi kwamba rais mstaafu anaweza kuwa kikwazo katika juhudi za kinara wa DCP kudhibiti eneo hilo. Mvutano wa hivi majuzi uliibuka kuhusu mpango wa Ruto wa Ruwaza ya 2060. Gachagua amemtaka Kenyatta kukataa kile alichodai ni juhudi za Rais kumpa nafasi ya kuongoza mpango huo. Naibu kiongozi wa Jubilee Jeremiah Kioni alikanusha madai ya kuwepo kwa uhusiano huo. "Wanaojaribu kufanya hivyo, haijalishi ni kina nani, wanafanya juhudi ambazo hazina msingi," alisema Kioni. Vile vile, Kioni alikataa madai kwamba Kenyatta anafaa kuwajibishwa kwa maamuzi ya mawaziri wa zamani waliokubali nafasi katika serikali ya Ruto . Mzozo huo sasa umevuka mjadala wa Ruwaza ya 2060 na kugusa swali kubwa: Nani ataamua mwelekeo wa kisiasa wa Mlima Kenya kuelekea 2027? Kwa Gachagua, fursa ni kubwa. Eneo lililomsaidia kwa kishindo Ruto akashinda mwaka 2022 sasa ni miongoni mwa yale yanayokabili vikali serikali . Mchanganuzi Dismas Mokua anasema hasira dhidi ya serikali imempa Gachagua nafasi ya kuimarisha ushawishi wake. "Changamoto yake ni kubadilisha hasira hiyo kuwa harakati ya kudumu ya kisiasa na kuhakikisha inamnufaisha badala ya kiongozi mwingine," aeleza. Mokua anasema Kenyatta bado ni mhusika muhimu kwa sababu hahitaji kutangaza azma ya kuwania urais ili kubaki kuwa mshawishi. "Chama chake cha Jubilee kinampa jukwaa la kisiasa huku mitandao yake Mlima Kenya na maeneo mengine ikimpa uwezo wa kuunda miungano ," alihoji. Baadhi ya wachanganuzi wanaamini uungwaji mkono wa Kenyatta unaweza kuwa na uzito miongoni mwa wapigakura wanaotafuta njia mbadala ya Ruto na Gachagua. Hali hii inakumbusha kampeni za 2022. Wakati huo Gachagua na washirika wake walimshambulia vikali Kenyatta wakisema aliwageuka watu wake Mlimani baada ya kuvurugika kwa uhusiano wake na Ruto, na kumuunga mkono aliyekuwa kiongozi wa ODM, marehemu Raila Odinga. Ujumbe wa Gachagua ulikumbatiwa na wapigakura Mlima Kenya. Ruto akajitokeza kama kiongozi ambaye angerudisha ushawishi wa eneo hilo serikalini, huku Kenyatta akisawiriwa kama kiongozi aliyepoteza mwelekeo wa maslahi ya watu wake. Mkakati huo ulimsaidia Ruto kuzoa kura tele katika maeneo mengi ya Mliman i. Lakini sasa hali imegeuka. Ruto anakabiliwa na upinzani kutoka kwa baadhi ya wapigakura wao hao, huku Gachagua akijaribu kujionyesha kama chombo ambacho Mlima Kenya unaweza kutumia kurejesha ushawishi wake. Swali ni iwapo Gachagua ataweza kuzuia kiongozi mwingine kujaza nafasi hiyo ya kisiasa. Kenyatta amekuwa mwangalifu zaidi katika kueleza uhusiano wake na Gachagua, ambaye naye kwa upande wake amekuwa akisema atashauriana na rais huyo mstaafu.
read moreRight Column Content