kahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 05 Oct 2026 03:53:25
Trump unveils 'Super Intelligence Force' to oversee AI policy
US President Donald Trump says he has created a new task force focused on artificial intelligence, which will be led by Director of National Intelligence Jay Clayton. The Super Intelligence Force will work to ensure that the US continues to lead in the technologys development and will coordinate the governments engagement with the public, Trump [...] The post Trump unveils Super Intelligence Force to oversee AI policy appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 05 Oct 2026 03:58:17
Brazil election goes to run-off as right-wing Flávio Bolsonaro wins first round
The right-wing Flávio Bolsonaro has won the first round of Brazils presidential election, beating the incumbent left-wing President Lula da Silva. But he did not obtain more than 50% of the votes required to win outright. There will be a run-off vote between these two candidates on 25 October. Flávio Bolsonaro is the son of [...] The post Brazil election goes to run-off as right-wing Flávio Bolsonaro wins first round appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 05 Oct 2026 04:19:29
Walt Mossberg Net Worth
Walt Mossberg is a retired American technology journalist who has a net worth of $6 million. He is best known for his influential career at The Wall Street Journal, where he worked from 1970 until 2013 and became one of the most prominent technology writers in the United States. Mossberg began his career as a [...] The post Walt Mossberg Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 05 Oct 2026 03:55:19
Padri asimulia nyakati za mwisho za waumini wa ajali ya Sultan Hamud
ASUBUHI kabla ya safari yake ya mwisho, Scholastica Ochieng alimwambia kasisi wake, Padri Patrick Maingi, kuwa kukamilisha sala za Novena kulikuwa kumempa amani ya moyoni. Baadaye siku hiyo, alijiunga na waumini wengine wa Kanisa Katoliki la St Mathias Mulumba, Mikindani, Mombasa, waliokuwa wakijiandaa kusafiri hadi Subukia, Kaunti ya Nakuru, kwa Siku ya Kitaifa ya Maombi. Scholastica na mwenzake Ann Mwanthi pia walikuwa wamelipa zaka zao siku chache kabla ya safari. "Hatuitaki kuenda mbele za Mungu tukiwa na madeni. Tunataka kumaliza madeni yetu ili tukienda, twende tukiwa na dhamira safi," waliambia Padri Maingi. Hawakujua hayo yangekuwa miongoni mwa mazungumzo yao ya mwisho. Saa tisa alasiri Ijumaa, Padri Maingi aliwaaga mahujaji 17 wakipanda magari mawili kuelekea Subukia. "Walikuwa na furaha sana na walikuwa wakitarajia safari njema," akasema. Miongoni mwao alikuwa Veronica Ngandi, ambaye alikuwa akijiandaa kufunga ndoa baada ya familia yake kufanya mazungumzo ya mahari Kitui. Padri Maingi alisema Veronica alipanga kuanza maandalizi ya mwisho ya harusi baada ya kurejea kutoka kwa safari hiyo. "Alikuwa anatazamia harusi yake. Aliniambia baada ya hija angeanza maandalizi lakini sasa harusi yake itakuwa mbinguni," akasema. Sarapia, kutoka Taita Taveta, pia alikuwa na furaha kwa sababu alikuwa hajawahi kusafiri mbali na Voi. Hata hivyo, saa chache baadaye, magari hayo yalihusika katika ajali Salama kwenye barabara ya Nairobi-Mombasa na mahujaji wote 17 wakafariki. Padri Maingi alijulishwa kuhusu ajali hiyo na afisa wa trafiki John Mrei, aliyewatambua waathiriwa kutokana na kofia walizovaa zilizokuwa na jina la kanisa. Miili hiyo ilipelekwa Hospitali ya Sultan Hamud, Makueni, ambako ndugu walitambua waathiriwa 14 wanawake na wanaume watatu. Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Dayosisi ya Mombasa Dominic Kimengich alitaka barabara ya Nairobi-Mombasa ibadilishwe na ijengwe kuwa ya njia mbili, akisema eneo la Salama limekuwa hatari kwa wasafiri. Gavana wa Makueni Mutula Kilonzo Junior pia alitaka serikali ichukue hatua za haraka kuzuia vifo zaidi katika eneo hilo hatari.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 05 Oct 2026 03:50:36
Two pupils drown while attempting to retrieve water jerrycan in Tharaka Nithi
Two schoolgirls aged 15 and 13 drowned in Thingithu River in Tharaka West Sub-County, Tharaka Nithi County, while attempting to retrieve a water jerrycan. The deceased were a Grade 9 pupil, and a Grade 7 pupil, police said. According to police, pupils from the school had gone to Thingithu River to fetch water under the [...] The post Two pupils drown while attempting to retrieve water jerrycan in Tharaka Nithi appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 05 Oct 2026 02:55:27
Sifuna sasa afyatuka, azindua chama hatimaye
SENETA WA Nairobi Edwin Sifuna jana alizindua rasmi chama cha The Equitable Party (TEP) atakachotumia katika uchaguzi mkuu ujao baada ya juhudi za kusajili Linda Mwananchi Movement (LMM) kukumbwa na vikwazo vingi. Katika hatua kubwa ya kuimarisha azma yake ya kuwania urais, Bw Sifuna alichukua uongozi wa chama hicho akilenga kubadilisha jina lake ili kifahamike kama Linda Mwananchi Movement. Afisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa (ORPP) mnamo Alhamisi iliidhinisha kuhifadhi jina Linda Mwananchi Movement kwa siku 90, kwa agizo la Jopo la Kutatua Migogoro ya Vyama vya Kisiasa. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Gavana wa Siaya James Orengo, Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi na Seneta wa Kisii Richard Onyonka. TEP ilianzishwa mnamo 2022 na Mkenya anayeishi Amerika, Dkt Gilbert Marava Shanga. Viongozi waanzilishi walijiondoa baada ya mazungumzo baina yao na mrengo wa Linda Mwananchi, na kumkabidhi Bw Sifuna uongozi wa chama hicho. Uzinduzi huo ulifanyika wiki moja tu baada ya Linda Mwananchi kwa kauli moja kumwidhinisha Seneta Sifuna kuwa kiongozi wake na mgombea wake wa urais katika uchaguzi ujao. Katika hotuba yake, Bw Sifuna alizungumzia changamoto walizokumbana nazo katika juhudi za kusajili Linda Mwananchi pamoja na kufukuzwa kwao kutoka ODM. Alishutumu ORPP akisema imekuwa ikitumiwa kama chombo cha kuzuia vyama vya upinzani kufanya shughuli zao. "Tunazindua chama chetu leo kwa sababu nyumba ambayo Baba alituachia ilitekwa," akasema Bw Sifuna, akirejelea marehemu Raila Odinga. Bw Sifuna alisema iwapo serikali itaendelea kuzuia kubadilishwa kwa jina la chama hicho, wataendelea kutumia jina la TEP hadi uchaguzi wa 2027. "Chama kitaendelea na utambulisho wake wa sasa hadi kura zipigwe 2027. Ikiwa wataendelea kuweka vikwazo kama walivyofanya awali, tutaendelea na safari yetu kwa sababu sasa tuna chama," akaongeza. Alisema chama hicho kitalenga kurejesha imani ya Wakenya katika Katiba na utawala wa sheria, huku kikihakikisha makundi yote yanatambuliwa na kupewa nafasi sawa katika uongozi na maendeleo ya nchi. "Siwezi pekee yangu kuunda vuguvugu. Vuguvugu hili ni lenu nyote mliochagua njia ya mabadiliko na ambao mapambano na kujitolea kwenu kumetengeneza safari hii," akasema. Bw Sifuna pia alieleza baadhi ya masuala ambayo anatarajia kushughulikia iwapo atapata nafasi ya kuongoza nchi, akitaja mzigo wa kodi unaowakabili wafanyabiashara wadogo na gharama ya juu ya kufanya biashara. Seneta huyo amekuwa akipata uungwaji mkono mkubwa katika kura za maoni, huku utafiti wa Tifa wa mnamo Julai ukionyesha kuwa angepata asilimia 15 ya uungwaji kitaifa iwapo angewania urais. Hii ilimweka nyuma ya Rais William Ruto pekee, ambaye alikuwa na asilimia 24. Bw Sifuna pia aliwaacha nyuma viongozi wengine wa upinzani, akiwemo kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka. Wakati wa uzinduzi huo, Sifuna aliwataka Wakenya wenye msimamo kama wake kujiunga na vuguvugu hilo. "Huu ni mwito wa umoja, kufanya kazi pamoja, kukua pamoja na kujenga vuguvugu litakalorejesha matumaini tuliyokuwa nayo mnamo 2010 tulipopitisha Katiba yetu. Vuguvugu hili linaanza na jambo moja rahisi; lazima serikali iwafanyie kazi wananchi," alisema. Mbunge wa Suba Kusini, Caroli Omondi, ambaye ni msemaji wa Linda Mwananchi, alisema mipango inaendelea kubadilisha jina la chama hicho ili liakisi sura ya viongozi na wanachama wake. Gavana Orengo naye alisema yuko tayari kuunga mkono mpango wowote wa kuzuia Rais Ruto kuchaguliwa tena. "Uko mahali panapofaa, uko katika vuguvugu linalofaa na una uongozi unaofaa wa kukupeleka katika nchi ya ahadi. Tunawajibika kwa wananchi wa Kenya," akasema Bw Orengo. Seneta Osotsi alisema walifanikiwa licha ya kile alichodai kuwa ni juhudi za serikali kuwazuia kupata chama. "Tuna jina letu, mliona walivyotutesa lakini tulienda kortini na tukawashinda," alisema. Gavana Natembeya alisema Bw Sifuna na wenzake wanafaa kuingia katika mazungumzo na viongozi wengine wa upinzani na kukubali mgombea mmoja wa urais, akisema seneta huyo wa Nairobi ana uwezo wa kumkabili Rais Ruto. Bw Owino aliwataka viongozi hao kudumisha umoja na kuwashtumu baadhi ya viongozi wa ODM kwa kuwafukuza baada ya kutaka mabadiliko. Pia aliwataka viongozi hao kutumia uzoefu wa Gavana Orengo na kumteua kuwa mmoja wa washauri wakuu wa vuguvugu hilo.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Mon, 05 Oct 2026 03:00:00
New dawn: End of long wait as Linda Mwananchi gets Sifuna's 2027 vehicle
Linda Mwananchi has finally found a political home for its 2027 presidential bid, taking over the leadership of The Equitable Party, with Senator Sifuna being the presidential candidate.
read moreRight Column Content